Kuhani Musa Richard Mwacha ni nani?

Kuhani Musa Richard Mwacha ni nani?

Siruhusu MTU yoyote akubaliane na Mimi lakini hili ni Jambo lililonitokea Nina miezi miwili nasali pale hata sijaenda kushuhudia bado.Sina MTU/ kiongozi ninaemfahamu pale baada ya kuumwa muda mrefu nilimshirikisha Rafiki yangu Yuko Mkoani,na matatizo mengine ya binafsi akaniambia niende pale. Kwanza lazima nikiri SIJAWAHI kusali kwenye haya Makanisa sababu sikuwa NAYAAMINI. Baada ya kwenda pale hata ugonjwa uliokuwa unanisumbua Kwa miaka 12 UMEYEYUKA. Ndio maana nasema IMANI Kwanza Mimi yamenitokea na siwezi kunyamaza hata nikiitwa mjinga cha muhimu NIMEPONA.
Kama bado upo hapo washauri pale ocean road kuna wagonjwa wanateseka sana ni vizuri kupita pale na kuwaombea wenye imani wapone warudi majumbani.
 
KKKT tumefundishwa hakuna miujiza ya kizembezembe. Ukichanganya na akili zangu nzuri naamini hawa watu ni wasanii tu. Kama unabisha acha kusimuliwa na watu wengine,jaribu kuingia jikoni kwao ujionee.
 
Ndio maana nimeleta maada hapa ili tusitapeliwe


Kama walikufa lazima ilithibitika kitabibu wamekufa, lazima walipewa nyaraka za kifo na kuzika, lazima wazikaji wapo wakiwemo viongozi wa dini na serikali

Na huo ndio msingi wa mjadala

Sio kukataa au kukubali ukiwa hujui hata unachokikataa wala kukikubali
Cheti makaratasi tu kwenye hii dunia ya sasa anything is possible..............
 
Pale Kuna maombi kulingana na kiwango chako Cha pesa kuna maombi ya laki laki maombi ya Elfu hamsini ,maombi ya Elfu ishirini na n.k

Uliona WAPI maombi kulingana na umaskini au utajiri WA MTU

Unahitaji kiwango Cha juu Cha upumbavu kumuelewa yule tapeli

USSR
Wanaonesha watu wanaoombewa tu, wako wapi waliopona baada ya kuombewa?
 
Miujiza kutendeka sio ishu maana hata shetani ni mtenda miujiza ,MUNGU ni roho kama alivyoshetani , nguvu ya Giza(shetani)na nguvu ya Nuru (MUNGU)

Nvyojua pale Kuna nguvu ya Giza na inatenda KAZI kwa matambiki ya kigiza bila watu kujua

USSR
We know this guy, alikotokea, alivyoanza , mwalimu wake n.k. Tukisema tutamharibia biashara bure.
 
Nope KUHANI Mussa alianziaga Kwa Mzee WA Yesu
Kumbe ulikuwa unamjua, yule tapeli wa imani, ndiko Mussa alikoanzia akiwa mmoja wa vijana wake aliokuwa akiwatumia kwa miujiza ya kupanga. Alipohitimu naye akaenda kuanzisha huduma yake. Utatozwa consultation fee, utajieleza shida zako kisha atatuma vijana wake kina Mussa wanakuja kwako, wakiwa hapo home wewe mwenyeji ukiwaacha sebuleni ndipo wanaweka hirizi fake nyuma ya fridge au sofa au popote. Ukirudi wanasema haya tufanye maombi, ndipo wanajifanya kutoa unabii kuwa kuna kitu kimewekwa na wachawi sehemu fulani humu ndani, wanaenda kukichukua , na wewe unabaki mdomo wazi ukiamini kuwa ni kweli. Miujiza na unanii wote ni kuhusu uchawi tu hakuna kingine ili kutisha watu.
 
Ukitaka kujuwa mambo mengine ni mazingaombwe, ni pale serikali inapowaingilia na wao kuwa wapole. Wangekuwa wanachokiubiri ni cha kweli, mamlaka zingewaogopa. Hii ni biashara, akifutiwa leseni hana cha kufanya pamoja na mbwembwe zote hizo unazoziona. Watu waamke, kinachotafutwa hapo ni hela tu.
 
Natamani kusikia kama naww ni mmoja wa waliokufa ukafufuliwa vinginevyo ni maigizo yakawaida tu
Sio mmoja wapo, ila naamini hivyo. Ikiwa unaamini kuwa Mungu yupo na ndiye muumbaji wa kila kitu, je kwa nini iwe ngumu kuamini anaweza kufufua mtu?


Tatizo kubwa ni kuwa watumishi wa uongo wengi
 
Nimekuelewa sana
Asante. Ingawa hakuna sehemu yeyote Yesu alipokea pesa ili kumponya mtu au kiingilio cha kumuona.

Kingine nisichokipenda ni kutumia vitu kama maji, mafuta, juice au chumvi kama nyenzo ya uponyaji. Hii inakuwaje mtu yupo hapo na mtumishi yupo...kwa nini asiombe kwa jina la Mungu ili amponye? Ingekuwa maji yanaombewa na kupelekewa walio mbali hapo sawa.

Mimi binafsi siwezi kwenda mtumishi anayedai pesa. Never. Kwa sababu hakuna mtu anayemlipa Mungu pesa kulitumia jina lake.

1 Pet 1:18-19 inasema "Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu" bali kwa damu ya Yesu.​

 
Asante. Ingawa hakuna sehemu yeyote Yesu alipokea pesa ili kumponya mtu au kiingilio cha kumuona.

Kingine nisichokipenda ni kutumia vitu kama maji, mafuta, juice au chumvi kama nyenzo ya uponyaji. Hii inakuwaje mtu yupo hapo na mtumishi yupo...kwa nini asiombe kwa jina la Mungu ili amponye? Ingekuwa maji yanaombewa na kupelekewa walio mbali hapo sawa.

Mimi binafsi siwezi kwenda mtumishi anayedai pesa. Never. Kwa sababu hakuna mtu anayemlipa Mungu pesa kulitumia jina lake.

1 Pet 1:18-19 inasema "Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu" bali kwa damu ya Yesu.​

Chakula cha mungu ni sala, hayo mambo ya hela ni ujanja ujanja tu
 
Mimi nampendeaga kwenye mahubiri yake yuko vizuri sana katika kufafanua mambo mbalimbali katika biblia.
Kitu kinachonikwaza kwake ni namna anavyochelewesha ibada bila kujali watu wanatoka mbali mara nyingi nikipita tembeon siku za ijuma ana jumanne utawakuta watu wamezagaa kule had saa saba wanatoka ibadani kweli hii sio salama sana,ajitahidi amalize ibada walau saa mbili na nusu watu wawahi kwao.

Mengine jamaa yuko vizuri sana na nazani ndio maana amepata mafanikio Makubwa kwa muda mfupi an kuwazidi hata waliomtangulia

Kama anafafanua kwa uzuri ni mtumishi mzuri

Kwani hiyo ibada ya jumanne na ijumaa inayisha usiku huwa inaanza asubuhi? Au ni baada ya muda wa kazi ndio watu wanaenda kanisani?
Kwa Dar es salaam mtu ukitoka job uende kimara kwa ibada lazima hiyo ibada iwe inaanza saa moja au mbili
 
Back
Top Bottom