mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
- Thread starter
- #381
Uthibitisho kwamba nyie ni matapeli uko kwenye maandiko matakatifu. Yote mnayoyaeneza huko yako nje ya maandiko. Hayo mashuhuda mnayowadanya watu hata kwa waganga wa kienyeji yanapatikana!
Yataje yale yanayofanyika ambayo yako nje ya maandiko
Halafu nikuulize swali, unaposema mashuhuda yanayofanyika huko hata kwa waganga yanafanyika ulishawahi kusoma biblia walau ujue ya waganga wa kienyeji hayawahi shinda ya Mungu? Kabla ya kuleta blahblah nenda kamuulize Farao atakueleza yaliyomkuta
Kutoka 7: 8 - 12
Bwana akanena na Musa na Haruni, akawaambia, Farao atakaponena nanyi, na kuwaambia, Jifanyieni miujiza; ndipo utakapomwambia Haruni, Shika fimbo yako, uibwage chini mbele ya Farao, ili iwe nyoka.
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama Bwana alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka.
Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao. Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao.
Kama hujui usijitie aibu, tulia ujifunze ndio uongee.