IGWE
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 9,578
- 7,774
..acha ubishi-huyu kuhani wenu ni tapeli tuAkikujibu nitag please
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
..acha ubishi-huyu kuhani wenu ni tapeli tuAkikujibu nitag please
Huko ulaya na MAREKANI wezi kama kina Musa walikuwepo sana ni jambo la muda tu kiwango Cha elimu kikiwa kikubwa jamii itaondkana na haya maupuuzi
USSR
Hayo manufaa kwa manabii hao wa uongo yana gharama trust me ni swala la muda.Itafuteni kweli kwa kusoma neno na sio miujiza!MANUFAA KUPITIA NGUVU ZA GIZA YANA GHARAMA.Kama utapeli ni rahisi hivyo na una manufaa na haukatazwi na sheria za nchi na wewe fanya unufaike[emoji14][emoji14][emoji14]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti eehmganga wa kienyeji aliyechangamka[emoji137][emoji137][emoji137]Sio clips TU dada huyu yupo mitaa ninayoishi namsikia kila siku HASA USIKU ,ni mganga wa kienyeji TU aliyechangamka yesu alitoa Bure, hizi shuhuda ni michongo japo miujiza ipo
USSR
Hata utende maajabu gani lakini bila kuhubiri mtu atubu dhambi na kuwa safi katika moyo/roho yake miujiza hiyo haina faida kwa kuwa ni ya muda na ulaghai kumpoteza kabisa mtu kiimani na kiroho...acha ubishi-huyu kuhani wenu ni tapeli tu
Hata utende maajabu gani lakini bila kuhubiri mtu atubu dhambi na kuwa safi katika moyo/roho yake miujiza hiyo haina faida kwa kuwa ni ya muda na ulaghai kumpoteza kabisa mtu kiimani na kiroho.
“Yesu akawaita, akawaambia, ‘Wafalme wa Mataifa huwatawala,…na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini kwenu ninyi sivyo; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wa kwanza kwenu, atakuwa mtumwa wa wote.” (Luka 22:25; Marko 10:42-44).
Mtumishi wa kweli hajifanyi kama ‘Bwana’ juu ya watu wa Mungu – hajiinui juu ya washirika kama ‘rais’ wa watu. Kumbuka, Bwana Yesu, Mwana wa Mungu, alisema ‘KWENU NINYI SIVYO’. Mchungaji huharibu sura ya Yesu machoni pa watu kama akitawala kama ‘mkuu wa kijiji’ juu ya washirika; ameacha tabia ya Yesu kama anajifanya ‘mkubwa’ kanisani. Hayo yote ni kosa kubwa sana. Kama mchungaji akiwatawala watu kwa nguvu, hapo huonesha yeye hamfuati Yesu. Paulo aliandika juu ya huduma yake, “Si kwamba tunatawala imani yenu; bali tu WASAIDIZI wa furaha yenu… Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu WATUMISHI WENU kwa ajili ya Yesu.” (2 Wakor.1:24; 4:5).
“lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. WALA SI KAMA WAJIFANYAO MABWANA JUU YA MITAA YAO, bali kwa kujifanya VIELELEZO kwa lile kundi.” (Waebr.13:2,3). Inapaswa mtumishi wa Mungu awe kielelezo kwa washirika na siyo kujifanya ‘Bwana’. Bwana Yesu ametufundisha inapaswa awe ‘mtumishi’ au ‘mtumwa’ wa washirika!
Hakuna sababu kumlaumu! “Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe.” (2 Wakor.6:3). Na hata Mungu ni shahidi mwendo wake! (1 Wathes.2:5).
– Mtumishi wa kweli wa Mungu HATAFUTI fedha zako. HATAMANI pesa zako wala hatakulazimisha umpe pesa kwa ajili ya huduma au maombi yake.
“Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.” (Matendo 20:33). Huyu ni mtumishi wa Mungu kwelikweli.
– Mtumishi wa Mungu HATAFUTI kujifanya mtajiri kupitia huduma yake kwako.
UNABII wa KWELI kutoka kwa Mungu Mtakatifu aliye HAI ukifanikishwa na ROHO MTAKATIFU
a) “...Yesu aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama naye Musa alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.”.....Waebrania 3:1-2
b) “Basi sasa, angalieni, mfalme anakwenda mbele yenu; na mimi ni mzee, mwenye mvi; tena, tazameni, wana wangu wapo pamoja nanyi; nami nimekwenda mbele yenu toka ujana wangu hata leo.
Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za BWANA, na mbele ya masihi
wake, nalitwaa ng’ombe wa nani? Au nalitwaa punda wa nani? Au ni nani niliyemdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi.
Nao wakasema, hukutudhulumu, wala hukutuonea, wala hukupokea kitu kwa mkono wa mtu awaye yote.”....1Samweli 12:2-4
c) “Maana unabii haukutolewa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu”.......2Petro 1: 21
d) Waombaji kwa bidii mbele za Mungu aliye hai kama Yesu kristo, Eliya na Anna.....Luka 22:41, Luka 2:36-37 na Yakobo 5:17-18.
e) Wenye huruma kwa ajili ya taifa na watu wake.. “Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka.” ..... Samweli 12:23
f) “Musa akarejea kwa BWANA akasema, Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu. Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao – na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.”......Kutoka 32:31-32
g) “Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia, akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikilize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto…”.........Kumbukumbu 13:1-3
h) “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa - mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! watu huchukua zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.”......Mathayo 7:15-20
i) “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”.........Wagalatia 5:22-23
j) “Wapenzi msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.”..........1Yohana 4:1
k) “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”........Ufunuo wa Yohana 22:18-19
l) “Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”........Ufunuo wa Yohana 22:19
m) Namna ya unabii unavyotokea kupitia kwa mtumishi mwaminifu, asiyejivuna:
“Kisha akawaambia,
Sikizeni basi maneno yangu;
Akiwapo nabii kati yenu,
Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono,
Nitasema naye katika ndoto.
Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa;
Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?”...........Hesabu 12:6-8
n) Tahadhari kwa mtoaji na mpokeaji unabii kwamba usitoe wala usipokee unabii wa uongo: “Ndipo BWANA akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya mioyo yao. Na watu hao, waliopewa unabii na wao, watatupwa nje katika njia kuu za Yerusalemu kwa sababu ya upanga na njaa; wala hawatakuwa na mtu wa kuwazika, wao na wake zao, na wana wao, na binti zao; maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.” ...........Yeremia 14:14,16 na
“Tazama, mimi ni juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema, Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA.”.............Yeremia 23:31-32 halikadhalika “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA. Tazama, mimi ni juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema, Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA.”............Yeremia 23:28,31-32
*Kabla ya Yesu kupaa aliahidi kumtuma Roho mtakatifu kama msaidizi
".....Ukisoma katika kitabu cha Yohana 14:16-17 16 Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa Kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui. Bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”
Utaona hapa YESU kabla ya kupaa aliwaahidi mitume wake atawatumia roho msaidizi kutoka mbinguni na yeye atawaongoza awapeleke mahali alipo yeye mbinguni sababu hakuna mwanadamu atakayeweza kujiongoza yeye peke yake afike mbinguni, njia aliyetutumia YESU ni kupitia roho mtakatifu ambaye ndiye msaidizi wa YESU, na roho huyu yeye huyasimamia yale tu ambayo YESU aliyaelekeza na katika neno la MUNGU lifuatwe kama lilivyo bila kuchanganywa na uongo.
*Shetani naye ametengeneza roho msaidizi kulaghai waumini
Roho msaidizi wa shetani ni roho ambaye katika biblia ya shetani na yeye alicopy hivyo hivyo ila dunia imefungwa macho na kupigwa upofu ila wapo baadhi ya watumishi ambao wanaenda kuonana na shetani uso kwa uso kama baba yao na huku duniani wakijifanya ni watumishi wanaomtumikia MUNGU kumbe ni watumishi wa shetani kabisa na wanamipango ya kuangamiza nafsi za watu ziende jehanamu. Kama nilivyoelekeza katika mafundisho yangu Nabii Hebron nilisema yupo yesu wa uongo na huyu ni shina la shetani na yeye yupo kuzimu ila ile siku ya mwisho na yeye atatoka kimwili kuwapokea wafuasi wake ambao ni wakristo vile vile ambao hawakumfwata YESU wa kweli wa mbinguni sababu na YESU wa kweli na yeye atakubalika na ile siku ya mwisho atawachukua wale walio wakristo wa kweli sasa umeshaelezwa kuwa kama wewe ni mkristo wa uongo siku ile ya mwisho utapokelewa na mkristo wa uongo na kama wewe ni mkristo wa kweli utapokelewa na YESU wa kweli.
Huyu roho msaidizi wa shetani alitumwa duniani kuwasaidia watumishi ambao ni wapinga kristo na ambao wamemsaliti YESU ambao wapo kwa ajili ya kuwapoteza wanadamu wasiende mbinguni. Roho huyu msaidizi ndiye ndiye anayewaongoza na ndipo utashangaa mbona mtumishi anamtaja roho mtakatifu kanisani lakini hawaruhusu kuokoka au wanamtaja YESU lakini hawabatizwi kama YESU au mtumishi anawaombea watu kwa kuwachangisha watu pesa tofauti na neno la MUNGU lisemavyo “umepewa bure, toa bure” unapoona ni tofauti basi sasa uelewe anaongozwa na roho msaidizi wa shetani na ndiyo sababu biblia haifuatwi na umeshajiuliza ni kwa nini biblia inabebwa kanisani lakini inafuatwa kwa kuchanganywa na uongo? Ni sababu huyu roho msaidizi wa shetani yeye siyo mtakatifu ni muongo hiyo ndiyo dalili ya kujua ni roho msaidizi wa shetani.
Jambo hili ni moja ya mambo ambaye alinifundisha YESU aliponipeleka mbinguni tokea 2010 ili nijue ni jinsi gani shetani alivyoiteka ulimwengu na kufanya YESU akose watu wengi wa kwenda mbinguni na shetani akawa ndiyo mwenye watu wengi 98% na YESU akawa na 2% ya watu watakaoenda mbinguni. Hii idadi inatisha natumaini mnazidi kuelewa na kuweza kumrejea YESU wa kweli na kumkataa na kumkana yesu wa uongo hadharani pamoja na roho wake msaidizi aliyemtuma hapa ulimwenguni kote akaweka mizizi yake, sasa ni wakati wake kuporomoka na ni serikali ya mbinguni itafanya hiyo kazi na wataendelea mpaka atakapokuja YESU kulinyakua kanisa takatifu yaani mkristo wa kweli. Kama ilivyo kazi za roho mtakatifu zilivyo na yeye roho msaidizi wa shetani hufanya hivyo hivyo mfano kazi ya roho mtakatifu ni kusimamia kweli ya neno la MUNGU lifuatwe, roho huyu wa shetani. Roho huyu wa shetani hulipindua pindua mfano; tazama ubatizo aliobatizwa YESU katika mto je ndiyo batizo wakristo wanazofuata? Hapo uelewe roho msaidizi wa shetani ndiye anayewaongoza na siku ile ya mwisho atawakabidhi hao watu kwa shetani na watu hawajui jambo hili. Ameintuma YESU, amenituma MUNGU, amenituma ROHO MTAKATIFU wa kweli, ninaeleza ukweli utakayesikia na kugeuka utapona ila utakaye ng’ang’ana huyo roho msaidizi wa shetani atakupeleka jehanamu; yeye kazi yake ni kuwapeleka watu jehanamu ndiyo kazi aliyetumwa na shetani, ni jinsi gani utamjua au kumtambua kuwa ni roho msaidizi wa shetani ndani ya kanisa au ndani ya mtumishi yeyote yule.
Jambo la kwanza kabisa nataka uelewe haitwi kwa jina lake kuwa ni roho msaidizi wa shetani yeye anatajwa kama roho mtakatifu ila utamjua kwa matendo anayoyaongoza huyo anayeitwa roho mtakatifu. Utayaona ni kinyume na neno la MUNGU mfano wa kufuata matendo baadhi yanayofanywa makanisani katika sehemu baadhi.
1. Kubatizwa kwa maji ya kikombe, kubatizwa katika kisima, kubatizwa kwa jina la mchungaji, kubatizwa ubatizo tofauti na wa mtoni, maji tele yanayotembea (hapa ni roho msaidizi wa shetani anayetia nguvu na watu humfuata. Batizo hizo siyo za haki mbele za MUNGU na siku ile ya mwisho shetani atamwambia MUNGU wewe ni wa haki je kwa nini wamepokea kinyume na neno lako? Sijui utamjibuje MUNGU.
2. Unapopewa huduma ya maombezi halafu ukachajiwa pesa hapo uelewe siyo roho mtakatifu anayewaongoza kabisa kabisa, bali ni roho msaidizi wa shetani anayempa nguvu hizo na pia nataka uelewe roho huyu msaidizi na yeye ananena vile vile na hapo watu wengi wamepigwa upofu wanaona ni MUNGU.
3. Kuwa mkristo halafu hataki kuokoka bali kung’ang’ania kujiita mkristo na hautaki wokovu, watu wa namna hiyo wanashikiliwa na roho msaidizi wa shetani na ndiye anayewaongoza na kuwapa mioyo migumu hata madhabahu za jinsi hiyo nataka uelewe zinaongozwa na roho msaidizi wa shetani ili awaongoze kwenda jehanamu sababu hata wewe soma katiba ya MUNGU yaani neno lake hayo hayapo yamekatazwa ila katika katiba ya shetani yapo. Yametolewa katika ulimwengu wa roho yafuatwe na yamefuatwa sana na jinsi unavyoyafuata ndivyo unavyojiunganisha zaidi na safari ya kwenda jehanamu. ..."
Mimi ni msikilizaji wa wahubiri wengi wa imani na madhehebu tofautitofauti
Na naweza kusema bila kificho wala kupepesa macho kwamba Kuhani Musa Richard Mwacha ni Kati ya watumishi wachache wachache wanaokemea uovu waziwazi na kuishi kile wanachokihubiri
Unatambua kwamba hata kuzimu kuna yesu ambaye anaandaliwa siku ikifika naye ajitokeze akisema yeye ndio yesu huku akitenda matendo makuu?
Soma vizuri nilichokielezea namna ya kumtabua pasi na shaka kwa kurejea neno takatifu la Mungu aliye hai na kumsikiliza Roho mtakatifu ndio atakuthibitishia nani ni nani!!!
Shetani ana akili kuliko za kwako na ana uwezo wa kutambua unachowaza, unachotarajia kutenda na kuingia kwako kwa upenyo wa ulimwengu wa kiroho ambao mpaka umekombolewa ndio utabaini
Imani ni ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu; ni ile hali ya akili ya mtu kupokea ukweli uliofunuliwa na Mungu akiambatanisha nafsi yake kwa Mungu.
Kuhani Musa Richard Mwacha amejulikana kama mtumishi wa Mungu mwenye imani kwa Kristo. Na amekua na huduma yake katika jiji la Dar es salaam kwa miaka michache sasa.
Ukifuatilia ni muda mfupi tangu aanze huduma ila utakutana na mambo mengi sana na kati ya hayo mengi ni style ya mahubiri yake, miujiza na maajabu kwenye ibada zake na idadi kubwa ya waumini alionao ndani ya muda mfupi sana maana miaka 3 au mi4 bado huduma ni changa.
Watu wengi tunajiuliza mengi sana juu ya mtumishi huyu. Wengi wetu hatuamini kama yanayonekana kuotokea ni ya kweli lakini pia wapo wanaoamini ni kweli.
ILA SWALI MOJA LA MSINGI "KUHANI MUSA NI NANI HASWA?
Shuhuda zimetolewa hadharani, na ni shuhuda zinazodhihirisha mambo magumu kufikirika katika hali ya kawaida. Ila hawa walioshuhudia wapo kati yetu, mtaani kwetu hata majumbani kwetu, kigoma, chato, kilimanjaro, sumbawanga, kagera, Dar es salaam mmetisha sana. Wenyeji wa huko mnasemaje kuhusu Kuhani Musa?
Fred William Rwegasira.
View attachment 2123813
Mr Rwegasira ni mzaliwa wa mkoa wa Kagera, Bukoba kule, Mkazi wa Salasala - Dar es salaam. Na sasa anaishi kimara
Innocent Carol Paulo
View attachment 2123832
Innocent Carol Paulo ni mzaliwa wa Chato. Na mkazi wa Tabata - Dar es salaam
Levina Lyamuya na mdogo wake
View attachment 2123876
Levina ni mwenyeji wa Kilema, Moshi- Kilimanjaro
Malkia
Wakorinto
KUHANI MUSA RICHARD MWACHA NI NANI??