MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Nimeshuhudia watu wakipona kwa waganga wa kienyeji, wapo waliopona kwa mashekhe! Kwanini nishangae uponyaji kwa wanaojiita manabii? Hata Kristo alisema atawakana bila kujali walifanya nini kwa jina lake! Soma hii...
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
Mathayo 7:22
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Mathayo 7:23
Onyo! acha kuvutwa na miujiza badala ya neno ambalo ndio Kristo mwenyewe! Usirukie wimbi la kiroho bila kupima na kuongozwa na Roho Mtakatifu!
Mimi nafahamu wengi wakiwemo ndugu wa karibu wanavyohangaika na haya makanisa! Walituimbia tuokoke wakiwa kwa Kakobe, Gwajima, Mwamposa na sasa wapo huko kwa kuhani Musa! Mbaya zaidi maisha yao ni yale yale! Wengjne wamefungua na makanisa wanahangaika huko na watu!
Wengine tuliamua kukaa bila kuyumbayumba Kanisa Katoliki! Mawimbi yakija tunakimbilia kitubio, tunaabudu Ekaristi, hudhuria misa na jumuiya, kutii maagizo ya Kanisa! Upendo kwa jirani na kusaidia wenye huhitaji! Ukipata kidogo unatoa Zaka! Maisha yanaenda salama na amani! Tutulie kwa Bwana kwenye Kanisa lako na kutii badala ya kurukaruka kutafuta overnight miracles!