Kuhusu Katiba Mpya: Hoja ya Rais Samia haina mashiko

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.

Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, hoja ya Katiba Mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo:

1. Katiba mpya haizuii kujenga uchumi
Rais anaposema eti tumpe muda ajenge uchumi kwanza ndo afikirie Katiba Mpya, tungependa kumueleza Rais kuwa kuwa na katiba mpya hakumzuii yeye au Serikali yake kujenga Uchumi, Labda Rais atueleze, je Katiba bora iliyo nzuri inazuiaje yeye kuvutia wawekezaji, inazuiaje kuboresha utalii, inazuiaje kujenga miundo mbinu? Hapa kimsingi Rais hana hoja yenye mashiko kabisa juu ya kukataa kuwapa wananchi aina ya Katiba wanayoitaka.

2. Mchakato wa Katiba Mpya si hisani ya Rais bali ni hitaji la kisheria
Ipo sheria ya mwaka 2012 inayo-govern Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya, Sisi wananchi tunamtaka Rais atekeleze Sheria hiyo, asifanye hili suala kama hisani yake binafsi, hili ni hitajio la wananchi wengi.

3. Hofu ya Rais ni ya kisiasa na si kimaslahi ya kitaifa
Kauli ya Rais ya kukataa kuipa Katiba kipaumbele ilianza kwenye awamu ya tano ambayo yeye alikuwa Makamu wa Rais, Rais wa wakati huo na yeye alisema hoja hizohizo za kujenga uchumi kwanza kabla ya kuleta Katiba Mpya, leo hii tuna miaka mitano bado tunapigwa kalenda hizohizo za ngoja tujenge uchumi. Huhitaji kuwa genius kuona kwamba hofu ya viongozi hawa ni hofu za kisiasa tu, za kuhofia hatma zao na vyama vyao kisiasa iwapo Taifa litapata Katiba Mpya, ni dhahiri wahafidhina ndani ya CCM hawataki Katiba Mpya, lakini kama alivyowahi kusema Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Hoja ya Katiba Mpya haitakufa mpaka ipatikane.

4. Kujenga Uchumi bila kuwa na Katiba ya kuulinda ni kazi bure
Hii katiba tuliyonayo inampa Rais Mpya power za kuvunjilia mbali mafanikio ya Serikali zilizopita, anaweza kusitisha mradi wa kimkakati, anaweza kuingia mikataba ya siri isiyo na faida, anaweza kutapanya rasilimali zetu na asishtakiwe. Kwa hiyo ni dhahiri hata ujenge uchumi mzuri kivipi, bila Katiba nzuri huwezi kuulinda Uchumi huo, ndiyo maana hitajio letu la Katiba Mpya ni muhimu sana.

5. Watanzania hatuko tayari kurudi katika utawala wa kidikteta aina ya awamu ya tano
Ktk utawala wa awamu ya tano tuliona matendo ya kinyama na kiuonevu yaliyofanyika, sababu mojawapo ya matendo hayo ni kuwa na Katiba inayotoa mwanya mtawala kuvunja sheria bila consequences ikiwemo kushtakiwa, Katiba hii imetoa mamlaka makubwa kwa Rais, na kiukweli ni Katiba ya kidikteta, Hatuwezi kuruhusu scenario ya kupata aina ya uongozi wa awamu iliyopita, na guarantee bora ya kutofika huko ni Katiba Mpya na si maneno matamu tu ya Rais Samia.
 
Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.
Mumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi? Wananchi wengi, tunataka uchumi, tupate mkate wetu wa leo na kesho, mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa, sisi wananchi bora mkono uwende kinywani. Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi, hata kwa kupiga kura, kwenye maeneo yenu.
 
Kwa nini wanasiasa, hamuwaulizi wananchi, nyinyi mwataka Katiba mpya, wakati wananchi, twataka mkono uwende kinywani. Nyinyi wanasiasa mwatetea upande wenu, hamtaki kuwasikiza wananchi wanataka nini.
 
Nani anataka kupiga kura yake ya kuchagua Rais, Mbunge au diwani kisha kura hiyo ikaibiwa kwa mtutu wa bunduki? Chama kiko madarakani kwa miaka 60 sasa kimefanya lipi katika kuboresha uchumi wa nchi katika hiyo miaka 60?

Ajira hakuna graduates wanasaga lami, elimu yetu ni ya hovyo sana, matibabu pia ni hovyo sana, usafiri pia ni hovyo sana. Mishahara ya wenye ajira ni ya chini mno miaka sita sasa bila nyongeza. Hebu tia akili kichwani japo KIDUCHU badala ya KUKURUPUKA.

Mumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi?.Wananchi wengi,tunataka uchumi,tupate mkate wetu wa leo na kesho,mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa,sisi wananchi bora mkono uwende kinywani.Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi,hata kwa kupiga kura,kwenye maeneo yenu.
 
Nani anataka kupiga kura yake ya kuchagua Rais, Mbunge au diwani kisha kura hiyo ikaibiwa kwa mtutu wa bunduki? Chama kiko madarakani kwa miaka 60 sasa kimefanya lipi katika kuboresha uchumi wa nchi katika hiyo miaka 60? Ajira hakuna graduates wanasaga lami, elimu yetu ni ya hovyo sana, matibabu pia ni hovyo sana, usafiri pia ni hovyo sana. Mishahara ya wenye ajira ni ya chini mno miaka sita sasa bila nyongeza. Hebu tia akili kichwani japo KIDUCHU badala ya KUKURUPUKA.
Wanasiasa, mjuwe sisi wananchi, hatutaki madaraka yoyote kwenye siasa, kwetu sisi twahitaji mkono wende kinywani, tukishapata mahitaki muhimu, hatuna zaidi ya hapo.
 
Kwa taarifa yako mimi si mwanasiasa lakini nataka kuona Tanzania yenye Utawala bora utawala wa sheria. Tanzania yenye chaguzi zilizo huru na haki na Watanzania tukawa na uhuru wa kuchagua madiwani. wabunge na Rais tuwatakao bila ya kura zetu kuibiwa kupitia mtutu wa bunduki na ile Tume FAKE ya uchaguzi. Tumechoka na chama kung’ang’ania madarakani kwa miaka 60 kwa mtutu wa bunduki huku wakiwa hawana jipya.

Wanasiasa,mjuwe sisi wananchi,hatutaki madaraka yoyote kwenye siasa,kwetu sisi twahitaji mkono wende kinywani,tukishapata mahitaki muhimu,hatuna zaidi ya hapo.
 
Back
Top Bottom