Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.
Ningependa kumkumbusha rais Samia kuwa, hoja ya katiba mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo
1. Katiba mpya haizuii kujenga uchumi.
Ujinga wako unakusaidiaJe ?!Poleni sana maana mlikurupuka nyote michadema
Huyu mama ni dikteta. Anajitia kutumia sauti laini lkn ana tamaa ya madaraka pia. She is a cheetah in sheep skin.Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.
Hii katiba ya kidikteta anayotawala kwayo, akiamua kukunjua makucha tu tunaumia vibaya mno na huwezi kumshitaki popote maana katiba inamlinda!Tumsaidie Mama kuhakikisha katiba inaheshimiwa.
Mengine haya mbona ya kawaida? Tulitegemea atwambie kesho mambo ya katiba, rasmi?
Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.
Mkuu tulitegemea mama anatupa ratiba ya mikutano ya siasa na katiba mpya?
Haya ni ya kupigania:
Tumsaidie Rais Samia kuijenga nchi hii
Mabibi na mabwana, Mama Samia anahitaji uungwaji mkono katika kuijenga nchi hii. Mama ni muungwana na anayo nia ya dhati ya kuiendesha nchi kwa mujibu wa katiba. Pamoja na yote anayosema na nia yake njema ya kufanana na JPM, mama ameonyesha kwa vitendo kuwa si katika dhuluma wala katika kuvunja...www.jamiiforums.com
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.
Ningependa kumkumbusha rais Samia kuwa, hoja ya katiba mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo
1. Katiba mpya haizuii kujenga uchumi.
Rais anaposema eti tumpe muda ajenge uchumi kwanza ndo afikirie katiba mpya, tungependa kumueleza rais kuwa kuwa na katiba mpya hakumzuii yeye au serikali yake kukjenga uchumi, Labda Rais atueleze, je katiba bora iliyo nzuri inazuiaje yeye kuvutia wawekezaji, inazuiaje kuboresha utalii, inazuiaje kujenga miundo mbinu?. Hapa kimsingi rais hana hoja yenye mashiko kabisa juu ya kukataa kuwapa wananchi aina ya katiba wanayoitaka.
2. Mchakato wa katiba mpya si hisani ya rais bali ni hitajio la kisheria
Ipo sheria ya mwaka 2012 inayogovern mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya, Sisi wananchi tunamtaka rais atekeleze sheria hiyo, asifanye hili suala kama hisani yake binafsi, hili ni hitajio la wananchi wengi.
3. Hofu ya rais ni ya kisiasa na si kimaslahi ya kitaifa
Kauli ya rais ya kukataa kuipa katiba kipaumbele ilianza kwenye awamu ya tano ambayo yeye alikuwa makamu wa rais, rais wa wakati huo na yeye alisema hoja hizohizo za kujenga uchumi kwanza kabla ya kuleta katiba mpya, leo hii tuna miaka mitano bado tunapigwa kalenda hizohizo za ngoja tujenge uchumi. Huhitaji kuwa genius kuona kwamba hofu ya viongozi hawa ni hofu za kisiasa tu, za kuhofia hatma zao na vyama vyao kisiasa iwapo Taifa litapata katiba mpya, ni dhahiri wahafidhina ndani ya CCM hawataki. katiba mpya, lakini kama alivyowahi kusema katibu mkuu mstaafu wa CCM, Hoja ya katiba mpya haitakufa mpaka ipatikane.
4. Kujenga uchumi bila kuwa na katiba ya kuulinda ni kazi bure
Hii katiba tuliyonayo inampa rais mpya power za kuvunjilia mbali mafanikio ya serikali zilizopita, anaweza kusitisha mradi wa kimkakati, anaweza kuingia mikataba ya siri isiyo na faida, anaweza kutapanya rasilimali zetu na asishtakiwe. Kwa hiyo ni dhahiri hata ujenge uchumi mzuri kivipi, bila katiba nzuri huwezi kuulinda uchumi huo, ndiyo maana hitajio letu la katiba mpya ni muhimu sana
5. Watanzania hatuko tayari kurudi katika utawala wa kidikteta aina ya awamu ya tano
Ktk utawala wa awamu ya tano tuliona matendo ya kinyama na kiuonevu yaliyofanyika, sababu mojawapo ya matendo hayo ni kuwa na katiba inayotoa mwanya mtawala kuvunja sheria bila consequences ikiwemo kushtakiwa, Katiba hii imetoa mamlaka makubwa kwa rais, na kiukweli ni katiba ya kidikteta, Hatuwezi kuruhusu scenario ya kupata aina ya uongozi wa awamu iliyopita, na guarantee bora ya kutofika huko ni katiba mpya na si maneno matamu tu ya rais Samia
Hii katiba ya kidikteta anayotawala kwayo, akiamua kukunjua makucha tu tunaumia vibaya mno na huwezi kumshitaki popote maana katiba inamlinda!
Somo tulilopata kwa JPM tunapaswa kulizingatia sana, huu urais hauna guarantee, leo yupo kesho anaweza asiwepo. Kwa hiyo vitu vya msingi kama katiba mpya na nzuri huwezi kuviweka kiporo!
@BAK uko vizuri [emoji851][emoji851][emoji851]Kwa taarifa yako mimi si mwanasiasa lakini nataka kuona Tanzania yenye Utawala bora utawala wa sheria. Tanzania yenye chaguzi zilizo huru na haki na Watanzania tukawa na uhuru wa kuchagua madiwani. wabunge na Rais tuwatakao bila ya kura zetu kuibiwa kupitia mtutu wa bunduki na ile Tume FAKE ya uchaguzi. Tumechoka na chama kung’ang’ania madarakani kwa miaka 60 kwa mtutu wa bunduki huku wakiwa hawana jipya.
Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.
Kwa hiyo meko aliwaletea katiba?Hatokuja kufanikiwa kuzuia huu mchakato we muache tu akamuulize Meko huko alipo
Mtafanya nini sasa?Kuna watu wanataka kumdanganya au anatikisa kiberiti tu.
Endeleeni kudemkaRais kutuzuia wananchi kutaka namna ya kuongozwaje hiyo ni dharau kubwa ya rais na chama cha mapinduzi kwa wananchi.
Hilo ni jambo ambalo hatuwezi kulikubali!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Yani wewe ndio sijuagi unasimamia nini!Tumsaidie Mama kuhakikisha katiba inaheshimiwa.
Mengine haya mbona ya kawaida? Tulitegemea atwambie kesho mambo ya katiba, ni rasmi?
Mimi nilisema Mkuu Maza sina imani naye sasa maneno yangu yametimia Mkuu.
Hilo linajulikana na hapa ndipo tunapokuwa wazi:
Tumsaidie Rais Samia kuijenga nchi hii
Mabibi na mabwana, Mama Samia anahitaji uungwaji mkono katika kuijenga nchi hii. Mama ni muungwana na anayo nia ya dhati ya kuiendesha nchi kwa mujibu wa katiba. Pamoja na yote anayosema na nia yake njema ya kufanana na JPM, mama ameonyesha kwa vitendo kuwa si katika dhuluma wala katika kuvunja...www.jamiiforums.com
Mama kazungukwa na wahafidhina.
Tumsaidie kuiheshimu katiba.
Kwamba ukiwa na katiba mpya kila kitu kitakuwa kimenyooka ni kujidanganya.
Kwamba upigaji utaisha kabisa tukiwa na katiba mpya ni kujidanganya.
CCM imejichimbia sana ni vigumu kukubaliana na mabadilko makubwa ya kisiasa yatakayoipunguzia uhalali wa kuongoza nchi.
Lakini utafutaji wa katiba ni mchakato wa wapambanaji kutochoka kuuamini.