Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Subri apigwe na ugonjwa tu kama wa kisukari, kansa au figo uone kama ataendelea na ngonjera zake hapo juu.

Wewe hauwezi hata jiongezea japo umri ufikishe miaka 200, halafu unaanza kuvimba dhidi ya aliyeviweka vyote hivi tunavyoviona na tusivyoviona.

Hizo imani zote lengo mama ni kumuabudu na kumtafuta Mungu mkuu muumba wa vyote ingawa zinatofautiana utaratibu, hivyo inawezekana wote wakawa sahihi.
Hatukatai but Mungu yupi??,maana kila jamii ina Mungu wake.
 
Okay,..kwa majibu haya uliyotoa.., watu wenye akili timamu wakisema una ubishi usioingia akilini.....utawakatalia?

Kwa majibu hayo uliyotoa inathibitisha wazi kwamba umejipanga kubisha tu hata uletewe ukweli ulio wazi.

NB:- Nasema hivyo kwasababu akili yenye afya njema haiwezi kukataa uwepo wa designs tofauti tofauti kwenye viumbe hai, Dunia na ulimwengu kwa ujumla.
Mkuu huo uthibitisho wa uwepo wa design toafuti tofauti ya Dunia unaupata wapi au kutoka kwa nani?.sio vyote vina uthubitisho. Vitu ambavyo ni man made utapata uthibitisho wa design,je vitu ambavyo sio man made-kama wanyama,milima,miti,bahari,maziwa, upepo,joto,na baridi utajuaje ni design au sio design na kama ni design ni nani anathibitisha?.
So,vitu ambavyo sio man made yamkini vilitokea tu au vilitengenezwa ila hakuna uthibitisho-hivyo huwezi jua kama vina design au havina design.
 
Unamaanisha nini unapotaka reference kwenye macho kuona design?

Akili yenye afya ikiona Tunda La Nanasi na
Unadhani kama Mungu yupo atakua anahitaji kuprove chochote? Unafikiri atapata hasara yoyote au faida yoyote ukimheshimu au ukimjua? No.

Kama yupo na kama amefanya yote hawezi kuhitaji chochote kwetu, zaidi sana tunahitaji kutoka kwake
Mungu yupi sasa unamzungumzia,Duniani kuna jamii nyingi ya watu na kila jamii ina Mungu wake.sasa hapa wewe unamzungumzia Mungu yupi???

At least 18,000 different gods, goddesses and various animals or objects have been worshipped by humans.
 
Nitafute nikupe siwezi kukuelezea tu hapa ukaelewa coz hata mimi nilikua kama wewe Mwaka jana tu nilibadiliasha gear angani,
Kiufupi nilishafikia kua Senior Atheist humu humu ila kutokana na kuchimba ukweli kuhusu accient civilization na high advanced tech ya kale nikaja kuingia 18 za Ulimwengu wa Roho (Spiritual Realm)
Nikaja pata mambo makuu yaliyonibadilisha mtazamo na sikuona aibu kurudi hapa JF na nikakiri kua nilikua sina maarifa na kama ulikua mfuatiliaji wa nyuzi zangu za maswala ya Accient civilization utajionea namna gani nimebadilika,
Now natambua Ulimwengu wa Roho unavyo endesha mambo makubwa na maendeleo na tafiti soon nitakuja dondosha uzi hapa namna gani Spiritual Realm inaendesha mambo yake na athari zake nitqkukaribisha katika hiyo thread!
Ulimwengu wa roho ni vitu visivyothibitika,kama unaendesha mambo makubwa ni hisia zako ndio zinakutuma hivyo.hakuna uthibitisho katika hilo.
 
Hakuna contradiction hapa kitu kama hukioni wewe Sio kila mtu hakioni au hakipo
Hata ungerudi Mwaka 1420 na kamwambia Vasco Da Gama kwamba tunaweza kutoka Portugal to India kwa chombo kinachopaa angani kwa masaa tu tunafika atakuona Mwendawazimu na unajicontradict unavyompa formula zake,
Hata huu umeme unatumia ukirudi Mwaka 1677 ukamwambia George Washington kwamba unaexist atakuona punguani ila haimanishi kitu ambacho hukioni wewe hakipo ila inahitaji formula kukiona kinaexist hapo ndipo siri ya maarifa inaanzia
Fungua ubongo tukupe maarifa vitu tunavyoexiperince wenzio bila hivyo utakua gizani na utajionea na maarifa na hoja kumbe bado kindergarten kuhusu mifumo ya vitu vingi!
Mkuu emu kunywa kwanza maji,halafu usome ulichoandika.
 
Mkuu huo uthibitisho wa uwepo wa design toafuti tofauti ya Dunia unaupata wapi au kutoka kwa nani?.sio vyote vina uthubitisho. Vitu ambavyo ni man made utapata uthibitisho wa design,je vitu ambavyo sio man made-kama wanyama,milima,miti,bahari,maziwa, upepo,joto,na baridi utajuaje ni design au sio design na kama ni design ni nani anathibitisha?.
So,vitu ambavyo sio man made yamkini vilitokea tu au vilitengenezwa ila hakuna uthibitisho-hivyo huwezi jua kama vina design au havina design.
Unapouliza kwamba uthibitisho wa designs tofauti tofauti unaupata wapi, unaonyesha wazi kwamba hujaelewa maana ya design...........Tunaposema kuna designs tofauti tofauti kwenye Viumbe hai na ulimwengu (Universe) kwa ujumla tunamaanisha vitu mbalimbali tunavyoviona ambavyo vina sifa tofauti kwenye muundo, rangi, ladha, mwendo, size, mvuto, matumizi na kadhalika.


Kwa mfano, Macho yako mawili na figo zako mbili hazifanani,..Kwanini? kwasababu figo na macho zina muundo, size na hata matumizi na kazi tofauti,. hivyo tunasema viungo hivyo viwili vina design tofauti.......lakini pia unaweza kutofautisha kati ya Mnyama Chui na Mnyama Pundamilia kwa kuwa wanyama hao wana muundo, size, muonekano na mvuto tofauti,........

SO KWA KUMALIZIA NI KWAMBA UTHIBITISHO WA UWEPO WA DESIGNS TOFAUTI TUNAUPATA KWA KUANGALIA MIPANGILIO NA MUONEKANO TOFAUTI TOFAUTI WA VITU MBALIMBALI, NA SIO KWAMBA KUNA MTU MAALUMU WA KUKUAMBIA KWAMBA WEWE Econometrician NA MBU NI VIUMBE AMBAO MNA UMBILE( AMBALO NDIYO DESIGN YENYEWE HIYO) TOFAUTI.

Ikiwa hujaelewa unaweza kuuliza zaidi,.
 
Mungu yupi sasa unamzungumzia,Duniani kuna jamii nyingi ya watu na kila jamii ina Mungu wake.sasa hapa wewe unamzungumzia Mungu yupi???

At least 18,000 different gods, goddesses and various animals or objects have been worshipped by humans.
Duniani kuna watu ambao wanaweza hata kukufanya wewe kuwa Mungu lakini hiyo haikufanyi wewe Econometrician kuwa Mungu............watu wenye akili timamu dunia nzima wanapozungumzia kuhusu Mungu wanamaanisha yule ambae ameweka mpangilio wa vitu mbalimbali ikiwemo kukufanya uwe na vidole vya kutype hapa,.... Namaanisha Mungu ambaye amefanya maisha haya tunayoyaona yawepo kwenye hali na muundo huu uliopo......sasa ukiona mtu anasema Mungu wake ni Jiwe, Pipi au Chocolate hiyo isikuchanganye as long as akili yako inafanya kazi vizuri na unaweza kutofautisha right & wrong.


Naamini hii itakufanya uelewe na hutorudia kuuliza tena watu wenye akili zenye afya wanamaanisha Mungu yupi,..........Yaani in short ni kwamba kama hakuna Mungu aliyeumba viumbe na ulimwengu kwa ujumla,.. basi kutakua hakuna yoyote anaestahili kuitwa Mungu muumbaji....


Ikiwa hujaelewa,. unaweza kuuliza
 
YESU NDIE NJIA, KWELI NA UZIMA,AAMINIYE ATAOKOLEWA ASIYEAMINI ATAHUKUMIWA.
issue sio dini issue ni kutambua uwepo wa Mungu na kumuishi, ukifa utakuwa judged kwa terms za Mungu mwenyewe especially matendo yako kwa Mungu na kwa wengine, ila mwsho wa siku neema ya Mungu ndo itaamua final destination yako ni wapi
 
M nilipofikia najiona nipo,nilikuepo na nitakuepo(wakati wa sasa,uliopita na ujao)

Kuna creator (Mungu) lengo tuujaze huu ulimwengu how? Ndio watu wanatuma vyombo mars,mwenzini n.k kwa technology ya sasa ivyo huu mwili ukichakaa nitaondoka ila baada ya muda fulani nitarudi kuendeleza gurudumu.

Nikimaanisha hakuna moto wala pepo ila tuko kwenye mzunguko.
 
NIELEWE KWA MAKINI SANA.

Mungu wa Israel
Mungu Allah,
Mungu wa wabudha,
Miungu ya kale pale misri,
Na Mungu au Miungu yote ambayo inaabudiwa ikiwemo mizimu na isiyo mizimu, ikiwemo hai na isiyo hai.

Ukweli mchungu ni huu, pamoja na ufahamu wetu wote tulionao lakini bado hatufahamu kuhusu Mungu ama chanzo cha ulimwengu.

Sisemi kuwa Mungu yupo au hayupo hapana, bali naandika kuhusu giza la ufahamu tulilonalo juu ya yupi ni Mungu sahihi ama kipi ni chanzo sahihi cha ulimwengu!

Nafahamu watu na imani zenu mnaona kama naandika maandiko yasiyosahihi!,ila naomba utulivu wa fikra zako japo kwa uchache tutazame vitu kwa undani zaidi.

Hebu fikiri imani uliyonayo sasa, najua wengi wenu mmeirithi toka kwenye jamii ulipozaliwa hivyo ulivyo laiti ungezaliwa katika jamii inayoabudu budha nawe ungeamini na kuabudu na pia ungejiona upo sahihi, imani ambayo ingekuwa tofauti nawe ungeona Kama ni uongo tupu!

Ulishawahi kujiuliza kwanini?
Jibu baki nalo!

Swali zuri nalotaka ujiulize ni kwanini tuna aina nyingi hivi ya Mungu/Miungu? Na wakati ukiangalia kiuhalisia sisi sote ni binadamu wamoja, mazingira mamoja, tunavuta hewa moja n.k.

Kwenye vitu vidogo vidogo hivi tunafanana lakini hili kubwa tunatofauti sana!

Anaeabudu tofauti nawewe unamuona sio sahihi, nayeye pia anakuona wewe sio sahihi!

So yupi ni sahihi?

Kipi kinathibitisha kuwa wewe sio au ndio unaeamini mahali sahihi?

Mtu aliekinyume na imani yako ambae amezaliwa nakuamini tofauti unafikiri amefanya kosa lipi kwa Mungu wako kwa kutokumuamini kuwa ndie Mungu sahihi, ikiwa hakupata ufahamu wowote juu ya Mungu wako?

Je, unafikiri kati yako na Mungu nani alistahiri kumtoa kwenye tope mwenzake nakumleta mahali sahihi?

Maswali haya nikuchokoza ubongo wako ili ufikiri na uelewe nini namaanisha.

Je, huyo Mungu wako mwenye uweza haoni kama ana hatia kwa kuiachia Miungu mengine iabudiwe na kuwapoteza watu wake na hata kuja kuwapa adhabu watu hao?

Ukweli mchungu mwengine ni huu, mpaka Sasa binadamu hatufahamu Mungu sahihi na ndio maana bado tuna Miungu mingi tunayoabudu!

Laiti kama usahihi wa Mungu kweli ungeonekana kati ya Miungu tunayoijua basi binadamu asingekuwa kiumbe mwenye kutapatapa ktk imani!

Kwani kusingekuwa nashaka juu ya Mungu husika kwenye vichwa vyetu!

Tumezaliwa nakukuta vitu hivi vya imani, tumerithishwa tukavipokea (wapo wasiopokea) na tukaviamini (wapo wasioamini pia).

Jiulize, kwani imeshindikana nini kumfahamu Mungu mmoja wa kweli pasipo kurithishwa?

Imagine uzaliwe ujue kunyonya,ujue kupumua ujue kutazama ila Mungu wa kweli usimjue bali urithishwe.!😀
Kimekosekana nini mpaka Tushindwe kumjua Mungu ndani yetu pasipo kufundishwa?

Binafsi mpaka hivi sasa katika Mungu na Miungu ambayo nimeilist hapo juu hakuna hata mmoja ambae logics zake zimeniingia akilini na kunishawishi kuwa yeye ndie Mungu wa kweli!

Hata robo ya ulimwengu jinsi unavyofanya kazi bado hatujaujua ama siri na kanuni za ulimwengu unavyofanya kazi bado hatujazijua!.
MIUNGU wengi tulionao tunaowaabudu bado hawana majibu juu ya chanzo chao pia na ulimwengu kiujumla! Nafikiri zipo sheria mama za kiulimwengu ambazo tukizigundua basi tunaweza kuujua ukweli wote!

Tunajikuta katika lindi la imani hizi kwasababu Kuna kitu hatujajua bado! Giza la ufahamu mbele yetu ndilo linatuweka katika matokeo haya!

Hatujui usahihi wa kweli ipi ndio maana tunatofauti katika Mungu tumuabudie!, kweli huwa haina mashaka ila uwezo wa ufahamu wako ndio unaamua ubebe kipi na uache kipi.

Kwa akili naufahamu wako umeamini kuwa wapo watu wameteuliwa kuwa karibu na Mungu, hivyo wanaweza kukusogeza karibu na Mungu! Kwanini sio wewe mwenyewe ikiwa wewe ni asili toka kwake?

Siamini katika Mungu wa mashaka ambae toka binadamu amekuwepo ktk dunia hii tunaambiwa yupo ila anawashukia wachache na hali ipo Kama hivi ilivyo! Hata kuthibitika kwake bado imekuwa ni mashaka au matendo yake hayathibitiki bali masimulizi!

Mungu ambae ameumba ulimwengu wenye sayari lukuki na akamtupa shetani katika dunia ambayo inaviumbe wake wapendwa! Mungu ambae anasema kwamba shetani amekuja kutujaribu hivyo ni kazi yake mwenyewe anaipima na Kama hukuwa sahihi basi unapewa adhabu! Sa nani hayupo sahihi ikiwa mimi nilieumbwa au yeye alieniumba?

Haitoshi yupo Mungu na Miungu iliyobumbwa kwa vito ambavyo vimetoka hapahapa duniania na tunaambiwa wao ndio walituumba!

Nfikiri tunasafari ndefu ya kufahamu ukweli juu ya nadharia ya Umungu na Mungu mwenyewe pamoja na chanzo cha ulimwengu.

Ila nikupe ukweli wote Dini ni matrix iliyotengenezwa na wachache wanaoujua ukwel ili kutawala wengne, soul zetu zimetoka kwa Mungu kweli na zinatambua Hilo, Ila akili zetu zimetekwa na matrix huku duniani, Cha msingi apo nikufanya juhudi binafsi za kiroho ili kujitambua wewe Ni Nan umetoka wap,umekuja kufanya nin na utaenda wap? Kumeditate Ni muhimu ili kuwa na utulivu na kufungua Soul zetu.
Mhindi Kuabudu Ng'ombe kama Mungu na hapo hapo Ng'ombe huyo huyo mungu wake anamkatia majani inafikirisha sana.
 
Mimi nadhani ifike mahali tuache kujadili maswala ya mungu/miungu nk. Naona kama ni kupoteza muda tu.

Ni sawa na kujadili mambo ya kifo, kwamba nini kitatokea baada ya kifo. Hakuna alieko hai anaejua nini kitatokea baada ya kifo! Kwahiyo kujadili ni kupoteza muda tu na kujazana ujinga.

Hapa duniani hakuna binadamu yoyote anaejua KWA UHAKIKA Mungu ni nini, yupo au hayupo, kama yupo yuko wapi, mbinguni ni wapi, sisi tulitoka wapi nk. Wote tunajua tunachojua kupitia kusikia au kusoma hadithi za watu ambao nao walisikia au kusoma hadithi za wengine.
 
Bro hata kama hayupo ungebalance kidogo basi you are hurting my feelings maana hapa nilipo ni miujiza tu inaweza niokoa
Mkuu,

Kwenye hii Dunia ili utie huruma inabidi uwe na uhakika una watu watakao kuonea huruma, otherwise jitahidi kukaza.

In the jungle of life your salvation is largely in your hands, There is no God who can do anything for you.

Tafakari picha hii, Ndipo utajua hakuna Mungu wa kusaidia chochote.

Jitihada zako ndizo zitakazo kuokoa.
 

Attachments

  • Screenshot_20240527-134558_1.jpg
    Screenshot_20240527-134558_1.jpg
    136.3 KB · Views: 8
YESU NDIE NJIA, KWELI NA UZIMA,AAMINIYE ATAOKOLEWA ASIYEAMINI ATAHUKUMIWA.
issue sio dini issue ni kutambua uwepo wa Mungu na kumuishi, ukifa utakuwa judged kwa terms za Mungu mwenyewe especially matendo yako kwa Mungu na kwa wengine, ila mwsho wa siku neema ya Mungu ndo itaamua final destination yako ni wapi
Mungu huyo, Alishindwaje kuumba binadamu watakao mtambua na kumwamini siku zote na wakati wote?

Huyo Mungu, Hakujua kwamba anapaswa kuaminiwa na kila mtu?

Au alifanya makusudi kuumba binadamu wenye uwezo wa kutomwamini ili aje awaadhibu?

Halafu akisha waadhibu anapata faida gani?
 
Back
Top Bottom