Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 9,830
- 20,686
Unajua wewe una ji contradict mwenyewe wala hata huelewi ulicho kiandika.Mungu hapimwi katika vitu na Mazingira ya Kibinadamu,huwezi ona,kugusa au kusema namna fulani ndio kipimo cha kufanya yeye awepo au asiwepo hata hizi dini hizi majority of them hawaelewi concept ya Uungu
Yaani ni Mbumbumbu sababu wao wanajaribu kumtafuta Mungu out of them hawaelewi kua Uungu ni Asili yaani Nature
Ni hivi kila kitu kinachoexist katika Ulimwengu huu ikiwemo wao ndio MUNGU kama Asili maana huwezi tenganisha Uungu na vitu vyake yaani yeye ni chanzo cha vyote na haexist mahali popote ukamwona maana hata hapo popote ni yeye mwenyewe,
GOD is everything dat exist,
Yaani kila kitu ni Mungu na Mungu ndio kila kitu,
Dini na mafundisho yake toka kale yalipokea tofauti kuhusu Uungu wakidhani yeye ni extra kumbe ni Intra
Aliyekuja kufunua siri ya Uungu ni Master Yashua Amashiach Mnazarene (Jesus Christ)
Yeye ndie pekee aliyefunua siri ya Uungu kwamba yeye ni Mwana wa Mungu yaani Uungu usioonekana ndie yeye katika mwili (code 1)
Na anaenda mbali kia kila mtu Mungu yupo ndani yake ni wewe kukubaliana na anachokisema na ukatambua itakuafanya uamshe Roho Mtakatifu (Mungu ndani Yako)
Na kufanya kuwa sehemu yake (code 2)
Kwamba wewe ndie Mungu na kila kitu kinachokuzunguka kiliumbwa ukitawale sababu wewe ndie muumbaji wa vyote
(man is fresh and spirit)
Yaani kabla hujawa mwili ulikua Roho na katika Roho ulikua mmoja na Mungu (Katika Asili)
Hivyo katika Ulimwengu wa Roho Bwana
Yashua Amashiach
(Jesus Christ) ndie mzaliwa wa kwanza wa Mungu maana yeye ndie aliyekua wa kwanza kujua siri ya Uungu na kutufunulia Wanadamu hivyo yeye na ile Asili vilikua kwanza kushikana na huwezi vitenganisha kwa sababu ni kitu kimoja katika Mazingira tofauti,
Ukitambua hii siri ya Uungu na ukifanya kile Neno la Yesu limekuagiza ufuate na ukitambua inafungua milango ya wewe kuzaliwa mara ya pili
(kuingia katika Ulimwengu wa Roho)
Na hapo unaenda kua Immortal!
Nitaendelea siku nyingine kukufunulia siri ya Uungu!
Siri ambazo religion never tell you because of ignorance and lack of truth!
Accumen Mo Saad30
Mwanzoni ulianza kwa kusema, Mungu hapimwi katika vitu na mazingira ya kibinadamu.
Halafu tena unasema kila kitu kinacho exist na chenyewe ni Mungu...
Hapa tayari umeshampima huyo Mungu kwaku mfananisha na vitu na mazingira ya kibinadamu.
Kama Mungu ni kila kitu na kila kitu ni Mungu, Kwa hiyo huyo Mungu alijiumba ili awe kila kitu kisha ajitawale tena yeye mwenyewe?
Kama kila kitu ni Mungu including sisi binadamu, Utasemaje kwamba tuliumbwa?
Kama sisi binadamu tuliumbwa, Je sisi sio Mungu?
Kama sisi binadamu ni Mungu, Ni Mungu gani tena alituumba?