Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Kujibu hata mtu yeyote anaweza kujibu anachojisikia.

Lakini kutoa jibu lenye ukweli na mantiki hujajibu zaidi ya kutoa majibu na ufafanuzi uchwara...
Kama hujakubaliana na nilivyo eleza, ni haki yako kuamua kubaki na mtazamo wako. Sina cha zaidi kaka/dada.
 
kisukari, kansa au figo uone kama ataendelea na ngonjera zake

NIELEWE KWA MAKINI SANA.

Mungu wa Israel
Mungu Allah,
Mungu wa wabudha,
Miungu ya kale pale misri,
Na Mungu au Miungu yote ambayo inaabudiwa ikiwemo mizimu na isiyo mizimu, ikiwemo hai na isiyo hai.

Ukweli mchungu ni huu, pamoja na ufahamu wetu wote tulionao lakini bado hatufahamu kuhusu Mungu ama chanzo cha ulimwengu.

Sisemi kuwa Mungu yupo au hayupo hapana, bali naandika kuhusu giza la ufahamu tulilonalo juu ya yupi ni Mungu sahihi ama kipi ni chanzo sahihi cha ulimwengu!

Nafahamu watu na imani zenu mnaona kama naandika maandiko yasiyosahihi!,ila naomba utulivu wa fikra zako japo kwa uchache tutazame vitu kwa undani zaidi.

Hebu fikiri imani uliyonayo sasa, najua wengi wenu mmeirithi toka kwenye jamii ulipozaliwa hivyo ulivyo laiti ungezaliwa katika jamii inayoabudu budha nawe ungeamini na kuabudu na pia ungejiona upo sahihi, imani ambayo ingekuwa tofauti nawe ungeona Kama ni uongo tupu!

Ulishawahi kujiuliza kwanini?
Jibu baki nalo!

Swali zuri nalotaka ujiulize ni kwanini tuna aina nyingi hivi ya Mungu/Miungu? Na wakati ukiangalia kiuhalisia sisi sote ni binadamu wamoja, mazingira mamoja, tunavuta hewa moja n.k.

Kwenye vitu vidogo vidogo hivi tunafanana lakini hili kubwa tunatofauti sana!

Anaeabudu tofauti nawewe unamuona sio sahihi, nayeye pia anakuona wewe sio sahihi!

So yupi ni sahihi?

Kipi kinathibitisha kuwa wewe sio au ndio unaeamini mahali sahihi?

Mtu aliekinyume na imani yako ambae amezaliwa nakuamini tofauti unafikiri amefanya kosa lipi kwa Mungu wako kwa kutokumuamini kuwa ndie Mungu sahihi, ikiwa hakupata ufahamu wowote juu ya Mungu wako?

Je, unafikiri kati yako na Mungu nani alistahiri kumtoa kwenye tope mwenzake nakumleta mahali sahihi?

Maswali haya nikuchokoza ubongo wako ili ufikiri na uelewe nini namaanisha.

Je, huyo Mungu wako mwenye uweza haoni kama ana hatia kwa kuiachia Miungu mengine iabudiwe na kuwapoteza watu wake na hata kuja kuwapa adhabu watu hao?

Ukweli mchungu mwengine ni huu, mpaka Sasa binadamu hatufahamu Mungu sahihi na ndio maana bado tuna Miungu mingi tunayoabudu!

Laiti kama usahihi wa Mungu kweli ungeonekana kati ya Miungu tunayoijua basi binadamu asingekuwa kiumbe mwenye kutapatapa ktk imani!

Kwani kusingekuwa nashaka juu ya Mungu husika kwenye vichwa vyetu!

Tumezaliwa nakukuta vitu hivi vya imani, tumerithishwa tukavipokea (wapo wasiopokea) na tukaviamini (wapo wasioamini pia).

Jiulize, kwani imeshindikana nini kumfahamu Mungu mmoja wa kweli pasipo kurithishwa?

Imagine uzaliwe ujue kunyonya,ujue kupumua ujue kutazama ila Mungu wa kweli usimjue bali urithishwe.!😀
Kimekosekana nini mpaka Tushindwe kumjua Mungu ndani yetu pasipo kufundishwa?

Binafsi mpaka hivi sasa katika Mungu na Miungu ambayo nimeilist hapo juu hakuna hata mmoja ambae logics zake zimeniingia akilini na kunishawishi kuwa yeye ndie Mungu wa kweli!

Hata robo ya ulimwengu jinsi unavyofanya kazi bado hatujaujua ama siri na kanuni za ulimwengu unavyofanya kazi bado hatujazijua!.
MIUNGU wengi tulionao tunaowaabudu bado hawana majibu juu ya chanzo chao pia na ulimwengu kiujumla! Nafikiri zipo sheria mama za kiulimwengu ambazo tukizigundua basi tunaweza kuujua ukweli wote!

Tunajikuta katika lindi la imani hizi kwasababu Kuna kitu hatujajua bado! Giza la ufahamu mbele yetu ndilo linatuweka katika matokeo haya!

Hatujui usahihi wa kweli ipi ndio maana tunatofauti katika Mungu tumuabudie!, kweli huwa haina mashaka ila uwezo wa ufahamu wako ndio unaamua ubebe kipi na uache kipi.

Kwa akili naufahamu wako umeamini kuwa wapo watu wameteuliwa kuwa karibu na Mungu, hivyo wanaweza kukusogeza karibu na Mungu! Kwanini sio wewe mwenyewe ikiwa wewe ni asili toka kwake?

Siamini katika Mungu wa mashaka ambae toka binadamu amekuwepo ktk dunia hii tunaambiwa yupo ila anawashukia wachache na hali ipo Kama hivi ilivyo! Hata kuthibitika kwake bado imekuwa ni mashaka au matendo yake hayathibitiki bali masimulizi!

Mungu ambae ameumba ulimwengu wenye sayari lukuki na akamtupa shetani katika dunia ambayo inaviumbe wake wapendwa! Mungu ambae anasema kwamba shetani amekuja kutujaribu hivyo ni kazi yake mwenyewe anaipima na Kama hukuwa sahihi basi unapewa adhabu! Sa nani hayupo sahihi ikiwa mimi nilieumbwa au yeye alieniumba?

Haitoshi yupo Mungu na Miungu iliyobumbwa kwa vito ambavyo vimetoka hapahapa duniania na tunaambiwa wao ndio walituumba!

Nfikiri tunasafari ndefu ya kufahamu ukweli juu ya nadharia ya Umungu na Mungu mwenyewe pamoja na chanzo cha ulimwengu.

Ila nikupe ukweli wote Dini ni matrix iliyotengenezwa na wachache wanaoujua ukwel ili kutawala wengne, soul zetu zimetoka kwa Mungu kweli na zinatambua Hilo, Ila akili zetu zimetekwa na matrix huku duniani, Cha msingi apo nikufanya juhudi binafsi za kiroho ili kujitambua wewe Ni Nan umetokva wap,umekuja kufanya nin na utaenda wap? Kumeditate Ni muhimu ili kuwa na utulivu na kufungua Soul zetu.
Mimi huwa nafikili yakuwa kuna mzunguko usio na kikomo wa viumbe hai na visivo hai ambao chanzo chake hakijajulikana mpaka leo
 
Infropreneur Je, unakubali kama Viumbe hai, Dunia na ulimwengu kwa ujumla upo designed kwenye muundo (system)sahihi?
 
Infropreneur Je, unakubali kama Viumbe hai, Dunia na ulimwengu kwa ujumla upo designed kwenye muundo (system)sahihi?
Kwanza ulijuaje kama viumbe hai, dunia na ulimwengu kwa ujumla vipo Designed?

Kwani haiwezekani visiwe Designed?

Kuna ulazima upi wa kwamba viumbe hai, dunia na ulimwengu kwa ujumla vimekuwa Designed?
 
Kwanza ulijuaje kama viumbe hai, dunia na ulimwengu kwa ujumla vipo Designed?

Kwani haiwezekani visiwe Designed?

Kuna ulazima upi wa kwamba viumbe hai, dunia na ulimwengu kwa ujumla vimekuwa Designed?
Okay, nimejua kama vipo designed kwasababu naona design.
 
Kwa upande wako, unamzungumzia vipi mwandishi wa kitabu hicho. Ni mtu wa aina gani?
Ni mtu huru, anayefikiri pasipo mihemko, moral is what you are capable of, and dogma is what you must do,ni mode ya maisha kuwa moral right dogmatically.
 
Okay, nimejua kama vipo designed kwasababu naona design.
Unaona Design kutoka kwenye reference ipi?

Kwenye nini?

Hicho kinacho kufanya uone ulimwengu umekuwa designed, Je chenyewe hakihitaji uono huu wa kuwa Designed?
 
Ni mtu huru, anayefikiri pasipo mihemko, moral is what you are capable of, and dogma is what you must do,ni mode ya maisha kuwa moral right dogmatically.
Lakni inamaana mtu akiwa huru basi anafanya chochote anachotaka bila kujali ethics sindiyo?
 
Unaona Design kutoka kwenye reference ipi?

Kwenye nini?

Hicho kinacho kufanya uone ulimwengu umekuwa designed, Je chenyewe hakihitaji uono huu wa kuwa Designed?
Unamaanisha nini unapotaka reference kwenye macho kuona design?

Akili yenye afya ikiona Tunda La Nanasi na Tunda la Parachichi,..itajua wazi kwamba matunda hayo mawili yana design mbili tofauti.


akili akili akili....
 
Unamaanisha nini unapotaka reference kwenye macho kuona design?

Akili yenye afya ikiona Tunda La Nanasi na Tunda la Parachichi,..itajua wazi kwamba matunda hayo mawili yana design mbili tofauti.


akili akili akili....
Yani ni hivi,

Kwa nini unaona tu lazima ulimwengu umekuwa designed, Lakini huoni na hujiulizi huyo Designer wa ulimwengu, na yeye alikuwaje designed?

Kwa nini unauliza tu ulimwengu umekuwaje designed, Halafu unashindwa kujiuliza hivi,

Je ni kweli ulimwengu umekuwa designed au pengine unaweza na uliweza kuji Design wenyewe tu?

Kwa nini hujiulizi kama ulimwengu uliweza kuji design wenyewe, ila unauliza ulimwengu ulikuwa designed?
 
Back
Top Bottom