Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Finally, ukifa ndiyo utajua hujui
Hata kabla hatujafa tayari tunajua hatujui, sasa kama tupo hai na hatujui itawezekanaje kujua wakati tutakapokuwa bila uhai? Tunapaswa kujua sasa,ili tuwe na hakika ya aftermath kwenye ulimwengu huu, labda kuna mtu au watu wanajua? Kama wapo kwa nini hawataki na sisi tujue? Au hakuna anayejua? Sasa kwa nini watudanganye kuwa wanajua? Na eti hicho wanachokijua wao ndiyo sahihi kabisa,kisichopaswa kuhojiwa wala kupingwa, na mbona sifa za mungu haziwiani na uhalisia? Mfano mungu wa upendo anayeabudiwa na waislam, waislam ambao wanafanyiwa ukatili wa kutisha huko palestina na kwingineko, mamilioni ya wayahudi walichinjwa kwenye hollocaust huko ujerumani huku yhw akiwatazama tu bila kuwasaidia chochote,wakristo wanateseka kila mahali dunia hii,na jehova ameamua kuacha wafe tu, angalau Budha wanatumia zaidi akili zao binafsi kupambana na mazingira, ndiyo maana labda wao kidogo wana utulivu, ila pia wanapata taabu nyingi tu za ki asili zinazowaumiza mwili na roho, fikiria matetemeko ya ardhi yanayowaua kwa maelfu nani kayatengeneza? Mafuriko yakipita hayachagui mcha mungu wala muovu, yanasomba wote, vimbunga hivyo hivyo, vita ndiyo balaa kabisa, tena kwenye vita mataifa yale yanayomtumikia mungu kwa sana ndiyo huwa wahanga, kwa nini?
Huku kwetu ukionekana una maisha mazuri waumini wanasema wewe ni devil worshiper, kwani mungu wetu hana wivu? Awaonee wivu wafuasi wa shetani wanaofanikiwa kwa kila jambo huku wafuasi wake wakichakaa kwa kila aina ya madhila? Maswali ni mengi kuliko majibu,na mara zote majibu huzua maswali zaidi,asante mtoa mada.
 
Umeeleza nini zaidi ya kujibu usivyo ulizwa?

Nakuuliza hivi 👇

Kama ubongo sio akili, Hiyo akili inakaa wapi?

Jibu swali acha danadana.
Akili haiwezi kuonekana, lakini ipo. Kama ambavyo ile comment ya DNA inavyo sema.
 
Wewe ndio inabidi u relax!!!

Na uchambue maoni yako kwa kina.

Kabla ya kufanya "ad hominem attack" kwa mtu, Hakikisha kwanza huyo mtu hoja zake umezielewa sio umekurupuka tu kumshambulia pasipo kuchunguza ukweli wa hoja zake.
Bro/Sister when I say relax then u should refrain from replying. You have neither clue nor idea as to why I said that to the guy. You think I just start with him on 'this thread'... No.. it's from other threads. So chill up, relax!! chew the bubble gum then go for a sleep or take a nap joh...

Cheers!!
 
Bro/Sister when I say relax then u should refrain from replying. You have neither clue nor idea as to why I said that to the guy. You think I just start with him on 'this thread'... No.. it's from other threads. So chill up, relax!! chew the bubble gum then go for a sleep or take a nap joh...

Cheers!!
Another petty bloated entitled brat throwing tantrums.

Find someone of your league to parallel your mediocrity.
 
K
Je! unaambini biblia ni neno la mungu?
KUna mtu pia atakuuliza, je unaamini kuwa quran ni kitabu cha mungu?

Baadaye m=budha atakuuliza je unaamini kuwa moral and dogma ni kitabu cha mungu? Utajibu kulingana na imani uliyorithishwa? Au utajibu kutokana na uelewa wako binafsi?
 
K

KUna mtu pia atakuuliza, je unaamini kuwa quran ni kitabu cha mungu?

Baadaye m=budha atakuuliza je unaamini kuwa moral and dogma ni kitabu cha mungu? Utajibu kulingana na imani uliyorithishwa? Au utajibu kutokana na uelewa wako binafsi?
Moral and dogma, unakifahamu hichi kitabu mkuu?
 
Ni kweli physics sijasoma, ila hiyo physics ya mainstream Education yaweza kuwa sababu pia kuzaa watu ambao wamelishwa uongo mwingi na kuaminisha mambo yasio na uhalisia.
Wewe ni mmojawapo wa walio lishwa hayo mambo yasiyo na uhalisia, ndio maana huna facts zaidi ya ufafanuzi uchwara wa vichochoroni na vilabuni huko...
 
Subri apigwe na ugonjwa tu kama wa kisukari, kansa au figo uone kama ataendelea na ngonjera zake hapo juu.

Wewe hauwezi hata jiongezea japo umri ufikishe miaka 200, halafu unaanza kuvimba dhidi ya aliyeviweka vyote hivi tunavyoviona na tusivyoviona.

Hizo imani zote lengo mama ni kumuabudu na kumtafuta Mungu mkuu muumba wa vyote ingawa zinatofautiana utaratibu, hivyo inawezekana wote wakawa sahihi.
Magonjwa yote hayo yanatupata sote, whether unaamini mungu yupi au hauamini kabisa, wote tutaugua in one place or another, and our common deal is death, waovu na watakatifu wote tutanywea kikombe kimoja, sasa kwa nini tunabaguana? Kila kimpatacho binaadam kitampata tu, no matter what.
 
Wewe ni mmojawapo wa walio lishwa hayo mambo yasiyo na uhalisia, ndio maana huna facts zaidi ya ufafanuzi uchwara wa vichochoroni na vilabuni huko...
Japo Vichochoroni na vilabuni sio maeneo yangu, Lakni ninacho jua ni kwamba Ubongo na akili ni vitu viwili.
 
NIELEWE KWA MAKINI SANA.

Mungu wa Israel
Mungu Allah,
Mungu wa wabudha,
Miungu ya kale pale misri,
Na Mungu au Miungu yote ambayo inaabudiwa ikiwemo mizimu na isiyo mizimu, ikiwemo hai na isiyo hai.

Ukweli mchungu ni huu, pamoja na ufahamu wetu wote tulionao lakini bado hatufahamu kuhusu Mungu ama chanzo cha ulimwengu.

Sisemi kuwa Mungu yupo au hayupo hapana, bali naandika kuhusu giza la ufahamu tulilonalo juu ya yupi ni Mungu sahihi ama kipi ni chanzo sahihi cha ulimwengu!

Nafahamu watu na imani zenu mnaona kama naandika maandiko yasiyosahihi!,ila naomba utulivu wa fikra zako japo kwa uchache tutazame vitu kwa undani zaidi.

Hebu fikiri imani uliyonayo sasa, najua wengi wenu mmeirithi toka kwenye jamii ulipozaliwa hivyo ulivyo laiti ungezaliwa katika jamii inayoabudu budha nawe ungeamini na kuabudu na pia ungejiona upo sahihi, imani ambayo ingekuwa tofauti nawe ungeona Kama ni uongo tupu!

Ulishawahi kujiuliza kwanini?
Jibu baki nalo!

Swali zuri nalotaka ujiulize ni kwanini tuna aina nyingi hivi ya Mungu/Miungu? Na wakati ukiangalia kiuhalisia sisi sote ni binadamu wamoja, mazingira mamoja, tunavuta hewa moja n.k.

Kwenye vitu vidogo vidogo hivi tunafanana lakini hili kubwa tunatofauti sana!

Anaeabudu tofauti nawewe unamuona sio sahihi, nayeye pia anakuona wewe sio sahihi!

So yupi ni sahihi?

Kipi kinathibitisha kuwa wewe sio au ndio unaeamini mahali sahihi?

Mtu aliekinyume na imani yako ambae amezaliwa nakuamini tofauti unafikiri amefanya kosa lipi kwa Mungu wako kwa kutokumuamini kuwa ndie Mungu sahihi, ikiwa hakupata ufahamu wowote juu ya Mungu wako?

Je, unafikiri kati yako na Mungu nani alistahiri kumtoa kwenye tope mwenzake nakumleta mahali sahihi?

Maswali haya nikuchokoza ubongo wako ili ufikiri na uelewe nini namaanisha.

Je, huyo Mungu wako mwenye uweza haoni kama ana hatia kwa kuiachia Miungu mengine iabudiwe na kuwapoteza watu wake na hata kuja kuwapa adhabu watu hao?

Ukweli mchungu mwengine ni huu, mpaka Sasa binadamu hatufahamu Mungu sahihi na ndio maana bado tuna Miungu mingi tunayoabudu!

Laiti kama usahihi wa Mungu kweli ungeonekana kati ya Miungu tunayoijua basi binadamu asingekuwa kiumbe mwenye kutapatapa ktk imani!

Kwani kusingekuwa nashaka juu ya Mungu husika kwenye vichwa vyetu!

Tumezaliwa nakukuta vitu hivi vya imani, tumerithishwa tukavipokea (wapo wasiopokea) na tukaviamini (wapo wasioamini pia).

Jiulize, kwani imeshindikana nini kumfahamu Mungu mmoja wa kweli pasipo kurithishwa?

Imagine uzaliwe ujue kunyonya,ujue kupumua ujue kutazama ila Mungu wa kweli usimjue bali urithishwe.!😀
Kimekosekana nini mpaka Tushindwe kumjua Mungu ndani yetu pasipo kufundishwa?

Binafsi mpaka hivi sasa katika Mungu na Miungu ambayo nimeilist hapo juu hakuna hata mmoja ambae logics zake zimeniingia akilini na kunishawishi kuwa yeye ndie Mungu wa kweli!

Hata robo ya ulimwengu jinsi unavyofanya kazi bado hatujaujua ama siri na kanuni za ulimwengu unavyofanya kazi bado hatujazijua!.
MIUNGU wengi tulionao tunaowaabudu bado hawana majibu juu ya chanzo chao pia na ulimwengu kiujumla! Nafikiri zipo sheria mama za kiulimwengu ambazo tukizigundua basi tunaweza kuujua ukweli wote!

Tunajikuta katika lindi la imani hizi kwasababu Kuna kitu hatujajua bado! Giza la ufahamu mbele yetu ndilo linatuweka katika matokeo haya!

Hatujui usahihi wa kweli ipi ndio maana tunatofauti katika Mungu tumuabudie!, kweli huwa haina mashaka ila uwezo wa ufahamu wako ndio unaamua ubebe kipi na uache kipi.

Kwa akili naufahamu wako umeamini kuwa wapo watu wameteuliwa kuwa karibu na Mungu, hivyo wanaweza kukusogeza karibu na Mungu! Kwanini sio wewe mwenyewe ikiwa wewe ni asili toka kwake?

Siamini katika Mungu wa mashaka ambae toka binadamu amekuwepo ktk dunia hii tunaambiwa yupo ila anawashukia wachache na hali ipo Kama hivi ilivyo! Hata kuthibitika kwake bado imekuwa ni mashaka au matendo yake hayathibitiki bali masimulizi!

Mungu ambae ameumba ulimwengu wenye sayari lukuki na akamtupa shetani katika dunia ambayo inaviumbe wake wapendwa! Mungu ambae anasema kwamba shetani amekuja kutujaribu hivyo ni kazi yake mwenyewe anaipima na Kama hukuwa sahihi basi unapewa adhabu! Sa nani hayupo sahihi ikiwa mimi nilieumbwa au yeye alieniumba?

Haitoshi yupo Mungu na Miungu iliyobumbwa kwa vito ambavyo vimetoka hapahapa duniania na tunaambiwa wao ndio walituumba!

Nfikiri tunasafari ndefu ya kufahamu ukweli juu ya nadharia ya Umungu na Mungu mwenyewe pamoja na chanzo cha ulimwengu.

Ila nikupe ukweli wote Dini ni matrix iliyotengenezwa na wachache wanaoujua ukwel ili kutawala wengne, soul zetu zimetoka kwa Mungu kweli na zinatambua Hilo, Ila akili zetu zimetekwa na matrix huku duniani, Cha msingi apo nikufanya juhudi binafsi za kiroho ili kujitambua wewe Ni Nan umetoka wap,umekuja kufanya nin na utaenda wap? Kumeditate Ni muhimu ili kuwa na utulivu na kufungua Soul zetu.
Elimu tatu za Dunia na ulimwengu ambazo ujumla wake ndo unapata matrix iliyowafunga wengi kifikra ni

1.Theology
2.Psychology
3.Philosophy

Hizo ndo zilikuwa zimeteka wengi ila wachache walikuwa wanajua kweli.Ila Muumba ni zaidi ya izo elimu tatu za dunia kiufahamu.

Muumba ni mmoja na hagawanyiki, hana mwanzo wala mwisho anaishi umilele,wala hana dini wala dhehebu kama tulivyofundishwa na yeye ndiye CHANZO HALISI cha mema na mazuri yote.

Wengi tulikuwa kwenye utumwa wa asili maana akasema ikifika majira yake miungu yote isiyoumba mbingu na nchi lazima iangamie.

Yeremia 10:11
Mtawaambia hivi, Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi, nayo itatoweka chini ya mbingu.
 
Japo Vichochoroni na vitabuni sio maeneo yangu, Lakni ninacho jua ni kwamba Ubongo na akili ni vitu viwili.
Kama ubongo na akili ni vitu viwili tofauti,

Akili inakaa wapi?

Sehemu gani?


Jibu hoja wewe!! acha viroja
 
MUNGU wa kweli ni Mungu wa Mbinguni, wanamwita Yaweh, Jehovah, ambaye pia ndiye Mungu wa Abraham, Mungu wa Isaka na Mungu wa Israel. Aliyeumba Mbingu na Dunia na Viumbe wote wanaoonekana na wasio onekana, vilivyohai na visivyohai. Yeye ndiye Asili ya yote, Hana mwanzo na hatakaa awe na Mwisho.

Ukielewa chukua, hutaki endelea na majizingaombwe ya Dunia.
Wa imani nyingine pia wana conclusion yao,isiyofanana na yako, nao wanakuambia ukielewa chukua,hutaki endelea na mazingaombwe ya dunia,dunia yenyewe ni hii hii, wote tupo hapa, tunaishi hapa,tutafia hapa, na huyo mungu hakuwahi wala hatawahi kuishi miongoni mwetu hapa duniani, the mythical myth,tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa nature.
 
Nilisha jibu, pitia comment za nyuma.
Umejibu nini zaidi ya ufafanuzi uchwara na hoja za kubwabwaja bwabwaja tu...

Naku uliza hivi 👇

Kama ubongo sio akili, Akili inakaa wapi?

Jibu swali, Acha mbambamba...
 
Umejibu nini zaidi ya ufafanuzi uchwara na hoja za kubwabwaja bwabwaja tu...

Naku uliza hivi 👇

Kama ubongo sio akili, Akili inakaa wapi?

Jibu swali, Acha mbambamba...
Nlisha jibu, pitia comment za nyuma.
 
Back
Top Bottom