Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

NIELEWE KWA MAKINI SANA.

Mungu wa Israel
Mungu Allah,
Mungu wa wabudha,
Miungu ya kale pale misri,
Na Mungu au Miungu yote ambayo inaabudiwa ikiwemo mizimu na isiyo mizimu, ikiwemo hai na isiyo hai.

Ukweli mchungu ni huu, pamoja na ufahamu wetu wote tulionao lakini bado hatufahamu kuhusu Mungu ama chanzo cha ulimwengu.

Sisemi kuwa Mungu yupo au hayupo hapana, bali naandika kuhusu giza la ufahamu tulilonalo juu ya yupi ni Mungu sahihi ama kipi ni chanzo sahihi cha ulimwengu!

Nafahamu watu na imani zenu mnaona kama naandika maandiko yasiyosahihi!,ila naomba utulivu wa fikra zako japo kwa uchache tutazame vitu kwa undani zaidi.

Hebu fikiri imani uliyonayo sasa, najua wengi wenu mmeirithi toka kwenye jamii ulipozaliwa hivyo ulivyo laiti ungezaliwa katika jamii inayoabudu budha nawe ungeamini na kuabudu na pia ungejiona upo sahihi, imani ambayo ingekuwa tofauti nawe ungeona Kama ni uongo tupu!

Ulishawahi kujiuliza kwanini?
Jibu baki nalo!

Swali zuri nalotaka ujiulize ni kwanini tuna aina nyingi hivi ya Mungu/Miungu? Na wakati ukiangalia kiuhalisia sisi sote ni binadamu wamoja, mazingira mamoja, tunavuta hewa moja n.k.

Kwenye vitu vidogo vidogo hivi tunafanana lakini hili kubwa tunatofauti sana!

Anaeabudu tofauti nawewe unamuona sio sahihi, nayeye pia anakuona wewe sio sahihi!

So yupi ni sahihi?

Kipi kinathibitisha kuwa wewe sio au ndio unaeamini mahali sahihi?

Mtu aliekinyume na imani yako ambae amezaliwa nakuamini tofauti unafikiri amefanya kosa lipi kwa Mungu wako kwa kutokumuamini kuwa ndie Mungu sahihi, ikiwa hakupata ufahamu wowote juu ya Mungu wako?

Je, unafikiri kati yako na Mungu nani alistahiri kumtoa kwenye tope mwenzake nakumleta mahali sahihi?

Maswali haya nikuchokoza ubongo wako ili ufikiri na uelewe nini namaanisha.

Je, huyo Mungu wako mwenye uweza haoni kama ana hatia kwa kuiachia Miungu mengine iabudiwe na kuwapoteza watu wake na hata kuja kuwapa adhabu watu hao?

Ukweli mchungu mwengine ni huu, mpaka Sasa binadamu hatufahamu Mungu sahihi na ndio maana bado tuna Miungu mingi tunayoabudu!

Laiti kama usahihi wa Mungu kweli ungeonekana kati ya Miungu tunayoijua basi binadamu asingekuwa kiumbe mwenye kutapatapa ktk imani!

Kwani kusingekuwa nashaka juu ya Mungu husika kwenye vichwa vyetu!

Tumezaliwa nakukuta vitu hivi vya imani, tumerithishwa tukavipokea (wapo wasiopokea) na tukaviamini (wapo wasioamini pia).

Jiulize, kwani imeshindikana nini kumfahamu Mungu mmoja wa kweli pasipo kurithishwa?

Imagine uzaliwe ujue kunyonya,ujue kupumua ujue kutazama ila Mungu wa kweli usimjue bali urithishwe.!😀
Kimekosekana nini mpaka Tushindwe kumjua Mungu ndani yetu pasipo kufundishwa?

Binafsi mpaka hivi sasa katika Mungu na Miungu ambayo nimeilist hapo juu hakuna hata mmoja ambae logics zake zimeniingia akilini na kunishawishi kuwa yeye ndie Mungu wa kweli!

Hata robo ya ulimwengu jinsi unavyofanya kazi bado hatujaujua ama siri na kanuni za ulimwengu unavyofanya kazi bado hatujazijua!.
MIUNGU wengi tulionao tunaowaabudu bado hawana majibu juu ya chanzo chao pia na ulimwengu kiujumla! Nafikiri zipo sheria mama za kiulimwengu ambazo tukizigundua basi tunaweza kuujua ukweli wote!

Tunajikuta katika lindi la imani hizi kwasababu Kuna kitu hatujajua bado! Giza la ufahamu mbele yetu ndilo linatuweka katika matokeo haya!

Hatujui usahihi wa kweli ipi ndio maana tunatofauti katika Mungu tumuabudie!, kweli huwa haina mashaka ila uwezo wa ufahamu wako ndio unaamua ubebe kipi na uache kipi.

Kwa akili naufahamu wako umeamini kuwa wapo watu wameteuliwa kuwa karibu na Mungu, hivyo wanaweza kukusogeza karibu na Mungu! Kwanini sio wewe mwenyewe ikiwa wewe ni asili toka kwake?

Siamini katika Mungu wa mashaka ambae toka binadamu amekuwepo ktk dunia hii tunaambiwa yupo ila anawashukia wachache na hali ipo Kama hivi ilivyo! Hata kuthibitika kwake bado imekuwa ni mashaka au matendo yake hayathibitiki bali masimulizi!

Mungu ambae ameumba ulimwengu wenye sayari lukuki na akamtupa shetani katika dunia ambayo inaviumbe wake wapendwa! Mungu ambae anasema kwamba shetani amekuja kutujaribu hivyo ni kazi yake mwenyewe anaipima na Kama hukuwa sahihi basi unapewa adhabu! Sa nani hayupo sahihi ikiwa mimi nilieumbwa au yeye alieniumba?

Haitoshi yupo Mungu na Miungu iliyobumbwa kwa vito ambavyo vimetoka hapahapa duniania na tunaambiwa wao ndio walituumba!

Nfikiri tunasafari ndefu ya kufahamu ukweli juu ya nadharia ya Umungu na Mungu mwenyewe pamoja na chanzo cha ulimwengu.

Ila nikupe ukweli wote Dini ni matrix iliyotengenezwa na wachache wanaoujua ukwel ili kutawala wengne, soul zetu zimetoka kwa Mungu kweli na zinatambua Hilo, Ila akili zetu zimetekwa na matrix huku duniani, Cha msingi apo nikufanya juhudi binafsi za kiroho ili kujitambua wewe Ni Nan umetoka wap,umekuja kufanya nin na utaenda wap? Kumeditate Ni muhimu ili kuwa na utulivu na kufungua Soul zetu.
Kaka upo sahihi.
Wengi akili zetu zipo programmed na mapokeo.
Nashauri tuamke kutoka ndani ili kujitambua zaidi.
 
Bila ubongo unaweza kutumia hiyo akili yako kufikiri?

Kama ubongo sio akili, Tukutoe huo ubongo kichwani halafu utumie hiyo akili yako kufanya vitu.
Akili haiwezi fanya kazi kama mojawapo ya kiungo muhimu mwilini hakipo, kwa maana ya utimamu wa mwili kutokuwa active.

Sio ubongo tu. Hata ukitoa mapafu tu basi akili bado haiwezi kufanya kazi
 
Kumbuka Brain ni physical, ili ipate hitilafu basi sababu inakuwa physical pia.
Sasa nadhani unafahamu kuna watu wamepata uchizi bila hata kuguswa physically.

Kupata uchizi ni matokeo ya kuvugika kwa mfumo wa akili, yani bado brain inakuwa inafanya kazi vizuri tu na ina sence na kutafsiri vitu kama maumivu,harufu, sauti na mengineyo.
Sawa, nadhani ukiendelea kuchunguza wataalamu wame share picha za ubongo ukiwa na hitilafu flani, na ukiwa na normal health. Katika hali hizo mbili ubongo wakiscan picha zinaonekana tofauti, kwaio inaweza kupata physical problem pia na ikaathiri utendaji kazi wake na kusababisha kupatikana akili iliyo na hitilafu.

Unaweza ukagoogle picha za ubongo zinavyokuwa binadamu akipata ule ugonjwa wa uzeeni ambao unasababisha kumbukumbu kuwa chini.
 
Bila ubongo unaweza kutumia hiyo akili yako kufikiri?

Kama ubongo sio akili, Tukutoe huo ubongo kichwani halafu utumie hiyo akili yako kufanya vitu.

Je Hilo linawezekana?
Hahah umenivunja mbavu aisee... 😂 😂
 
Akili haiwezi fanya kazi kama mojawapo ya kiungo muhimu mwilini hakipo, kwa maana ya utimamu wa mwili kutokuwa active.

Sio ubongo tu. Hata ukitoa mapafu tu basi akili bado haiwezi kufanya kazi
Ulisema ubongo sio akili, Sasa nakuuliza hivi Tukutoe huo ubongo kichwani halafu utumie hiyo akili yako ambayo ipo separated na ubongo unaweza?

Acha kuleta ufafanuzi uchwara.

Jibu swali.
 
Ulisema ubongo sio akili, Sasa nakuuliza hivi Tukutoe huo ubongo kichwani halafu utumie hiyo akili yako ambayo ipo separated na ubongo unaweza?

Acha kuleta ufafanuzi uchwara.

Jibu swali.
Ukinitoa ubongo utakuwa umesababisha kufeli kwa mfumo wangu wa upumuaji pamoja na mapigo ya moyo kwa maana ubongo ni kiungo muhimu katika shughuli hizo.

Hapo akili haiwezi kufanya kazi kabisa kwa maana mwili umezima.
 
Sawa, nadhani ukiendelea kuchunguza wataalamu wame share picha za ubongo ukiwa na hitilafu flani, na ukiwa na normal health. Katika hali hizo mbili ubongo wakiscan picha zinaonekana tofauti, kwaio inaweza kupata physical problem pia na ikaathiri utendaji kazi wake na kusababisha kupatikana akili iliyo na hitilafu.

Unaweza ukagoogle picha za ubongo zinavyokuwa binadamu akipata ule ugonjwa wa uzeeni ambao unasababisha kumbukumbu kuwa chini.
Ni kweli ubongo unaweza pata maradhi au matatizo ambayo yanaonekana, hivyo itasababisha shida kwenye mfumo wa akili.

Lakni bado ni vitu viwili tofauti
 
Ukinitoa ubongo utakuwa umesababisha kufeli kwa mfumo wangu wa upumuaji pamoja na mapigo ya moyo kwa maana ubongo ni kiungo muhimu katika shughuli hizo.

Hapo akili haiwezi kufanya kazi kabisa kwa maana mwili umezima.
Sasa kama akili haiwezi kufanya kazi bila ubongo, Utasemaje ubongo sio akili?

Kama ubongo sio akili, Kwa nini ukitolewa ubongo, akili haiwezi kufanya kazi yenyewe tu?
 
Ni kweli ubongo unaweza pata maradhi au matatizo ambayo yanaonekana, hivyo itasababisha shida kwenye mfumo wa akili.

Lakni bado ni vitu viwili tofauti
Kama ubongo na akili ni vitu viwili tofauti.

Hiyo akili inakaa wapi?
 
Sasa kama akili haiwezi kufanya kazi bila ubongo, Utasemaje ubongo sio akili?

Kama ubongo sio akili, Kwa nini ukitolewa ubongo, akili haiwezi kufanya kazi yenyewe tu?
Ubongo sio akili. Nadhani nimesha eleza yote kuhusu hilo. Kama bado huelewi basi that's up to you.
 
Ubongo sio akili. Nadhani nimesha eleza yote kuhusu hilo. Kama bado huelewi basi that's up to you.
Umeeleza nini zaidi ya kujibu usivyo ulizwa?

Nakuuliza hivi 👇

Kama ubongo sio akili, Hiyo akili inakaa wapi?

Jibu swali acha danadana.
 
Wewe inaonesha hata Physics hukusoma.

Unaleta mifano ya kitoto sana na ufafanuzi uchwara.
Ni kweli physics sijasoma, ila hiyo physics ya mainstream Education yaweza kuwa sababu pia kuzaa watu ambao wamelishwa uongo mwingi na kuaminisha mambo yasio na uhalisia.
 
Back
Top Bottom