NIELEWE KWA MAKINI SANA.
Mungu wa Israel
Mungu Allah,
Mungu wa wabudha,
Miungu ya kale pale misri,
Na Mungu au Miungu yote ambayo inaabudiwa ikiwemo mizimu na isiyo mizimu, ikiwemo hai na isiyo hai.
Ukweli mchungu ni huu, pamoja na ufahamu wetu wote tulionao lakini bado hatufahamu kuhusu Mungu ama chanzo cha ulimwengu.
Sisemi kuwa Mungu yupo au hayupo hapana, bali naandika kuhusu giza la ufahamu tulilonalo juu ya yupi ni Mungu sahihi ama kipi ni chanzo sahihi cha ulimwengu!
Nafahamu watu na imani zenu mnaona kama naandika maandiko yasiyosahihi!,ila naomba utulivu wa fikra zako japo kwa uchache tutazame vitu kwa undani zaidi.
Hebu fikiri imani uliyonayo sasa, najua wengi wenu mmeirithi toka kwenye jamii ulipozaliwa hivyo ulivyo laiti ungezaliwa katika jamii inayoabudu budha nawe ungeamini na kuabudu na pia ungejiona upo sahihi, imani ambayo ingekuwa tofauti nawe ungeona Kama ni uongo tupu!
Ulishawahi kujiuliza kwanini?
Jibu baki nalo!
Swali zuri nalotaka ujiulize ni kwanini tuna aina nyingi hivi ya Mungu/Miungu? Na wakati ukiangalia kiuhalisia sisi sote ni binadamu wamoja, mazingira mamoja, tunavuta hewa moja n.k.
Kwenye vitu vidogo vidogo hivi tunafanana lakini hili kubwa tunatofauti sana!
Anaeabudu tofauti nawewe unamuona sio sahihi, nayeye pia anakuona wewe sio sahihi!
So yupi ni sahihi?
Kipi kinathibitisha kuwa wewe sio au ndio unaeamini mahali sahihi?
Mtu aliekinyume na imani yako ambae amezaliwa nakuamini tofauti unafikiri amefanya kosa lipi kwa Mungu wako kwa kutokumuamini kuwa ndie Mungu sahihi, ikiwa hakupata ufahamu wowote juu ya Mungu wako?
Je, unafikiri kati yako na Mungu nani alistahiri kumtoa kwenye tope mwenzake nakumleta mahali sahihi?
Maswali haya nikuchokoza ubongo wako ili ufikiri na uelewe nini namaanisha.
Je, huyo Mungu wako mwenye uweza haoni kama ana hatia kwa kuiachia Miungu mengine iabudiwe na kuwapoteza watu wake na hata kuja kuwapa adhabu watu hao?
Ukweli mchungu mwengine ni huu, mpaka Sasa binadamu hatufahamu Mungu sahihi na ndio maana bado tuna Miungu mingi tunayoabudu!
Laiti kama usahihi wa Mungu kweli ungeonekana kati ya Miungu tunayoijua basi binadamu asingekuwa kiumbe mwenye kutapatapa ktk imani!
Kwani kusingekuwa nashaka juu ya Mungu husika kwenye vichwa vyetu!
Tumezaliwa nakukuta vitu hivi vya imani, tumerithishwa tukavipokea (wapo wasiopokea) na tukaviamini (wapo wasioamini pia).
Jiulize, kwani imeshindikana nini kumfahamu Mungu mmoja wa kweli pasipo kurithishwa?
Imagine uzaliwe ujue kunyonya,ujue kupumua ujue kutazama ila Mungu wa kweli usimjue bali urithishwe.![emoji3]
Kimekosekana nini mpaka Tushindwe kumjua Mungu ndani yetu pasipo kufundishwa?
Binafsi mpaka hivi sasa katika Mungu na Miungu ambayo nimeilist hapo juu hakuna hata mmoja ambae logics zake zimeniingia akilini na kunishawishi kuwa yeye ndie Mungu wa kweli!
Hata robo ya ulimwengu jinsi unavyofanya kazi bado hatujaujua ama siri na kanuni za ulimwengu unavyofanya kazi bado hatujazijua!.
MIUNGU wengi tulionao tunaowaabudu bado hawana majibu juu ya chanzo chao pia na ulimwengu kiujumla! Nafikiri zipo sheria mama za kiulimwengu ambazo tukizigundua basi tunaweza kuujua ukweli wote!
Tunajikuta katika lindi la imani hizi kwasababu Kuna kitu hatujajua bado! Giza la ufahamu mbele yetu ndilo linatuweka katika matokeo haya!
Hatujui usahihi wa kweli ipi ndio maana tunatofauti katika Mungu tumuabudie!, kweli huwa haina mashaka ila uwezo wa ufahamu wako ndio unaamua ubebe kipi na uache kipi.
Kwa akili naufahamu wako umeamini kuwa wapo watu wameteuliwa kuwa karibu na Mungu, hivyo wanaweza kukusogeza karibu na Mungu! Kwanini sio wewe mwenyewe ikiwa wewe ni asili toka kwake?
Siamini katika Mungu wa mashaka ambae toka binadamu amekuwepo ktk dunia hii tunaambiwa yupo ila anawashukia wachache na hali ipo Kama hivi ilivyo! Hata kuthibitika kwake bado imekuwa ni mashaka au matendo yake hayathibitiki bali masimulizi!
Mungu ambae ameumba ulimwengu wenye sayari lukuki na akamtupa shetani katika dunia ambayo inaviumbe wake wapendwa! Mungu ambae anasema kwamba shetani amekuja kutujaribu hivyo ni kazi yake mwenyewe anaipima na Kama hukuwa sahihi basi unapewa adhabu! Sa nani hayupo sahihi ikiwa mimi nilieumbwa au yeye alieniumba?
Haitoshi yupo Mungu na Miungu iliyobumbwa kwa vito ambavyo vimetoka hapahapa duniania na tunaambiwa wao ndio walituumba!
Nfikiri tunasafari ndefu ya kufahamu ukweli juu ya nadharia ya Umungu na Mungu mwenyewe pamoja na chanzo cha ulimwengu.
Ila nikupe ukweli wote Dini ni matrix iliyotengenezwa na wachache wanaoujua ukwel ili kutawala wengne, soul zetu zimetoka kwa Mungu kweli na zinatambua Hilo, Ila akili zetu zimetekwa na matrix huku duniani, Cha msingi apo nikufanya juhudi binafsi za kiroho ili kujitambua wewe Ni Nan umetoka wap,umekuja kufanya nin na utaenda wap? Kumeditate Ni muhimu ili kuwa na utulivu na kufungua Soul zetu.
Well well well. Ninaomba utulivu wako kidogo.
1. Japo kua kila culture inaamini miungu yake lakini culture zote zina vitu vinavyofanana...A. Maisha baada ya kifo kwa mfano wa mizimu na mababu B. Uwepo wa ulimwengu mwingine usioonekana kwa macho C. Kuwepo kwa viumbe wengine wasioonekana kwa macho.
Hii inaonyesha kuwepo kwa vitu common kwa watu ambao hata hawako karibu kijeografia mfno. America kusini na Afrika mashariki.
2. Japo hapana evidence yoyote kuhusu kuwepo kwa miungu hiyo ila evidence inayotolewa na hizo culture ni evidence ambazo hata Wanascience hawana majibu. Mfano...Tunajua kuwa sayansi ya madawa asili yake ni waganga wa Jadi, pia Astrology asili yake ni waganga wa jadi...Culture zilikua zinajua vitu vingi kuhusu sayari na nyota kwa namba ambayo haielezeki kwa kuwa hawakuwa na teknolojia hiyo au satelite miaka hiyo.
3. Japo miungu ipo mingi kwa ajili ya uzazi wa mashamba, mvua, magonjwa, kuagua na elimu ya nyota..culture zote zinaamini kuwapo na Mungu mmoja aliyeumba vyote...wengine wanaamini ni jua, wengine nature etc.
Nina evidence nyingi ila nitakaribisha maswali ili nisichoke kuandika.
Inapokuja kwa mtu ambaye haamini kama Mungu yupo kwa sababu hakuna ushahidi.
1. Science pia haina uwezo wa kuprove kuwa Mungu hayupo.
2. Science ikisema hakuna ushahidi kuwa Mungu hayupo inashindwa kuelezea kwa ushahidi asili ya kila kitu moja wapo asili ya ufahamu...Kumbuka big bang na theory zingine zinaongelea matter kuform matter...Mwamba kutengeneza mwamba mwengine kisa kugongana inaeleweka kisayansi, Ila matter kutengeneza viumbe vyenye ufahamu na uamuzi na kijitambua ni kitu Science haiwezi kukijibu. How can matter make consiousnes?
3. Dunia na sayari zinaonekana zimekaa kwenye mfumo ambao haiwezekaniki kutokea kwa bahati tu.
Jua lingeongezeka joto hata kidogo au kupungua hata kdgo kusingekua na maisha, dunia ingekaa mbali au karibu kdogo na jua au na sayari zingine kusingekuwa na maisha, ng'ombe kula nyasi, nyasi kupita kwenye matumbo yanayosababisha gesi ambayo ikitoka inanufaisha nyasi ni kitu ambacho hakiwezi kitokea tu.
Huwezi kujiuliza kawanini kila ugonjwa na kila sumu inayopatikana kwenye nature kuna tiba yake hapo hapo? Hiyo yote ni kwasababu vitu viligongana hewani kutengeneza dunia na sayari?
Hujiulizi kwanini kuna misimu na majira ya joto, baridi, mvua na ukame? Kwamba kungekua na vitatu kati ya hvyo kusingekua na maisha duniani?
Hujiulizi kama maisha ya viumbe vyote asili yake ni single cell organism kutokea baharini mbona bacteria hawabadiliki na kuwa watu? Fine inachukua mamilioni ya miaka, mbona bacteria walikuwepo tokea hapo?
Hujiulizi mbona bacteria wanamaamuzi binafsi ya kujongea kutoka eneo moja kwenda jingine japo kua hawana ubongo?
Hujiulizi kwanini DNA zetu na nyani zinalingana kwa asilimia 98 lakini sisi tunaenda hadi mwezini?
Bado nina vitu vingi kuliko nilivyoandika ila napenda kuwauliza swali moja. Utumie sayansi unipe evidence na measurement ya Hasira, Akili, Mawazo au hata nguvu ya mvutano!!!
Hivi vitu havina evidence inayoshikika wala kuonekana, ila haimaanishi kuwa havipo.
Namna ya kujua uwepo wa Mungu ni kuangalia dunia na maisha kuwa vitu hivi havijatokea by chance na haiwezekaniki kila kitu kikawa precise kama vimedizainiwa perfect kwa ajili ya kusapoti maisha.
Naamini huamini kuwa ulikua nyani eti?