Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?


Kama Zanzibar sio inchi nenda kawaeleze huko Zanzibar Sie watanganyika tunataka Katiba mpya ambayo itarekebisha upuuzi wote.... "Mbowe sio Gaidi"
 
Sio kuwa ni Viongozi wa JMT hawawatambui Viongozi wa SUK, no Viongozi wanawatambua na wamewekewa hadi protocal yao wawapo huku Bara, ila katiba ya JMT ndio haiyatambui mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ya 2010 yaliyo unda SUK kwasababu mabadiliko hayo yanakwenda kinyume cha katiba ya JMT.

Kwa mujibu wa katiba ya JMT, Tanzania ni nchi moja ya Jamhuri ya Muungano. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT.

Kwa mujibu katiba ya Zanzibar, Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa nchi 2. Zanzibar ni moja ya nchi hizo mbili zinazounda JMT.

Hivyo kwa katiba ya JMT, nchi ni moja tuu, JMT, Zanzibar sio nchi, bali ni sehemu ya JMT. Lakini
kwa katiba ya Zanzibar, Tanzania ni nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, hivyo Zanzibar ni nchi.

Viongozi wa SUK wanatambuliwa ki protokali tuu lakini ndani ya katiba ya JMT, hawatambuliwi.
P
 
mzee wacha porojo na uwongo Please tuelezee ni vipi Tanganyika wamepoteza sovereignity please no porojo na pia utueleze ni nini maana ya sovereignity na tanganyika wapeipotezaje kwa hisani yako please please
 
wacha ujinga ni haki gani mzanzibari anazopata
 
Bro huwa nakukubali kwa uchambuzi,ulifaa wakupe hata ukatibu mkuu wa chama,
 
Bro huwa nakukubali kwa uchambuzi,ulifaa wakupe hata ukatibu mkuu wa chama,
Mkuu JUAN MANUEL , mimi sihitaji uteuzi wowote, usiwasikilize hawa hawa baadhi ya wajinga wajinga wa humu JF, wanaodhani Pasco Mayalla anafukuzia uteuzi.

Mtu ukiwa mzalendo unajikuta una wiwa kulisaidia taifa lako. Ili mtu ulisaidie taifa sio lazima uteuliwe kumsaidia Mama. Sisi wengine kama mimi tunaweza kulisaidia taifa vizuri zaidi huku tukikosoa kuliko hata ukiteuliwa.

Mfano mimi nakamilisha tuu taratibu, kipindi changu cha Kiti Moto2 kinarudi hewani. Sasa unawakaribisha watu kama hawa na kuwabananisha hivyo kulisaidia taifa. Mfano nikimualika Askofu Gwajima kwenye kipindi changu, kesho yake asubuhi yeye mwenyewe anaongoza kuwaswaga kondoo wake kwenye kuchanja!.
P
 
Ungekuwa karibu na Mungu ungesema, aliyesema Mbowe ni gaidi ni Muongo. Aliyesema wenzake Mbowe wameshafungwa ni muongo. But kwa sababu unataka kuwaunga wanaofurahia inflicting pains to other hakuna siku utatumia zawadi uliyopewa na Mungu kuwatetea innocents who are captives of CCM.
 
Kama Zanzibar sio inchi nenda kawaeleze huko Zanzibar Sie watanganyika tunataka Katiba mpya ambayo itarekebisha upuuzi wote....
Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, serikali mbili na katiba mbili. Katiba moja ya JMT ya mwaka 1977 imesema Tanzania ni nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT.

Katiba ya pili ni katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, ambayo ilirekebishwa mwaka 2010 inaitambua Zanzibar kuwa ni nchi na ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT.

This is contradiction.
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, Katiba ya Zanzibar ni Batili !. Ila kwa vile JMT inaendeshwa na katiba ya JMT na huo ubatili wa katiba ya Zanzibar hauhusu JMT, serikali ya JMT haijaingilia kati kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar yasituhusu. Ilichofanya katiba ya JMT ni kujinyamazia tuu kimya hivyo huo ubatili wa katiba ya Zanzibar, hauingii huku Bara, lakini ndani ya Zanzibar, katiba hiyo ni halali kabisa.
P
 
Katiba ibadikishwe haiwezekani nchi moja iwe na maraisi wawili na wote watoke upande mmoja wa wenye population isiyozidi 2M. Wakati wale 58M wamebaki wakibungaa macho tu. Utaratibu huu unakiuka maana halisi ya Demokrasia wengi wape wachache waheshimiwe mawazo yao.
 
Haya ya kuwepo kwa mawaziri na wabunge siyo uthibitisho wa Zanzibar sovereignty.
Katika hali ya kawaida, bila uwepo wa serikali moja, Zanzibar haiwezi kuwa na nguvu kwenye serikali ya Tanzania.
 
Gonjwa lile lile LA asili. Kutukuza Ukuu wa katiba ya JMT na kuacha kabisa hati za makubaliano ya Muungano ( Articles of Union) ambazo ndio msingi. Hio uniqueness ya Muungano huu ya Tanganyika kujigeuza kuwa Tanzania ndio inayojustify kwamba ni Zanzibar pekee iliyopoteza sovereignty.

Ubishi wa kujificha kwenye katiba mtoto wa kutengenezwa kwa ujanja wa kuimeza Zanzibar haukubaliki.

Shawishini kubadilishwa Katiba kila upande upate haki zake. Ujanja haufai.

Hata ujanja wa Katiba Pendekezwa kuweka kufungu cha Ukuu wa Katiba kuwa ya JMT ulishtukiziwa. Jini Tanganyika litoke kwenye chupa kwanza. Tupate fursa ya kuweka Muungano wetu sawa na kukubaliana mambo yetu kutokana na mahitaji ya sasa.

Acheni mbinu za kizamani kunyamazisha watu kwa mgongo was Katiba inayolinda Tanganyika kwa kiini macho.

Watu wanafurukutwa hapa. Tanganyika haijapoteza Sovereignigy by practice. Kila inachotaka inakipata lkn Zanzibar haiwezekani.

Acheni unafiki. Hio ndio mantiki ya Makamo was 1.
 
Huyo mtu ni hatari kwa Muungano toka enzi hizo .
 
Tanganyika na sisi tunataka Rais wa serikali yetu baada ya hapo ndio hili la Rais wa JMT na makamo wake wapatikane kutoka sehemu yeyote ya Muungano kwa kubadilishana liwe na mashiko.
 
Sidhani kama Zanzibar ilipoteza sovereignty yake kwa sababu zifuatazo;
1. Zanzibar ina Rais wake na ana makamu wa kwanza na wa pili
2. Zanzibar ina Baraza lake la Mawaziri ila tu haina baadhi ya wizara kama mambo ya ndani, mambo ya nje, ulinzi, nk.
3. Zanzibar ina Bunge lake, wao wanaliita Baraza la Wawakilishi
4. Zanzibar ina Mahakama zake na Ina Jaji mkuu na majaji wengine. Kwahiyo ina Rais, Bunge na Mahakama.
5. Zanzibar ina vikosi vyake vya ulinzi (vikosi maalum zaidi ya vitatu) ila vimewekwa chini ya Wizara ya Serikali za Mitaa
6. Zanzibar ina taasisi zake kama Takukuru yake, TRA yake, CAG wake, mamlaka zake za Bandari na viwanja vya ndege, soka lake, nk, nk.
7. Rais wa Zanzibar anateua wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa upande wa Zanzibar.

Sasa mnataka Zanzibar iwe na nini cha ziada ili iitwe nchi?

Mimi naona iliyopoteza ni Tanganyika ambayo haina chochote katika hivyo vyote!

Hayo ni maoni yangu binafsi
 


Sijui nani aliwadanganya Wtanganyika wakakubaliana na huu ujinga. Wao hawana nafasi ya kujadili mambo yasiyo ya muungano yanayo wahusu wa Zanzibari. Lakini Wazanzibari kupitia Bunge la JMT wananajadili mambo ya Tanganyika na kulipwa stahiki zote.

Hivi Watanganyika hatuzioni hizo fursa za ajira tunazozikosa kwa mfumo huu wa sasa? Tungekuwa na Rais wetu, makamo wawili, baraza letu la wawakikishi nk. Sijui nani ametuloga na hatujiongezi.
 
Tanganyika na sisi tunataka Rais wa serikali yetu baada ya hapo ndio hili la Rais wa JMT na makamo wake wapatikane kutoka sehemu yeyote ya Muungano kwa kubadilishana liwe na mashiko.
Wenzako hawataki hilo kutokana na Ajenda zao zilizojificha. "Yaani mtu kakupiga roba unaninginiza miguu, unaupapatua mkono wake anakwambia tulia vumilia hii ni kero itatatuka". Lakini anazidi kuukaza mkono shingoni kwako.

Ukihoji anakwambia Katiba yetu unaivunja.
 
Eti Zanzibar ina rais wake.Rais gani asyetambuliwa popote duniani? labda kidogo Oman na UAE ndio huwa wanampa hadhi huyo rais wa Zanzibar.Huyo Shein ameshashiba ndio maana anatetea huu utumbo .Hadhi ya Zanzibar itarudi tu iwapo Tanganyika itarudisha utanganyika wake maana iaonekana Tanganyika ndio Tanzania na Zanzibar sio Tanzania.Hata uanachama wa FIFA zanzibar imekataliwa inatambuliwa Tanzania tu TFF lakini wazanzibar hawaruhusiwi kugombea TFF wanaambiwa yenu ni ZFF ,wakati FIFA inasema waende kama TFF ya Tanzania maana zanzibar sio nchi
 
Pascal, hivi unadhani hii riwaya uliyoiandika humu, kuna ambaye hajui? Hivi wewe Pascal, uliyesomea sheria lakini hukuwahi kuwa mwanasheria, unadhani una uelewa kumzidi huyo aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar?

Umejibu kienyeji sana. Sidhani kama huyo Makamo wa Rais wa Zanzibar, alikuwa akimaanisha kama unavyodhani wewe.

Hii hoja imekuwa ikitolewa na wanasheria wengi, wa Tanzania bara na visiwani, kuwa katika Tanganyika na Zanzibar kuungana, Zanzibar ilipoteza sovereignity yake ila Tanganyika, Serikali ile ile iliyokuwepo ilijibadili na kuwa serikali ya Tanzania. Kilichobadilika ni jina tu. Mimi siyo mwanasheria, lakini huwa wanatoa hoja nzito ambazo ukizisikiliza zinashawishi kuliko hii riwaya uliyoiandika.

Hata kama hujawahi kuwa mwanasheria, lakini kwa elimu ile ya sheria uliyoipata, ulistahili kufanya argument more professionally kuliko ulivyofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…