vipik2
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 2,845
- 2,258
Wanabodi
Wale wenye access na Plus TV, watch now kipindi cha Uso kwa Uso, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman asema uongo wa wazi wa mchana kweupe kuhusu muungano wetu.
Masoud Masoud anadanganya uongo kuwa eti tulipoungana, ile 1964, ni nchi moja tuu ya Zanzibar, ndio pekee iliyopoteza sovereignity yake na kuikabidhi kwa serikali ya Tanganyika, lakini Tanganyika haikupoteza sovereignity yake, kitu ambacho sii kweli.
Ukweli ni kuwa, tulipoungana nchi zote mbili, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, nchi zote mbili zilipoteza sovereignity zake, kwa Zanzibar kupoteza sovereignity yake na Tanganyika pia ikapoteza sovereignity yake, tukaunda nchi moja mpya ya Tanzania. Nchi ya Zanzibar haipo na nchi ya Tanganyika pia haipo, kilichopo ni nchi moja mpya ya JMT, ambayo ina sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Mimi sitatizwi na uongo wowote wa kawaida ambao hauna madhara, lakini uongo mkubwa kama huu, kuhusu muungano wetu adhimu, la kutoka kwa mtu mwenye cheo kikubwa kama hiki, ni uongo wenye madhara makubwa sana kwa mustakabali mwema wa muungano wetu ambao una ill motives behind. Jee lengo la uongo huu ni nini?.
Wakati wa Bunge la Katiba, niliwahi kutoa angalizo hili kuhusu mtu huyu
na kweli Dr. Shein alimshughulikia.Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii
Wanabodi, Baada ya kupitishwa kwa katiba mpya tuipendayo ya serikali mbili, watu wote wenye hoja za serikali tatu, ni watu wa hatari sana kwa mustakabali wa taifa hili. Mmoja wa watu hawa ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, huyu ni mtu hatari sana kwa mustakabali na majaaliwa ya kupitishwa kwa...www.jamiiforums.com
Muungano wetu ni muungano wa nchi mbili zenye hadhi sawa sawa, hakuna mkubwa wala mdogo, ndani ya muungano Tanganyika na Zanzibar ziko sawa sawa na zote mbili zilipoteza sovereignity zake na kuikabidhi kwa serikali ya JMT.
Muungano wetu ni aina ya muungano very unique duniani, kimataifa muungano wetu ni union wa nchi mbili zimeungana na kuunda nchi moja ya Tanzania. Hivyo Tanzania kimataifa ni nchi moja ya JMT, ni taifa moja, ni dola moja yenye rais mmoja, rais wa JMT ambaye ni Samia. Pia tuna Amiri Jeshi Mkuu mmoja tuu. Kimataifa Zanzibar sio nchi, Zanzibar ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.
Muungano wetu ndani ya muungano, muungano wetu ni muungano wa nchi mbili, yaani federation, hivyo ndani ya muungano, Zanzibar ni nchi, yenye rais wake, serikali yake, ina katiba yake, ambayo mabadiliko yaliyofanywa 2010 kuunda SUK, hayatambuliwi na katiba ya JMT. Kwa vile ndani ya muungano Zanzibar ina mamlaka yake huru bila kuingiliwa na serikali ya JMT, la katiba hiyo ni kwa ajili ya mambo yake ya ndani, japo katiba hiyo iko kinyume cha katiba ya JMT, lakini kwa vile ni ya ndani ya Zanzibar,
Kwa upande wa GNU au SUK,
ni serikali ya coalition. Kwenye coalition zote kuna the majority na a minority. A minority ndani ya coalition anatekeleza sera za à majority. Hivyo Viongozi wa ACT ndani ya serikali ya SUK ya Zanzibar, wanatekeza sera CCM.
Hivyo Viongozi wote wa ACT Wazalendo waliomo ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar wanapaswa kuhubiri na kutekeleza sera za CCM, hivyo hata wanapoalikwa popote kwenye public, watatanguliza maslahi ya Zanzibar kwa mujibu wa sera za chama tawala.
Sasa mtu huyu ndio yuko ndani ya nyumba, yuko jikoni kabisa, asipothibitiwa, amini usiamini, amini nawaambieni akija tokea kufika kule juu kileleni, very soon, tutagawana fito!.
Paskali
Correction
Asante sana, anayezungumza ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe
Othman Masoud Othman Sharrif sio Makamo wa Pili. Naombeni sana mnisamehe kuwachanganya hawa Makamo wawili, hivyo vyeo vya Zanzibar ambayo havitambuliki ndani ya katiba ya JMT, vinatuchanganya sana sisi wengine ambao ni waumini wa supremacy ya Katiba ya JMT na sio katiba ya Zanzibar. Kama katiba yetu ya JMT haiwatambui Makamo hawa, who M I nisiwachanganye ?.
Mixing is highly regreted. Mode please do the needful.
P
Kama Zanzibar sio inchi nenda kawaeleze huko Zanzibar Sie watanganyika tunataka Katiba mpya ambayo itarekebisha upuuzi wote.... "Mbowe sio Gaidi"