Kuhusu mwanamke mjamzito aliemwambia mume wake akatumie kisu na mikasi kumzalisha, Chalamila ametoa utetezi hauna kichwa wala mdomo, wa hovyo kabisa!

Huyu ni mkuu wa mkoa wa ajabu sana, kiufupi hana akili
 
Kwa akili yake huu ndo anaita Ufafanuzi? Kwa mwanamke akitumia hela vibaya ndo akapasuliwe na mumewe?
 
Huyo ni kichwa maji, elimu yake haijamtoa ushamba, kichwa chake hakina uwezo wa kuchakata kipi azungumze kipi ameze.
Kwa viongozi wa namna hii hatuwezi fika mahali.
 
Hivi kuzaa si wanasema ni bure
Sio bure na haijawahi kuwa bure ila kuna kipindi ilikuwa afadhali kuliko sasa.
Masikitiko ni kauli ngumu isiyo na uweledi kutoka kwa mtu ambaye ni mkuu wa ulinzi na usalay wa mkoa mkubwa na wa mfano wa dar es laam.
 
Basi ndio maana anazidi kuropoka, maana alishatikisa kiberiti akaona hakina njiti ndani, mteuzi hana kauli kwake, labda anajua siri zake je?
Mteuzi hana nguvu akimuona RC Chalamila
 
Huyo ni kichwa maji, elimu yake haijamtoa ushamba, kichwa chake hakina uwezo wa kuchakata kipi azungumze kipi ameze.
Kwa viongozi wa namna hii hatuwezi fika mahali.
Lakini ndo ukweli Sasa mtu huna uwezo wa kutoa elfu 50 ya huduma ya kujifungua huyo mtoto utaenda kumlea vipi atakula Nini?
 
Alivyokuwa RC mwanza mama alimpiga benchi akaenda ikulu analia makamasi yanamtoka kama mtoto kuomba msamaha
Mbona awamu hii anamuacha tuu
Anatia aibu Jiji
 
Alivyokuwa RC mwanza mama alimpiga benchi akaenda ikulu analia makamasi yanamtoka kama mtoto kuomba msamaha
Nakumbuka! Mama alikuwa anafanya zira akawaambia watu wako huru kuandika mabango ya ujumbe, hata wakitaka kutukana sawa tu!
 
Mkiambiwa ukweli hamtaki, sasa mnataka muendelee kudanganywa kama tunavyodanganywa na CCM kwa zaidi ya miaka 60 tungali masikini
 
Katika RC wa hovyo ni huyu mm sijajua kwanini Rais alimrudisha katika wadhifa huo baada ya kumuengua.
Ni mropokaji asiyeweza kufuatilia mambo ya msingi kwa faida ya wananchi.DSM sasa hivi ni shaghala baghala kila kitu kama vile hamna utawala.
Leo nimepita njia ya mabibo sokoni nikajikuta natusi serikali kwa sauti nikiwa ndani ya gari.
Yani vituo vya daladala pale sokoni ni wamachinga wa ndizi wamepanga ndizi na kituo cha upande wa pili ni boda boda wamepaki hivyo daladala zinasimama katikati ya barabara.
Kutoka NIT mpaka ufike zile taa za kuunga moro Road nimetumia dakika 25 wakati ni kipande cha mita 120.
Sasa unajiuliza hii serikali ipo kweli?
Mama anapaswa ajue huyu anasaidia kupunguza kura za ccm .
 
Lakini ndo ukweli Sasa mtu huna uwezo wa kutoa elfu 50 ya huduma ya kujifungua huyo mtoto utaenda kumlea vipi atakula Nini?
Una umri gani mzee!? Kuna watu elfu 5 ya kula wanaibahatisha, ila kuipata 50 ndio kimbembe, jamani tembeeni muone hali zilivyo nchini.

50 unaitaja eazy tu, kuna watu 50k ni kipengele kikubwa kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…