Kuiba Trillion 2 halafu kesho yake unamwambia mtu lipa kodi kwa maendeleo ya taifa ni matusi, hii inauma sana

Kuiba Trillion 2 halafu kesho yake unamwambia mtu lipa kodi kwa maendeleo ya taifa ni matusi, hii inauma sana

Mimi naamini mojawapo y vitu vitaanzisha migomo na maandamano yasiyoisha hapa Tz ni wizi,ufisadi na ubadhirifu serikalini.Mimi ni mfanyakazi wa serikali na ni mfanyabiashara pia.Nikijumlisha fedha ninayokatwa kama PAYE,na kodi kwenye biashara ni hela nyingi mno kwa mwaka.Ajabu ikotoka ripoti ya CAG wizi ni mkubwa mno!Ripoti ya CAG inanileteaga stress sana.Kwa namna hii mtu unaweza hata kufikiria kukwepa Kodi,maana hata ukilipa halali zitaishia kuibwa na wakora wenye fursa serikalini.So sad [emoji22]
 
Halafu
Kuna wakati leo nimekaa natafakari sana jinsi tunavyobanwa katika kila angle ili tulipe kodi, hasa hasa hili suala la tozo za miamala, linaumiza sana.

Halafu unakuja kuambiwa watu wanaiba pesa tulizolipa kodi, nasikia kuna hadi trillion 2 zimelambwa. Hapa nimetoka kutuma pesa haifiki hata laki 5, imeondoka karibu 7k makato tu ya ajabu ajabu, nimejikuta moyo unaniuma sana, yaani moyo unaniuma nyieee.

Rais tuliyempa dhamana ya kutulinda na kutuvusha salama hadi 2025 yupo na anaona na anasikia, the best she can do ni kusema ‘Stupid!’ basi? Madame president is that the best you can do?

You people up there Ikulu, who do you think you are? Hivi mnadhani mnaongoza nguruwe? Mnataka kitokee nini ndio mjue kuna watu wanapaswa kubadilishwa? Please, mi naumia sana, kweli naumia, hizo pesa zinaniuma mno!

Kulipa tozo hadi mnakamua watu damu, halafu mnaiba tu like nobody’s business, hakuna anaechukuliwa hatua, maana yake nini? Hii dharau ya aina gani hii, halafu mnatuambia mambo ya kulipa kodi? Kweli, what do you take as for?

Hivi kwani uwaziri ni jina la ukoo kwamba mtu hawezi kubadilishwa? Mnatukatisha tamaa. Kwani nyie viongozi wetu mnahitaji kuiba kiasi gani ndio mridhike? Si muwe mnaiba hata milion 100 then maisha yanaendelea, sasa kweli unaina trillion 2 halafu iweje? Makusanyo ya watu milioni 60 kwa muda wa miezi miwili wewe unachukua unatia mfukoni?

Mna mioyo ya chuma kwani jamani? Waoneeni huruma watoto wa binadamu wenzenu jamani, ibeni ila angalieni na urefu wa kamba, tuibe kwa huruma, kwani hamna dini nyie, yaani trillion 2 hata siamini. Yaani moyo unaumaa, hivi nyie Watanzania trillion 2 mnazichukukije kwani? Nchi zingine hai wahusika wangekuwa wananing’inia kwenye mti, mfano China huu ujinga huwezi kufanya.

Sasa nasemaje, hizo trillion 2 zirudi, otherwise 2025 tutaondoka na kichwa cha mtu, sisi sio nguruwe, ni binadamu!

View attachment 2627251
Halafu waTanzania tuna tabia za mahaba niue ikitokea tukampenda mtu, kama ambavyo Samia alikuwa kaingia kwenye mioyo yetu, lakini yeye kwa dhahiri tumeona hatupendi raia wake!

Mtikisiko ulitokea Kariakoo na mwangwi kupazwa nchi nzima kuonesha udhaifu wa Serikali yake na yeye kushindwa kuchukua hatua immidietly kadhihirisha ninayoongea.

Kuna watu walikuwa wanamkingia kifua kwa utetezi mandazi, kuwa uozo huu ni wa wasaidizi wake, lakini sasa kwa kutokuchukua hatua kajidhihirisha kuwa kiini cha matatizo yote tunayoyapata waTz ni yeye!

Tumeshajua kuwa analinda genge lake alilolitengeneza kwa maslahi anayoyajua yeye na hawezi kwa vyovyote vile kuwatoa kwenye hivyo vyeo kwa namna yoyote ile.

Ukisikia kaleta mabadiliko kwenye baraza lake hilo ni ile pindua pindua ya kiini macho kama alivyofanya kwa maRC, wa huku peleka kule lakini sura ni hizo hizo na matendo yao ni hayo hayo.

Kwa kuwa tumeshaona dosari kwenye serikali hii nzima, shime waTz mwaka wao wa ukandamizaji uweni huu na ifikie mwisho.

Tusisubiri hadi 2025 wataifirisi nchi hawa na watakuja na hadaa chafu za kupoka uchaguzi na kubakia madarakani.

Iwe kwa heri ama kwa shari, lazima tuwafurushe hawa wakoloni weusi ili tuanze upya.

Na kuanza upya siyo jinga, hatujachelewa, muda wa mabadiliko ni sasa.
 
2025 mbona mbali sana, kama ni kutegemea uchaguzi tutambue nao hauna msaada maana wahusika wanajua cha kufanya kuufix.

Ni wakati sasa wa raia kujitetea kwa namna wanayoijua wenyewe hata ikiwa kuwapopo na mawe ikibidi
 
Raisi gani wa nchi hii alie wahi kufanyia kazi ripoti ya CAG tangu tupate uhuru?
Sasa kama ripoti za CAG hazifanyiwi kazi, na wizi unaendelea kila mwaka, kwanini tunaingia gharama ya kuwa na ofisi ya CAG na wafanyakazi wake, na wanalipwa mishahara minono na marupurupu kibao na gharama za uendeshaji wa ofisi?

Si bora hiyo ofisi ya CAG ingefutwa tu?

Yani kila mwaka, tunaingia gharama za kuja kuambiwa kuwa tumepigwa, na hatua hazichukuliwi, why? [emoji56]
 
Halafu

Halafu waTanzania tuna tabia za mahaba niue ikitokea tukampenda mtu, kama ambavyo Samia alikuwa kaingia kwenye mioyo yetu, lakini yeye kwa dhahiri tumeona hatupendi raia wake!

Mtikisiko ulitokea Kariakoo na mwangwi kupazwa nchi nzima kuonesha udhaifu wa Serikali yake na yeye kushindwa kuchukua hatua immidietly kadhihirisha ninayoongea.

Kuna watu walikuwa wanamkingia kifua kwa utetezi mandazi, kuwa uozo huu ni wa wasaidizi wake, lakini sasa kwa kutokuchukua hatua kajidhihirisha kuwa kiini cha matatizo yote tunayoyapata waTz ni yeye!

Tumeshajua kuwa analinda genge lake alilolitengeneza kwa maslahi anayoyajua yeye na hawezi kwa vyovyote vile kuwatoa kwenye hivyo vyeo kwa namna yoyote ile.

Ukisikia kaleta mabadiliko kwenye baraza lake hilo ni ile pindua pindua ya kiini macho kama alivyofanya kwa maRC, wa huku peleka kule lakini sura ni hizo hizo na matendo yao ni hayo hayo.

Kwa kuwa tumeshaona dosari kwenye serikali hii nzima, shime waTz mwaka wao wa ukandamizaji uweni huu na ifikie mwisho.

Tusisubiri hadi 2025 wataifirisi nchi hawa na watakuja na hadaa chafu za kupoka uchaguzi na kubakia madarakani.

Iwe kwa heri ama kwa shari, lazima tuwafurushe hawa wakoloni weusi ili tuanze upya.

Na kuanza upya siyo jinga, hatujachelewa, muda wa mabadiliko ni sasa.
Kwakweli kwa usalama wao, huyo Mwigulu achomoke na hizo trillion 2 zirudi! Kinyume cha hapo hii chuki itakuja kulipuka vibaya sana, inaumiza sana...
 
Hii nchi haiwezi kuendelea chini ya CCM hata iweje na ukizingatia Mama anashauriwa na kilaza (Kikwete) ndiyo kabisaaaa. We fikiria mtu nchi ilimshinda na leo hii unamchagua kuwa mshauri wako, is she really serious? Mama Samia ajiuzuru tu hatuoni uongozi wake.
 
Ukitaka kujua hii nchi inawajinga wengi soma ripoti ya CAG. CCM hoyeee, mmejua kutunyoosha wachawi nyie.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na wewe, hapa inatakiwa kulamba Shaba fisadi Moja baada ya jingine.
 
Watu wanagawa Bandari kwa kampuni za kihuni harafu unawaambia walipe kodi unazungumzia kuiba 2 Trilion mbona hiyo cha mtoto...
 
Halafu anatokea boya mmoja anataka kulazimisha mwalimu achangie mchango wa kukimbiza Mwenge hii Nchi Bora kuzaliwa mbwa hata Rwanda tu
 
Ut
Ngoja tuone 2025
Utafanya nini?
Wale wa goli la mkono bado wapo.
Waliotupoka ushindi 2015 kina Nape na Makamba na Mwigulu bado wapo. Na unaambiwa watu wema hawafi.
2025 itakua Kama 2020 au zaidi.
 
Ngoja tuone 2025
mtafanya nini na tume ni ile ile tena Kailima mchakachuaji namba moja karudishwa kule ili achakachue vizuri hiyo 2025? tumepigwa na kitu kizito bado tunasema tusubiri , hapa nawakubali wakenya kitu kikiwa ovyo wana react fasta sio sie wadanganyika, haki ya mtu haiombwi inadaiwa tukiweza hayo nchi itanyooka sana tu.
 
Back
Top Bottom