Kuidharau Yanga SC ikielekea CAFCC Semi ni Ushamba na Simba SC haijawahi Kucheza Fainali ya CAFCC

Unakubali jina limebadilika na mfumo wa uendeshaji alafu unalazimisha kuwa ni lile lile?

Shida Sana
Wewe ndio Una shida ndugu. Ligi yetu sasa hivi ina timu 16 ,inaitwa NBC premier League na iko chini ya TFF lakini hii hii ligi sio mara zote tangu kuanzishwa kwake ilikuwa na timu 16 na iliitwa NBC premier League na ilikuwa chini ya TFF.

Kwa hiyo timu inaposema imechukua ubingwa wa ligi mara 22 sio sahihi? Kwa hiyo timu iseme imechukua ubingwa mara 10 enzi za FAT mara 5 enzi za TFF , au iseme imechukua ubingwa mara 6 timu shiriki zikiwa 12 na mara Saba timu shiriki zikiwa 16?
 
Kwa kuwategemea kina Mwaikimba na Ditram Nchimbi unategemea ufike wapi kwenye michuano ya CAF?

Yanga unayoiona ni kama tumeiazima AS Vita watupe timu na kuleta kocha mzuri ndio hiki unachokiona, kwa sisi wenyewe tungekesha miaka yote hata ukibahatisha kuingia makundi lazima ugeuzwe jamvi la wageni.

Wachezaji wazawa wasipojifunza kitu kwa hawa Wacongo ndio basi tena, maana upande wa wanamuziki wanacopy vizuri tu sebene za Wacongo, wachezaji wanashindwa vipi kucopy? Wacongo wametuzidi kwa mbali sana.
 
Mshidi halafu shirikisho ni kitu kimoja?. Wacheni mchezo kufeli ni kufeli tu sawa?.
 
hizo ndo akili za watanzania
 
Bado haibadilishi ukweli kuwa shirikisho ni michuano ya mazezeta yaliyofeli CHAMPIONS LEAGUE.
Baki hivyo hivyo na hiyo akili ya kimbumbumbu.

Kazi yetu Yanga ni kufuta Kila excuse ya mashabiki wa Simba! Hamtuiti Tena wa matopeni, Hamtuiti Tena wapanda mabasi kuelekea Manungu Huku nyie mkichukua Mwewe kwenda ulimwenguni, na Sasa Ijumaa mechi na Wydad ni nyie mnaoumaliza mwendo wa kudaka Mwewe , ijumaa mnakandwa (7-0) mnarudi matopeni Buza kwa Mpalanger, Huku Mtani wenu Yanga tunatinga nusu fainali Shirikisho na kuendelea kupaa na "Mwewe" (ndege kwa wasiojua).

Tunabeba NBC league cup second season tunapata uzoefu mashindano ya kimataifa kupitia Shirikisho kwa kushinda mechi za ugenini sasa msimu ujao tukutane Klabu bingwa Afrika, maana Al Hilal walijiangusha mechi zote mbili ikawa sio soka Tena, na kawaida yetu ukitupiga kama Rivers United kisasi ni lazima hao Al Hilal tupangwe nao Tena watajua Yanga ni nani! Sasa Mtani muda huu ni vizuri uanze kutafuta kitu kingine Cha kujifariji maana msimu ujao Utopolo fc tutakushangaza klabu bingwa Africa !

Hebu tufikiri kidogo, hivi looser ni Simba asie na kombe lolote zaidi ya lile la kina Yakhe au Yanga inayojitafuta na kupambana kupata Mataji ligi kuu na kimataifa?
 
Kwa kipindi hiko mashindano yalikuwa matatu ila mashindano yenye hadhi yalikuwa mawili tu ambayo ni African cup of champions club na African cup winner's cup.

Shindano la kwanza lilikuwa linaitwa Afirican cup of champions club.
Hili ndio kwasasa ni sawa sawa na klabu bingwa kwahivi sasa, na timu zilizotakiwa kushiriki hii michuano ni zile tu zinazobeba ubingwa wa ligi kuu.

2) Africa cup winner's cup

Hili ndio ni sawasawa na kombe la shirikisho kwa hivi sasa, timu ambazo zilizokuwa zinazishiri ni timu ambazo zimetwaa ubingwa wa kombe la FA kwenye mataifa yao. Kama ikitokea aliyebeba kombe la FA ndio huyo aliyebeba na ligi kuu basi aliyecheza nae fainali (runner up) ndio atakayefuzu kucheza hili kombe la African cup winner's cup

3) CAF cup

Haya ni mashindano yaliyoanzishwa na Mnigeria kama kwaajili ya timu zilizoshindwa kufuzu mashindano ya kimataifa ya CAF.
Timu ambazo zinashika nafasi ya pili, na zilizoshindwa kufuzu mashindano ya CAF ( African cup winner's cup na African cup of champions club)
CAF cup ilianzishwa mwaka 1992 na mwaka 2003 ndio ikawa mwisho wa mashindano hayo hivyo yalidumi kwa miaka 12 tu

HITIMISHO

Kwanini African cup winner's cup ndio ni sawasawa na shirikisho kwasasa?
Sababu ya kwanza ni kama nilivyoeleza juu mfumo wake upo sawasawa na ilivyo CAF confederation cup.
Sababu ya pili ni CAF super cup
CAF super cup ni shindano linalohusha mabingwa wa kombe la CAF interclub yaani kombe la shirikisho na kombe la mabingwa.
Katika kipindi hiko kabla ya kuanzishwa kwa CAF confederation cup, CAF super cup ilikuwa inakutanisha bingwa wa African cup of champions club VS bingwa wa African cup winner's cup.

Katika mwaka 1993 bingwa wa African cup winner's cup alikuwa ni Al Ahly na bingwa wa African cup of champions club alikuwa ni Zamalek. Hivyo wakakutana kwenye CAF super cup mwaka 1994 na bingwa akauchukua Zamalek wa CAF super cup.

 
Ok! Sasa nje ya Kombe la Washindi kulikuwa na mashindano gani mengine ya CAF yalishirikisha vilabu vya nchi husika?
 

Mchambuzi wangu bora zaidi wa muda wote, thumb up kwako huwezi kuwa mpenda soka afu ushindwe ku- recognize mafanikio ya team pinzani yako…..
 
We jamaa kumbe unaakili sana ila huwa unazirusha tu (unajifanya hamnazo).
Subiri MAKOLO wakupopowe na kukuita UTO.
 
Shida kubwa ni wivu tu,, mtu akiwa na wivu atatafuta sababu yoyote ya ku-undermine mafanikio Husika ili mlengwa ujione si lolote si chochote.
Ikumbuke kuwa Hatua hizihiz ndizo Makolo waliliabisha Taifa letu kwa kufanya Ulozi mkubwa pale SA bila aibu Wala nishai..

Yanga hii sio yakujifananisha nayo..
 
Mkuu hiyo kitu ina impact kubwa sana kibiashara ndio maana husikii wakubwa wakikemea waache. Kuanzia kwenye mahudhurio ya uwanjani kwenye bidhaa za timu inawanufaisha sana na mimi sioni shida so long as inapohitajika kufanya jambo la timu linatekelezwa
 
Hakuna unachokojua aisee...
Fatilia vigezo vya kushiriki kombe la washindi
 
Subiri madongo toka kwa wafia timu wa Mudi wasiopenda kusikia ukweli
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji114] we kajamaa ni kambea sana ila Wiki iliyopita nilijaribu kuzoom comments zako sikuona hata Moja .
Yaan ulipotea jumla jumla baada ya kukandwa sawa sawa na mnyama[emoji1666]Cku ngapi hiz umeibuka gafla
 
Goli la Sakho liliopatikana kwenye kombe hilo waliansisha nyuzi kibao na kushangilia leo imekuwa vipi ndugu dundukaz ?
Shida ya nyie watu ni vilaza sana .
Kipindi anaongea msemaji wenu kuwa hilo hayo mashindano ni ya waliofeli mlimuunga mkono badala ya kumkataza huo ujinga wake ,na mlimuunga mkono sabab hamkua kwenye hayo mashindano.Leo hii mpo huko mnakumbushwa km ni sehemu ya waliofeli mnachukia wakat mwanzo mlisapot hicho kitu.
Badiriken msipende kubeza vitu wakat mnajua waz mnaweza pitia huko.
 
Usisumbuke Bure haya jamaa uwezo wa kuchakata mambo ni mdogo sana hata huku mtaan kwetu ni wengi sana alafu dizain wamezaliwa na mama mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…