Kombe la Shirikisho Ndio Hilo lilikuwa linaitwa la Washindi! Ambapo zamani hakukuwa na Makundi. Kwa hiyo kilichobadilika ni Jina na mfumo wa uendeshaji! Kumbuka awali aliyekuwa anashiriki ni Mshindi wa Pili, siku hizi zinashiriki hata Timu za Madara ya chini! Ndio maana Leo Kuna kina Marumo Galaxy ! + Loosers!
Kwa kipindi hiko mashindano yalikuwa matatu ila mashindano yenye hadhi yalikuwa mawili tu ambayo ni African cup of champions club na African cup winner's cup.
Shindano la kwanza lilikuwa linaitwa Afirican cup of champions club.
Hili ndio kwasasa ni sawa sawa na klabu bingwa kwahivi sasa, na timu zilizotakiwa kushiriki hii michuano ni zile tu zinazobeba ubingwa wa ligi kuu.
2) Africa cup winner's cup
Hili ndio ni sawasawa na kombe la shirikisho kwa hivi sasa, timu ambazo zilizokuwa zinazishiri ni timu ambazo zimetwaa ubingwa wa kombe la FA kwenye mataifa yao. Kama ikitokea aliyebeba kombe la FA ndio huyo aliyebeba na ligi kuu basi aliyecheza nae fainali (runner up) ndio atakayefuzu kucheza hili kombe la African cup winner's cup
3) CAF cup
Haya ni mashindano yaliyoanzishwa na Mnigeria kama kwaajili ya timu zilizoshindwa kufuzu mashindano ya kimataifa ya CAF.
Timu ambazo zinashika nafasi ya pili, na zilizoshindwa kufuzu mashindano ya CAF ( African cup winner's cup na African cup of champions club)
CAF cup ilianzishwa mwaka 1992 na mwaka 2003 ndio ikawa mwisho wa mashindano hayo hivyo yalidumi kwa miaka 12 tu
HITIMISHO
Kwanini African cup winner's cup ndio ni sawasawa na shirikisho kwasasa?
Sababu ya kwanza ni kama nilivyoeleza juu mfumo wake upo sawasawa na ilivyo CAF confederation cup.
Sababu ya pili ni CAF super cup
CAF super cup ni shindano linalohusha mabingwa wa kombe la CAF interclub yaani kombe la shirikisho na kombe la mabingwa.
Katika kipindi hiko kabla ya kuanzishwa kwa CAF confederation cup, CAF super cup ilikuwa inakutanisha bingwa wa African cup of champions club VS bingwa wa African cup winner's cup.
Katika mwaka 1993 bingwa wa African cup winner's cup alikuwa ni Al Ahly na bingwa wa African cup of champions club alikuwa ni Zamalek. Hivyo wakakutana kwenye CAF super cup mwaka 1994 na bingwa akauchukua Zamalek wa CAF super cup.