Kuifuta CCM sio kuondoa matatizo ya taifa hili. Hiyo ni propaganda yenye uongo Mkubwa

Kwahiyo mataifa yaliyopiga hatua ni kwasababu ya ubora wa malezi?

Kipi kilichopelekea mataifa hayo kufikia hapo, ni ubora malezi au uongozi?
 
Wew ni mtu Mwingine wa kuongeza kwenye ignore list
 
Upo Sahihi,cha kujiuliza ni kwamba,
Mbona hio hio ccm kuna vijana ambao sio machawa kabisa lakini wametoboa maisha kwa juhudi zao wenyewe??
Sisi maskini na wavivu ndo kila siku tunapiga kelele huku!!
 
Hivi mnajua kuwa Kenya Ina katiba mpya lakini maisha Yao ni close to worst?

Katiba sidhani kama itasaidia kuondoa tatizo.

sanasana itawapa watu uhuru WA kuandamana ovyo, na au mbinu mpya za mabepari kufanya Yao..zaidi...na zaidi..na zaidi..

Natamani tujitafakari wote taifa zima kabla ya hata kufanya mchakato WA katiba mpya, maana inaonekana kama vile ni wachache ndio wanataka haya mambo, huku wengi tukiwa hata hatuijui io katiba yenyewe.

Na kwanini tuhangaike kutoa boriti ya mtu mwengine wakati ya kwetu sisi wenyewe hatutaki itolewe? Ubinafsi upo na umekomaa kwenye ngazi ya familia, na mizizi yake ni mikubwa hatari kuliko hata ya huko juu. Nakuambia, hata mwananchi WA chini akipata nafasi, atakuwa mbinafsi, fisadi, na majina yote mtakayompa anapoona pa kula. Si sisiemu Wala demokrasia.

The greed is everywhere. Na hii labda ni Miungu mwenyewe ndio aje kutuhukumu..na hii ndio sababu inanifanya nisiipende Siasa, coz it moves people, and sometimes everyone into crazy wilderness
 
KUIFUTA CCM SIO KUONDOA MATATIZO YA TAIFA HILI. HIYO NI PROPAGANDA YENYE UONGO MKUBWA.
Napinga hili, CCM tunailaumu sababu imejenga mfumo wa hata hao waadilifu wachache wasindwe kuwa wazalendo maana maamuzi yote ya mwisho yapo kwa maslahi ya chama sio nchi!! Mfano DPP akimshtaki mfadhili wa CCM kwa kesi ya ufisadi lazima atatutumbuliwa maana akimfunga huyo mfadhili CCM itakosa maslahi yake!!!

Ila waadilifu wapo wengi tu ila katiba mbovu na mfumo mbovu wa CCM unawazuia kufikia potential yao. Mfano;
1.Sitta alijitahidi kuweka bunge huru ila CCM ikamuondoa 2010
2. JPM alijitahidi kuweka nidhamu utumishi wa umma
3. Mpina alipinga ufisadi kwenye sukari na nishati ila kakatwa.
4. OMO akiwa mwanasheria mkuu ZNZ alipinga vifungu vya katiba pendekezwa ila aliondolewa.
5. Gwajima kapinga utekaji kakatwa.

Maana yake ni kwamba hawa watu licha ya kuwa na MALEZI mazuri ila CCM imewakata kisa kupinga mambo ya hovyo au kutaka uhuru wa taasisi za kusimamia uwajibikaji.

So YES, CCM ikiondolewa kuna matatizo mengi yatapungua.
 
Asilimia 40% ni Ukoloni Mamboleo.
Binafsi ninaamini taifa letu bado halipo huru. Hicho ndicho ninajua. Ingawaje ukiniambia nikupe ushahidi naweza kukosa lakini ninachoamini ndivyo ilivyo.
Sio kweli, ni mawazo ya failures wanapenda kuweka lawama kwa watu wa nje ili kuepuka kuwajibika ndani!

Mbona Saudia ni kibaraka wa USA ila ina maendeleo? Rwanda mnasema ni puppet wa US ila mbona ana maendeleo? Maana yake unaweza kuwa na vita na mabeberu au ukawa unatumika na mabeberu ila bado ukawa na maendeleo!

Sasa sisi Tanzania karibu kila kitu tumewapa wageni mfano BRT, JNIA, Dhahabu, Uranium, Gesi n.k kipi ambacho hatujatoa bado hadi useme kwamba vita ya mabeberu ndio inafanya hatuendelei? Na kama wao ndio wanatukwamisha mbona hawamkwamishi Kagame kuleta maendeleo licha mnadai ni kibaraka wao?

Embu hii hoja iweke sawa
 
10. Ukisema ukaze watu wako wa chini wanakuwa sio waadilifu. Wanaungana na mabeberu wanakunyoosha.
Bahati nzuri au mbaya hao WATU ni 90% CCM members!! Ni nani ambaye sio CCM anaweza kutumiwa na mabeberu kupata tender ya madini au gesi? Nitajie mpinzani mmoja tu mwenye mamlaka hayo ya kugawa rasilimali?

Hayo yote yanakua solved na kuweka mifumo bora ya checks and balances kwenye KATIBA MPYA. Mfano hao wa chini wasipokua waadilifu ina maana Rais anaweza litumia bunge kuzuia hiyo mikataba mibovu ya kifisadi. Na sababu tume ni huru wabunge hawataogopa kuizuia maana wanajua ukiwakata bado watashinda hata wakiwa wagombea huru!!

Man Huwezi waondoa CCM kwenye lawama.
 
Hivi mnajua kuwa Kenya Ina katiba mpya lakini maisha Yao ni close to worst?

Katiba sidhani kama itasaidia kuondoa tatizo.
Based on what? Unatumia indicator zipi kusema hayo? Maana katiba inaongelea mambo mengi.
1. Devolution ina mafanikio yake binafsi hasa kusogeza maendeleo kwa muktadha wa eneo.
2. Chaguzi kuwa huru zimeongezeka accountability mfano 70% ya wabunge huwa hawatetei viti!!
3. Mahakama kuwa huru nadhani wote tunaona mpaka sheria kandamizi huwa zinapigwa stop, miswada ya bajeti pia huwa inazuiwa na mahakama!! Huoni imeokoa wastage kiasi gani?

So usiangalie tu uchumi wa mtu mmoja mmoja ambao unaweza sababishwa na unemployment na mfumuko wa bei alafu lawama ukaielekeza kwa katiba ambayo ina miaka 15 pekee!!
 
Unataka kusemaje?,kwamba hakuna watu waliolelewa malezi mazuri katika ukuaji wao lakini hatimaye wakaharibiwa na Mfumo-CCM?

Je,mtu yeyote mwenye maadili mema ndani ya CCM yupo salama?
 
Tatizo la jamii yetu siyo ubinafsi. Ni mila mbovu. Amini nakuambia Mtanzania hawezi mzidi ubinafsi Mmarekani. Nimeishi nao. Na bado Mmarekani ana maendeleo kuliko Mtanzania.
 
Ngazi ya familia itatengenezaje kizazi chenye maadili haliyakuwa;

1. Ukimkanya mwanao wa kumzaa kwa kumpiga akikushtaki sheria inakufunga, watunga sheria ni akina nani?

2. Asilimia kubwa siku hizi watoto wanaharibikia shuleni, shule ambayo kwa sasa haina faida yoyote ila mzazi akigoma kumpeleka mtoto wake anashitakiwa na kufungwa

3. Malezi ya watoto hadi utu uzima sio ya mzazi pekee, kwasasa ukishobokea mtoto wa mwenzako ukamkanya ukipelekwa kwenye mikono ya sheria unanyea debe au faini ya pesa sheria hizi nani anatunga?

4. Tukisema maadili na uadilifu ni pamoja na kuzuia vichochezi vya hivyo vitu mfano uvutaji wa bangi, uingizwaji wa midaharati nchini, mitumba na nguo zenye kutweza utu wa mtu, ajira kwa vijana ili wasiwe wezi nk je katika hili familia Ina mchango gani wa kuishinda Serikali?

5. Umegusia dini, dini ni nyenzo kubwa ya kulea watu katika maadili na uwajibikaji kama vile kukemea maovu ie wizi, umalaya, ufisadi, matusi na vitendo vyote vinavyosababisha mmomonyoko wa maadili kwa kutumia vitisho vya kiimani kuwa Mungu atawaadhibu na hawataipata pepo au hawatafika mbinguni swali je? Watumia midaharati na waliosoma elimu ya dunia wanaamini vitisho hivyo? Je wanastahiki kulaumiwa kuliko Serikali?

6. Njia nyingine inayotumiwa na dini ni kutoa adhabu kama vinavyoamlisha vitabu vitukufu ie Bible na Quran mfano mwizi akatwe mkono, mtembea na mke wa mtu auliwe kwa mawe, mzinifu apigwe viboko 80 nk je kwa kuzingatia sheria za nchi haya yanatekelezeka? Nani wa kulaumiwa kama sio Serikali inayosimamia hizi sheria?

Robert Heriel Mtibeli tuambie ccm ndio inayotunga na kusimamia sheria kwanini isibebe hilo jukumu ambalo wewe unasema hawahusiki?
 
Ngazi ya familia itatengenezaje kizazi chenye maadili haliyakuwa;

1. Ukimkanya mwanao wa kumzaa kwa kumpiga akikushtaki sheria inakufunga, watunga sheria ni akina nani?
Kwamba umtandike mtoto wako serikali ikufunge?
Unazungumzia kumpa adhabu ya kumuonya au kumfanyia Ukatili?


2. Asilimia kubwa siku hizi watoto wanaharibikia shuleni, shule ambayo kwa sasa haina faida yoyote ila mzazi akigoma kumpeleka mtoto wake anashitakiwa na kufungwa
Mtoto wa miaka 6 - 10 hawezi kuharibika kama wazazi wake mpo vizuri kumfundisha maadili.

Tatizo unakuta mtoto wa miaka 3 tayari anapelekwa shule. Mtoto hata hujamjengea foundation kama mzazi. Unapeleka akajengewe foundation na watu wengine.

Shule ya msingi lazima mtoto wako asomee shule ya kutwa na iwe karibu na unapoishi fullstop.

3. Malezi ya watoto hadi utu uzima sio ya mzazi pekee, kwasasa ukishobokea mtoto wa mwenzako ukamkanya ukipelekwa kwenye mikono ya sheria unanyea debe au faini ya pesa sheria hizi nani anatunga?
🤓🤓
Kwa nini umtandike mwanangu sio. Hapa kweli jamii imepuyanga.


Upo sahihi kabisa lakini elewa viongozi wa serikali ambao pia wanafamilia kwani ni wazazi kama wangekuwa waadilifu kikamilifu wangepiga marukufu na kuwa wakali kwenye suala la mihadarati, bange na dawa zingine za kulevya.

Polisi waadilifu wakija mitaani wakishughulikia matatizo ya vijana kama bange wanapigwa vita, wengine wanalogwa. Wazazi wanatetea watoto wao wasiwekwe ndani.

Nina visa mbalimbali na najua hata wewe unavyo. Kuhusu Panya road. Niliwahi kufuatilia miaka ya 2014 kule Tandale na manzese. Aiseeh wazazi wanahusika kwa asilimia 100.

Haya kuna Rafiki Yangu alikuwa mtendaji maeneo ya Kibati, huko Turiani. Alikamata Gunia Saba za Bange. Wale vijana akawaweka ndani. Wakamwambia watampa milioni 2. Mshikaji akakataa katakata.
Wazee wa kijiji, wazazi na diwani wakawa wanamuomba. Jamaa akakaza.
Alikuja ofisini kwangu pale Morogoro akawa ananihadithia kwamba ametishiwa kulogwa na jamaa anakuambia huko Turiani, hasa eneo la kibati sio lelemama.
Jamaa alikuwa na hofu.
Tayari polisi walishafungua jalada tayari kwa kwenda mahakamani.

Lakini huwezi jamaa alikufa kabla ya kesi kwenda Mahakamani. Ingawaje sitaki kuamini ulikuwa ni ushirikina. Lakini kwa mazingira aliyonisimulia Siku chache kabla ya kifo chake ninaweza kuamini kidogo.

Nimekupa mfano wa serikali inaweza kuchukua hatua lakini jamii ikawa haipo tayari.


Dini ni nyenzo muhimu katika kufunza maadili. Ni kweli.
Kulaumu sio suluhu Mkuu.

Mkuu serikali inaundwa na jamii. Yote unayoyaona yanafanywa na serikali kwasehemu yanatokana na jamii
 
Umepangua hoja yangu kwa mfumo wa upanguaji gia

Pia kuna some dots kwenye upanguaji zinashangaza

Mkuu unaleta Imani za kichawi kwenye inshu za kiserikali? Vipi tukisema wale walioua watu October 29 waliingiwa na majini waovu wakaua? Alooh

Pili, unasema ukatili wa mtoto! Unaupimaje ukatili adhabu kwa watoto zinategemea na kosa kuna kipindi mtoto anafanya kosa hadi mzazi haoni umuhimu wa kuwa na mtoto kama huyo kwa maana huruma inakaa pembeni akipewa adhabu stahiki akili zinarudi na kukaa sawa wewe ndio unaona ni ukatili? Haya Serikali Ina nini cha kufanya ambacho si ukatili ambacho kinazuia ushoga, uvutaji bangi, ulawiti, wizi na tabia zingine mbovu zaidi ya kuwavamia na kudai rushwa( kitendo ambacho pia kinahitaji adhabu ya kikatili) ambayo wewe hilo jumba bado waliangushia kwa jamii

Tatu, umeongelea wazazi kuwatetea watoto wao wanapofanya makosa, kwani mzazi ni nani? Ni kuwa wazazi wote wapo na maadili? Je wazazi wote wanaingia katika kundi hilo!?

Mtu akifikisha miaka 18 huyo sio wa mzazi tena ni wa jamii na Serikali je kati ya Serikali na jamii nani mwenye mkono mrefu kisheria za nchi? Nani wa kumuwajibisha akifanya kosa la kisheria na kimaadili kama sio Serikali? Au watu hawabadiliki?

Je hujawahi kuona kijana kalelewa vizuri ila akifika chuo anaharibika? Nani wa kumlaumu Serikali au mzazi?

Katika hili huwezi kutoa lawama hizi kwa Serikali ambayo kwa sasa inasimamiwa na ccm na pia huwa wanaapa wanapoteuana kulinda maadili ya nchi hii Wana wajibu wa kuhakikisha hayo yote yanakaa sawa kuanzia wao wenyewe hadi jamii nzima
 
Usitupange dogo

CCM inafutwa na tunaanza upya.

Kama inakuuma sana, futika pamoja na CCM
 
Umepangua hoja yangu kwa mfumo wa upanguaji gia

Pia kuna some dots kwenye upanguaji zinashangaza

Mkuu unaleta Imani za kichawi kwenye inshu za kiserikali? Vipi tukisema wale walioua watu October 29 waliingiwa na majini waovu wakaua? Alooh
😀
Mkuu MO29 dola ilikuwa na hofu na ilichofanya ni matokeo ya hofu. Hivyo ilifanya kutishia watu ili Jambo kama like lisitokee tena.
Mkuu hujawahi sikia mtoto anapigwa Hadi anakufa? Au hujawahi sikia mtoto anapigwa Hadi anakuwa mlemavu?

Sisemi watoto wasichapwe ila uchapaji uwe na haki

Sijawahi kuona aliyelelewa vizuri akaharibika.

Katika hili huwezi kutoa lawama hizi kwa Serikali ambayo kwa sasa inasimamiwa na ccm na pia huwa wanaapa wanapoteuana kulinda maadili ya nchi hii Wana wajibu wa kuhakikisha hayo yote yanakaa sawa kuanzia wao wenyewe hadi jamii nzima

Serikali inamchango wake kwa sehemu kubwa lakini mzizi wa serikali ni familia maana viongozi wote wametoka kwenye familia na wanafamilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…