Kuishi Dar ni ndoto ya Kila Mtanzania Kijana

Kuishi Dar ni ndoto ya Kila Mtanzania Kijana

Kwa sisi ambao tumezaliw jijin na kukulia apo popote tunaish ilimrad lengo la kpato lifikiwe🕊️
 
Nivigumu kukuelewesha ila ukivikosa hivyo vitu hapo juu ukiwa dar utateseka sana kuliko mtu ambae yuko mkoani. Au siku ukija kuishi huko dar utakuja kuona utofauti na huko mkoani
Hapa unamaanisha wewe unaishi wapi, mkoani au Dar?
 
ndoto ya Kila kijana ni kuwa na maisha safi kuwa na biashara safi/ Kazi yenye malipo mazuri ...kula vzr kulala vzr acc.kusoma vzr ...kuwa na afya njema
 
Life la dar mimi ndio sijalielewa kabisa especially joto kali, foleni barabarani, kila demu anajiuza(direct or indirect). Napambana tu niweke magoli yangu kwa sababu mzunguko wa hela dar ni mkunwa nikifanikiwa kuwa na mishe zinazojiendesha zenyewe naenda zangu kuweka maskani mkoani.
 
Dar ni Jiji la kwanza kwa maendeleo Tanzania na yamkini Afrika Mashariki.

Dar imejaa Fursa mbalimbali za kujikwamua Kiuchumi kwa kijana mtafutaji na mpambanaji hasa ambae ana lengo la kutoboa maishani. Lakini kijana huyu awe tayari kufanya kazi ya namna yoyote Mradi mkono uende kinywani.

Dar imejaa starehe na anasa za Kila namna ambazo asilimia kubwa sana zinawatoa kwenye reli vijana waliokuja kwa ajili ya kupambana, sababu damu inachemka hivyo starehe kwake inakua muhimu Sana kwa muda huo, changamoto vijana wengi wanashindwa kufikia malengo kwa kushindwa kubalance kati ya mapato na matumizi.

Dar ni sehemu hatari Sana kwa kijana ambae amekuja kiupambanaji lakini akawa mvivu wa mwili na akili akataka Kutumia short cut ili atoboe. Huyu ataangukia kwenye mikono ya ushoga, kubebeshwa madawa au kua jambazi/kibaka au utapeli. Maana ukubwa wa starehe uliopo utampeleka resi Apate pesa nyingi kwa haraka ili kumudu matumizi.

Dar ni sehemu sahihi sana kielimu kwa mtu aliyekuja kusoma, lakini kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni sehemu hatarishi pia hasa Kwa wale ambao hawakua na malezi sahihi toka kwao. Mtoto anakuja kusoma anarudi na ukimwi. Utashangaa mtoto wa first year ana iPhone 15 pro max ambayo hata mzazi wake Hana uwezo wa kumiliki. So kaipataje, KATOA MZIGO kwa wadau.

Dar ni njiapanda ya ndoto za vijana wengi wanaotaka kwenda kuishi ughaibuni. Hapa nipo michongo yote na connection huanzia. Ukiwa hapa utajua Nini maana ya green card na unaipataje, utajua balozi zote zilipo na Fursa zao.

Dar ndio sehemu ambayo mtu anakaa anatunga kamradi tu kwa hovyo hovyo na kanaitika anapiga hela. Yamkini aliyeanzisha marathon hakujua kama Utakua mchongo Mkubwa wa watu kupiga hela either binafsi au kupitia mashirika...

HIYO NDIO DAR, ONGEZEA YA KWAKO..


KARIBUNI SANA DAR ES SALAAM ILA MUWE NA PASSPORT (kidding)
kwa tafitiiii ipiii iyo uliyoifanya ukafikia hitimisho kwamb ndito ya kila kijana mtanzania ni kuish dar???? 2🤔🤔🤔
 
Unavyo ipamba dar utasema ni sehemu moja ya maana sana ..fika Sasa uone daah! Unaeza tamani kurudi ulipotoka muda huo huo ..uswahili mwingi sana humu dar, hakuna exposure yeyote yani hakuna mwingiliano mkubwa baina ya wenyeji na wageni hasa wa kutoka nje, kariakoo kama bwawa la mazi yani kila Kona ni harufu tu mbaya mbaya za vinyesi na mikojo vyoo vinatapishwa ovyo tu, joto hakuna namna, m'bu kama wote 😂😂😂😂
Huu mji wa dasalama ukija kizembe unaeza pakiwa mkongo ukiendekeza tamaa ..vijana wengi Wana left sana kwa kukimbilia material mazuri mazuri ..mademu nao wanaliwa kiasara asara yani balaa tupu ..kwa ufupi ni vurugu tu sema ndo hivyo pesa na connections nyingi unaeza pata ukiwa hapa..

Utapeli, ukuwadi, masikini wengi wanapatikana dar.

Ukitaka kula starehe vizuri aise nenda Chugastan, the City of God 😀😀
Hakuna sehemu tamu na yenyewe hadhi ya kula Bata kama Chuga.
 
Back
Top Bottom