Kuishi Dar ni ndoto ya Kila Mtanzania Kijana

Kuishi Dar ni ndoto ya Kila Mtanzania Kijana

Dar ni Jiji la kwanza kwa maendeleo Tanzania na yamkini Afrika Mashariki.

Dar imejaa Fursa mbalimbali za kujikwamua Kiuchumi kwa kijana mtafutaji na mpambanaji hasa ambae ana lengo la kutoboa maishani. Lakini kijana huyu awe tayari kufanya kazi ya namna yoyote Mradi mkono uende kinywani.

Dar imejaa starehe na anasa za Kila namna ambazo asilimia kubwa sana zinawatoa kwenye reli vijana waliokuja kwa ajili ya kupambana, sababu damu inachemka hivyo starehe kwake inakua muhimu Sana kwa muda huo, changamoto vijana wengi wanashindwa kufikia malengo kwa kushindwa kubalance kati ya mapato na matumizi.

Dar ni sehemu hatari Sana kwa kijana ambae amekuja kiupambanaji lakini akawa mvivu wa mwili na akili akataka Kutumia short cut ili atoboe. Huyu ataangukia kwenye mikono ya ushoga, kubebeshwa madawa au kua jambazi/kibaka au utapeli. Maana ukubwa wa starehe uliopo utampeleka resi Apate pesa nyingi kwa haraka ili kumudu matumizi.

Dar ni sehemu sahihi sana kielimu kwa mtu aliyekuja kusoma, lakini kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni sehemu hatarishi pia hasa Kwa wale ambao hawakua na malezi sahihi toka kwao. Mtoto anakuja kusoma anarudi na ukimwi. Utashangaa mtoto wa first year ana iPhone 15 pro max ambayo hata mzazi wake Hana uwezo wa kumiliki. So kaipataje, KATOA MZIGO kwa wadau.

Dar ni njiapanda ya ndoto za vijana wengi wanaotaka kwenda kuishi ughaibuni. Hapa nipo michongo yote na connection huanzia. Ukiwa hapa utajua Nini maana ya green card na unaipataje, utajua balozi zote zilipo na Fursa zao.

Dar ndio sehemu ambayo mtu anakaa anatunga kamradi tu kwa hovyo hovyo na kanaitika anapiga hela. Yamkini aliyeanzisha marathon hakujua kama Utakua mchongo Mkubwa wa watu kupiga hela either binafsi au kupitia mashirika...

HIYO NDIO DAR, ONGEZEA YA KWAKO..

KARIBUNI SANA DAR ES SALAAM ILA MUWE NA PASSPORT (kidding)
Ni mawazo yako tu.
 
MIMI::Upo wapi skuhzi met .... .

YEYE Dar es slam, wewe wapi met

MIMI,:nipo bado Kilimanjaro

YEYE:ujege mjini na wewe huku hela ndio zipo

MIMI:nitakuja(ga) tu..nitakuja ga nitakuja ga ..khokhokho
Baada ya week tatu

YEYE:met nina shida imenipata ghafla

MIMI:shida gani tena?

YEYE🙁Kwa kusikitika), yaani kuna mishe nlkuwa napiga basi kuna hasara imeingia kwenye kampuni afu ni kipindi natakiwa kulipa kodi , naomba nisaidie laki 2, baada ya week nairejesha plz.

MIMI:,oh (kwa majonzi),pole sana nkutumie kwa namna hiii?
YEYE:Ndio rafiki wangu wa dhati🤪🤪🤪

MIMI:umeiona eh?
YEYE:Ndio asante ubarikiwe

Two weeks later .....MIMI:mambo best ile issue

YEYE:Sorry asee (kwa majonzi)bibi mzaa babu wa babu alifariki nkatuma pesa nyumbani hapo

MIMI:Ni wapi huko jamani nkamzke,
YEYE🙁huku akidanganya kwa kung'ata meno) walishazika , ..

MIMI:ile hela vipi sasa nitegemee lini?

YEYE...(nipe week2)
week23 miezi inapita mitatu,4,5

MIMI:kimya

YEYE🙁baada ya miezi sita,) ujumbe mrefu sana,,, Hope mambow?uko poa mpendwa? Naomba unisamehe sana najua nlkukwaza muda wote huu nknk ile hela ntakutumia Dec..

MIMI;Kimya kimya kimya

YEYE:...Umeona huo muamala nmekutumia laki moja nyingne ntakutumia siku nyingine sunajua msimu wa sikuku huuumeingia..nikija Dec ntakutafuta

MIMI:Kimya kimya kimya.............(itaendelea)

wanadar muwege real asee ...
 
not only fly overs look even the members of parliament they dont want to stay in their regional the want to stay in dsm why..?
Waambie hao wabishi wahedi 😂😂😂... Dar ni Dar tu, ukiangalia kweli wabunge wao wa huko Mwakafyale sijui Mwamalili, mpaka Longido huko wote wanaishi Dar.... Wanakuja huko kipindi Cha kampeni tu watoe vipesa na viahidi warudi zao mjini kula maisha...😂😂. Nchi ngumu Sana hii
 
Aseee hii ni kweli.... Sema sio Dar tu. Maisha yapo hivyo...!!
 
Waambie hao wabishi wahedi 😂😂😂... Dar ni Dar tu, ukiangalia kweli wabunge wao wa huko Mwakafyale sijui Mwamalili, mpaka Longido huko wote wanaishi Dar.... Wanakuja huko kipindi Cha kampeni tu watoe vipesa na viahidi warudi zao mjini kula maisha...😂😂. Nchi ngumu Sana hii
😂😂💯 they know it but they act like they dont
 
Dar es salaam ni nzuri kwa mtu mwenye kazi nzuri yenye mshahara mnono au mtu mwenye biashara kubwa zinazojiendesha zenyewe ,mtu mwenye nyumba nzuri ya kukaa na usafiri binafsi. Njee ya hapo ni mji wenye mateso makubwa.
Mji gani hapa tz ambao ukiwa kinyume na hvyo ulivyoorodhesha utaishi kwa raha.?
 
Mji gani hapa tz ambao ukiwa kinyume na hvyo ulivyoorodhesha utaishi kwa raha.?
Nivigumu kukuelewesha ila ukivikosa hivyo vitu hapo juu ukiwa dar utateseka sana kuliko mtu ambae yuko mkoani. Au siku ukija kuishi huko dar utakuja kuona utofauti na huko mkoani
 
Back
Top Bottom