Kuishi Dar ni ndoto ya Kila Mtanzania Kijana

Dar ni Jiji la kwanza kwa maendeleo Tanzania na yamkini Afrika Mashariki.

Dar imejaa Fursa mbalimbali za kujikwamua Kiuchumi kwa kijana mtafutaji na mpambanaji hasa ambae ana lengo la kutoboa maishani. Lakini kijana huyu awe tayari kufanya kazi ya namna yoyote Mradi mkono uende kinywani.

Dar imejaa starehe na anasa za Kila namna ambazo asilimia kubwa sana zinawatoa kwenye reli vijana waliokuja kwa ajili ya kupambana, sababu damu inachemka hivyo starehe kwake inakua muhimu Sana kwa muda huo, changamoto vijana wengi wanashindwa kufikia malengo kwa kushindwa kubalance kati ya mapato na matumizi.

Dar ni sehemu hatari Sana kwa kijana ambae amekuja kiupambanaji lakini akawa mvivu wa mwili na akili akataka Kutumia short cut ili atoboe. Huyu ataangukia kwenye mikono ya ushoga, kubebeshwa madawa au kua jambazi/kibaka au utapeli. Maana ukubwa wa starehe uliopo utampeleka resi Apate pesa nyingi kwa haraka ili kumudu matumizi.

Dar ni sehemu sahihi sana kielimu kwa mtu aliyekuja kusoma, lakini kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni sehemu hatarishi pia hasa Kwa wale ambao hawakua na malezi sahihi toka kwao. Mtoto anakuja kusoma anarudi na ukimwi. Utashangaa mtoto wa first year ana iPhone 15 pro max ambayo hata mzazi wake Hana uwezo wa kumiliki. So kaipataje, KATOA MZIGO kwa wadau.

Dar ni njiapanda ya ndoto za vijana wengi wanaotaka kwenda kuishi ughaibuni. Hapa nipo michongo yote na connection huanzia. Ukiwa hapa utajua Nini maana ya green card na unaipataje, utajua balozi zote zilipo na Fursa zao.

Dar ndio sehemu ambayo mtu anakaa anatunga kamradi tu kwa hovyo hovyo na kanaitika anapiga hela. Yamkini aliyeanzisha marathon hakujua kama Utakua mchongo Mkubwa wa watu kupiga hela either binafsi au kupitia mashirika...

HIYO NDIO DAR, ONGEZEA YA KWAKO..

KARIBUNI SANA DAR ES SALAAM ILA MUWE NA PASSPORT (kidding)
Kwa mtu usiye na hela wala ramani, Dar ni kuzimu!
 
Mm nataka Mwanza au Morogoro
 
Dar ! sio mahali pa kuishi hata unipe Shell ya mafuta nyumba na vx v8 na Mke mzungu sikai .Jiji chafu hewa chafu Kariakoo huko mnakanyaga vinyesi usafiri tabu Maji tabu Kila kitu tabu unatembea unawaza wallet huku unafikiria vibaka kitaa unalala saa 5 usiku unaamka saa 10 usiku unatuambiaje Dar kuzuri
Njoo huku Rungwe Maji mtoni Baridi salama na Safi maziwa ltr 5 ni 3,000 gimbi 500 ndizi Bure
Kulala ni ww tu ukiamka saa 12 saa 1 upo ofisini
Huko kaa tu mwenyewe
Chakushangaza mbunge wenu anaishi dar
 
Back
Top Bottom