Au itakuwa hukumwelewa? But miujiza ipo sana
NI kweli miujiza ipo ila shaka yangu kubwa inatokana na mambo makuu mawili, kama umenisoma vizuri hapo juu. Ni kwamba huyu mtumishi baada ya kuwa amekaribishwa na kusimama kwenye madhabahu:
MOJA: Hakutoa hata ile sala fupi tu ya maombi, kuombea program iliypokuwa mbele yake
PILI: Kipindi chote alichokuwa amesimama madhabahuni, hakuwahi kusoma hata fungu moja fupi tu kutoka kwenye maandiko matakatifu.
Hoja yake kubwa ilikuwa ni kwamba apewe hela kwa ajili ya kwenda kufanya uinjilisti, ndiyo topic aliyoongelea mwanzo mpaka mwisho
Sasa haya yote ndiyo yanayonifanya niwe na mashaka makubwa sana kwamba mtumishi wa aina hii anaweza kweli akaambatana na muujiza wa kiwango cha juu kwa kiasi hicho tajwa, wakati hata kule kutoa sala fupi anapokuwa kwenye ibada kwaker ni shida, achilia mbali kusoma fungu fupi kutoka kwenye maandiko matakatifu. Tukio hili lilkitokea mwaka 2014 mwezi Septemba au Oktoba
Halafu kama wewe ni muumini kanisani, naktahadharisha uwe mwangalifu sana na mtumishi yeyote wa Mungu anayesimama madhabahuni halafu akawa anafanya mojawapo ya mambo haya matatu au yote kwa kwa pamoja
MOJA: Mtumishi kukaribishwa madhabahuni halafu akaanza kufundisha somo la maandiko matakatifu bila kuwa limetanguliwa na sala. Hata hivyo hii ina-apply tu kwa haya makanisa yetu ambayo huwa yanaendesha Ibada ambazo
usomaji wake wa maandiko hauko guided sana.
MBILI: Mtumishi wa Mungu kusimama madhabahuni akifundisha maandiko matakatifu, bila yeye kuwa anasoma maandiko hayo, badala yake anakuwa amechagua mtu aqu watu miongoni mwa waumini kuwa wanasoma mafungu ya maandiko hayo badala yake yeye ila yeye anakuwa hasomi kabisa. Kwenye ulimwengu wa roho, kuna tofauti kati ya maandiko matakatifu kusomwa kutokea madhabahuni na kutokea sehemu nyingine yoyote ile ndani ya nyumba ya Ibada. Ndiyo maana watumishi huwa wanapanda juu madhabahuni wakiwa na Bibila. Neno linalosomwa na mtumishi kutokea mbele ya waumini au madhabahuni lina nguvu kuliko lile linalosomwa na muumini mwingine yoyote aliyekaa sehemu yoyote ile katikati ya waumini wengine, ndani ya nyuma ya Ibada. Kwa hiyo ukimuona mtumishi ambaye hasomi neno kutokea mbele ya waumini au madhabahuni, uwezekano mkubwa ni kuwa kuna kitu hakiko sawa na kwamba anaweza kuwa anafanya uchakachuaji wa hali ya juu sana.
TATU: Mtumishi wa Mungu kusimama mbele ya madhabahu na kuanza kufundisha maandiko matakaitu kutokea mdomoni kwake. Yaani anakuwa hasomi maandiko na sana sana ikibidi llabda anafaribu kutaja taja mafungu tu. Huyu anayeangukia kwenye kundi hili la mwisho ndiyo hatari zaidi na ni wa kuogopa kama ukoma!