Kujaribu kuwazodoa kina Mandela, Nyerere, Lissu, nk ni kujidhalilisha!

Kujaribu kuwazodoa kina Mandela, Nyerere, Lissu, nk ni kujidhalilisha!

Muogope sana tundu LISU kwenye mikakati na msigwa alisafiri kwenda kumuaga LISU singida kwenye mikutano ileeee , ikabidi msigwa asubiri LISU aende kwa Mama wawili ubelgiji akijifanya kitibiwa

CHADEMA ,ili ikae sawa lazima mbowe awe pembeni , kibodi zikamatwe na akina heche

Tatizo tunataka u star. Ya kwamba nini tunataka au nini hatumtaki yaweza kuwa hatujui:

Kusuasua kwa harakati za ukombozi nchini ni matokeo ya uongozi dhaifu

Ninakazia:

CCM haitatolewa madarakani kijinga wala na wajinga.
 
Wewe unayo?

Dk. Remmy na beetle yake archaic aliandika kwa nyuma:

"Baba yako analo?"

Kwa hakika ujumbe huo uliwakata maini sana vizaba zabina waliokuwa wazodoaji kabla ya kuuona.
Sihitaji kuwa nayo, naongea ukweli tu kwamba Lissu hafikii viwango vya maadili na heshima vya Nyerere na Mandela.

Naikumbuka hiyo volkswagen, hayati Remmy alikuwa anafuga mbwa, mara nyingi akija kuwaleta pale veterinary mtaa wa Shaban Robert jirani na nyumba yetu miaka hiyo.
 
Sihitaji kuwa nayo,

Hii inaitwa sizitaki mbichi hizi.

naongea ukweli tu kwamba Lissu hafikii viwango vya maadili na heshima vya Nyerere na Mandela.

Kwa hakika hakuna Lissu alipolinganishwa na Mandela a nobel laureate. Haijulikani hili unaliokota wapi, kulileta kivyako vyako hapa ndugu.

Naikumbuka hiyo volkswagen, hayati Remmy alikuwa anafuga mbwa, mara nyingi akija kuwaleta pale veterinary mtaa wa Shaban Robert jirani na nyumba yetu miaka hiyo.

Ni vyema kama umeikumbuka hiyo beetle. Nami nikuulize kwa mara nyingine:

Haiba ya Lissu unayo?

Kama kuwashwa washwa ni wivu, basi Sitta hakuwa na neno jema sana kwake.

Habari ndiyo hiyo ndugu.
 
Hii inaitwa sizitaki mbichi hizi.

Kwa hakika hakuna Lissu alipolinganishwa na Mandela a nobel laureate. Haijulikani hili unaliokota wapi, kulileta kivyako vyako hapa ndugu.

Ni vyema kama umeikumbuka hiyo beetle. Nami nikuulize kwa mara nyingine:

Haiba ya Lissu unayo?

Kama kuwashwa washwa ni wivu, basi Sitta hakuwa na neno jema sana kwake.

Habari ndiyo hiyo ndugu.
Mandela, Nyerere hawakai kundi moja na Lissu. Nyerere alijenga viwanda zaidi ya 150 nchi nzima huwezi kumlinganisha na huyo mwendawazimu TAL.

Mandela aliheshimiwa kila mahali alipokwenda huwezi kumlinganisha na huyo mwanasheria mvaa miwani.
 
Ila mzodoaji tokea kwa mfuga mbwa cha kwake cha kuonyesha hamna.

Tofauti yako na wanaoita jalalani hali wao ni boda boda kumbe itakuwa iko wapi?
 
Lissu ni namba nyingine. Lissu ameanza kupigania wananchi hata kabla hajaingia kwenye siasa. Lissu hanunuliki. Lissu amekataa fedha ya Abdul, akamfukuza nayo. Acha upumbavu!

Hii ni habari mbaya mno kwa wote wamchukiao ndani na nje ya chama.

imhotep au nasema uongo ndugu yangu?
 
Lissu ni namba nyingine. Lissu ameanza kupigania wananchi hata kabla hajaingia kwenye siasa. Lissu hanunuliki. Lissu amekataa fedha ya Abdul, akamfukuza nayo. Acha upumbavu!
Upumbavu ni haya maneno eti aliikata pesa ya Abdul, stupid story.

Hana hadhi ya kuwekwa jukwaa moja na Mandela/Nyerere.
 
Ila mzodoaji tokea kwa mfuga mbwa cha kwake cha kuonyesha hamna.

Tofauti yako na wanaoita jalalani hali wao ni boda boda kumbe itakuwa iko wapi?
Huwezi kumuweka sehemu moja Mandela na Lissu. Mandela hiyo story inaonyesha unyenyekevu wa asili kitu ambacho Lissu hana, kajawa mbwembwe na maneno ya dhihaka ya wanasheria wetu.
 
Lissu ni mnyera tu hawezi kuweka katika nafasi moja na kina Mandela, Nyerere.

..Mwalimu Nyerere hakuteswa na Waingereza kama ambavyo Tundu Lissu, na wapinzani wengine wameteswa na serikali za Ccm, na vyombo vyake.

..Tunamheshimu Mwalimu Nyerere, lakini ukweli lazima usemwe kwamba Wakoloni ambao aliwapinga, walikuwa na utu, kuliko Ccm ambayo ametuachia, na tunapambana nayo.
 
Huwezi kumuweka sehemu moja Mandela na Lissu. Mandela hiyo story inaonyesha unyenyekevu wa asili kitu ambacho Lissu hana, kajawa mbwembwe na maneno ya dhihaka ya wanasheria wetu.

..Mandela hakuwa mnyenyekevu.

..alianzisha mapambano ya silaha na umwagaji damu dhidi ya Makaburu.

..vijana wa Ccm mnasoma wapi historia?

..Ccm si mnadai ni chama cha ukombozi kusini mwa Afrika, sasa kwanini hamjui historia ya ukombozi?
 
Ni high level ya ujinga kumweka lisu kwenye level moja na akina Nyerere, Mandela, Nkrumah, nk. Watanzania tuacheni ujinga.
 
Yamekuwa yakisikika maneno:

"JF ni Raha sana."

Kwa hakika ni kwa maana yake kamili.

Hayo ni pamoja na kuwaona baadhi ya wajumbe wakijitutumua kujaribu kuwazodoa watu ambao dunia Kwa ujumla wake imewavulia kofia.

Wandugu kwa level za kwetu kujimwambafai dhidi ya kina Lissu au Nyerere ni wenda wazimu.

Kwa level za dunia kujimwambafai dhidi ya watunukiwa nobeli (nobel laureates) yaani aina ya kina Mandela, Obama, Tutu na wa namna hiyo kwa nini isiwe zaidi burudani kwa wenye kujua maana?

Wanasema waswahili:

"Aibu mbona naona miye?"

Huyu ndiye Mandela, kwa ufupi mno katika hulka yake kama binadamu:

"After I became president, I asked my escort to go to a restaurant for lunch. We sat down and each of us asked what we wanted.

On the front table, there was a man waiting to be served. When he was served, I said to one of my soldiers: go and ask that gentleman to join us. The soldier went and conveyed my invitation to him. The man got up, took his plate and sat down right next to me.

While he ate his hands trembled constantly and he did not lift his head from his food. When we finished, he said goodbye without looking at me, I shook his hand and he left.

The soldier told me:

Madiba that man must have been very ill, seeing as his hands didn't stop shaking while he ate.-

Absolutely no! the reason for his trembling is another.

Then I told him:

That man was the warden of the prison where I stayed. After he tortured me, I screamed and cried asking for some water and he came humiliated me, laughed at me and instead of giving me water, he urinated in my head.

He is not sick, he was afraid that I, now president of South Africa, would send him to prison and do to him what he did to me. But I'm not like that, this conduct is not part of my character, nor of my ethics.

′′Minds that seek revenge destroy states, while those that seek reconciliation build nations. Walking out the door to my freedom, I knew that if I didn't leave all the anger, hatred and resentment behind me, I would still be a prisoner."

- Nelson Mandela.
Usichanganye madesa aisee

Wale wazee wana heshima yao… sio huyu wa mitusitusi
 
Usichanganye madesa aisee

Wale wazee wana heshima yao… sio huyu wa mitusitusi

..Nyerere alibahatika kuwapinga Waingereza ambao walikuwa na utu, au hawakuwa na maslahi makubwa na Tanganyika.

..Ccm ambayo wapinzani wanapambana nayo ni wakatili na wana hila kuliko wakoloni wa Kiingereza.

..Na tunaweza kufanya ulinganifu wa mambo mabaya yaliyowafika wapinzani wa Ccm, dhidi ya mambo waliyopitia Tanu wakati wakidai uhuru.

..Mifano, michache ni jinsi Ccm walivyowafunga jela karibu nusu ya kamati kuu ya Chadema. Kesi za kubumba za uhaini dhidi ya viongozi wa Cuf. Kesi ya kurusha ya ugaidi dhidi ya M Mbowe.

..Kwa upande mwingine, Je, Mwalimu Nyerere aliwahi kufungwa, au kulala mahabusu? Mwalimu Nyerere aliwahi kupigwa au kudhalilishwa na askari wa Muingereza?

..Tunamheshimu Baba wa Taifa kwa kuongoza mapambano ya uhuru, lakini tusijaribu kupuuza maovu yanayofanywa na Ccm aliyotuachia.
 
Habari ni nzuri, lakini najiuliza, Lissu anaingiaje kwa hao VIGOGO? 😳

..Ni kwasababu hajashika madaraka ambayo watajwa wameyashika.

..Lakini kwenye kupambania HAKI, Lissu amepitia mikasa ambayo baadhi ya watajwa hawakuipitia.

..Kwa mfano, ni ukweli kwamba Lissu hakuwahi kukaa gerezani. Lakini tujiulize shambulizi dhidi yake, tunaweza kusema lina afadhali kuliko kifungo?
 
Jambo moja tu, nadhani umelisahau na limefanya mada yako nzima itiwe dosari.

Huyo Advocate Tundu Antipas Lissu ndiyo mzodoaji mkubwa wa Mzee Nyerere.

Wengine wote hufanya hivyo hapa JF, ila Lissu alifanya hivyo mbele ya ulimwengu mzima na mpaka sasa kumbukumbu ziko kwenye mtandao wa bunge la Tanzania. Labda, tukumbushane tu alichokisema ndugu Tundu Lissu: "Waliozoea vya kunyonga, hawawezi vya kuchinja" akimaanisha kwamba Mzee Nyerere alizoea kuvunja sheria, hivyo hata CCM hawawezi leo hii kuanza kuheshimu katiba.

Kiufupi, Mzee Nyerere anapendwa sana, hata mimi binafsi nampenda. Ila huu ujinga wa kutaka kulazimisha asisemwe hata pale alipotusababishia tuvae viraka na kukosa hata sabuni za kuogea ni jambo la hovyo. Wengi walioishi miaka ya 80's watakwambia ukweli wa hali ilivyokuwa.

Binafsi huwa nashukuru UJAMAA uliisha, na Mzee Dr Salim Ahmed Salim alitusaidia mno. Ukiisoma historia ya Tanzania kwenye vitabu pamoja na UJAMAA unaweza kuhisi kila kitu Mzee Nyerere anaonewa, ila wale walioiishi walau kuanzia 1975-1985 watakwambia ukweli.

Kwamba tuogope kuwasema kisa ni International Statemen, au Nobel Laureates nadhani linanipa mno ukakasi. Kina Winston Churchill, Abraham Lincoln, Julius Ceaser, Joseph stiglitz, Henry Kissinger, hadu Mother Theresa wote tunawasema na kuwazodoa mpaka leo hii. Mzee Nyerere, Mandela na Tutu ni kina nani hadi wasizodolewe ???​

..lakini usisahau jinsi Tundu Lissu anavyomkubali na kumsifia Mwalimu Nyerere ktk masuala ya uadilifu, kutojihusisha na rushwa, na kutokudokoa mali za umma.
 
..Nyerere alibahatika kuwapinga Waingereza ambao walikuwa na utu, au hawakuwa na maslahi makubwa na Tanganyika.

..Ccm ambayo wapinzani wanapambana nayo ni wakatili na wana hila kuliko wakoloni wa Kiingereza.

..Na tunaweza kufanya ulinganifu wa mambo mabaya yaliyowafika wapinzani wa Ccm, dhidi ya mambo waliyopitia Tanu wakati wakidai uhuru.

..Mifano, michache ni jinsi Ccm walivyowafunga jela karibu nusu ya kamati kuu ya Chadema. Kesi za kubumba za uhaini dhidi ya viongozi wa Cuf. Kesi ya kurusha ya ugaidi dhidi ya M Mbowe.

..Kwa upande mwingine, Je, Mwalimu Nyerere aliwahi kufungwa, au kulala mahabusu? Mwalimu Nyerere aliwahi kupigwa au kudhalilishwa na askari wa Muingereza?

..Tunamheshimu Baba wa Taifa kwa kuongoza mapambano ya uhuru, lakini tusijaribu kupuuza maovu yanayofanywa na Ccm aliyotuachia.
Mandela na Nyerere were wise

Not huyu wa mitusi
 
Back
Top Bottom