Kujenga nyumba kubwa hasara zake ni kubwa kuliko faida

moja ya malengo yangu ni kumiliki nyumba kwenye kiwanja cha hekari zaidi ya 15 yenye mabafu ya kisasa ya kuogea 8 achilia mbali vyumba vya kulala, ukumbi wa sinema, sebule 3 na mengineyo jumba liwe zaidi ya bangaroooo.... yasipofanikiwa sasa nitajenga nyumba ya kisasa ya vyumba 6 yenye kila kitu kinachoitwa cha kisasa kwenye uwanja usiopungua heka 4 to 5
 
Halafu analala nani[emoji852][emoji849]?
 
N
Nyumba kama hii ni matumizi mabaya ya fedha,bora ujenge uweke eneo la jimu,bwawa la kuogelea na vitu vingine kuliko kujenga nyumba kama guest house
 
Umeongea vema na ni kweli nina limited pocket.....lakin having limited pocket doesn't necessarily means sina big dreams ama situation yangu ni permanent......Lakini i want to assure you kwamba hata nikiwa na unlimited pocket "big castle" will never be my dream kwasababu sijifikiri mimi mwenyewe nawaza na wengine kwenye uzao wangu.....siwezi invest 2 billion kwenye kitu kitakashindwa kuzalisha in 50 years to come.....Ndo maana nimesema watu wengi kama wewe tunaotokea kwenye umaskini mnakuwa na poverty mentality kwamba kwa vile baba hakuweza kujenga nyumba ya ghorofa ni lazima nijenge kwa ajili ya ufahari tu nakuwa onyesha watu sisi tumetokea familia ya Mushi (kwa mfano) wakati mjomba wako wakaribu yuko kiraracha kwenye nyumba ya udongo......think beyond not just for your self........Angalia kwa mfano ghorofa la billionea Msuya taking into account current status ya watoto......wakiachiwa unafikiri wanaweza kuli maintain kuwa kwenye standard kam baba yao alivyoliacha? lakini angalia at the same time investment ya baba yao ya Hotel ndo inayo wasomesha nakuwapatia mahitaji......Mimi i will go for a small house regardless ya kiasi gani ninacho the rest i will invest......
 
Dunia sio Mji udumuo. So tafuta sehemu ya kujibanza make Mungu keshatuandalia makao, ili alipo nasi tuwepo.
 
Nimetafakari na nimerudi. Jumba kubwa sometimes ni zuri kusudi kila mtu na kitanda chake, siku ya kugawa dozi ndo mnashare, siku nyingine kila mtu na hamsini zake.
 

Elewa mada, hapa hatuongelei kuishi vizuri, bali kujenga nyumba kubwa ya kuishi familia.
 
Hakunaga umoja kwenye familia za ngozi nyeusi.na hii husababishwa na wazazi kupendelea mmoja
Ni kweli Ila wengine hujenga ziwe Kama generational houses ndio maana mfano kwa matajiri wa huko kwa wenzetu ni kawaida kuona nyumba inamilikiwa na familia kwa miaka 50/100.
Ila hili kwetu ni gumu
 
Mimi nikashaona mtu kajenga nyumba kubwa ya kuishi familia huwa namuona ni ng'ombe tu.
 
Ukijenga nyumba kubwa sana ukifa watakaobaki wataliuza maana hawataweza kihudumia.
 
Hili ni tatizo sana
 

Hili halina ubishi kwa nchi masikini
Jamaa juzi ananiambia kajenga nyumba ya gorofa tatu kwa ushawishi wa mke wake
Jamaa yuko nje ya nchi akirudi home anakuta nyumba imejaa na wengine wanamuita ANKO hata hawajui
Inabidi ashukie hotel tu
Sasa huu si utumwa kwenye nyumba yako mwenyewe
Waafrika shida sana
 
Mbinguni kuna makao mazuri sana, ya nini kuhangaikia mapito ya hapa duniani huku tukijua tunapita tu.... bwana Yesu yuko bize kutuandalia makao mazuri kwa kila mmoja wetu.

Farijianeni kwa maneno hayo, mengine yote ni ubatili mtupu.... na hata usiku utapokwisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…