Dumbuya
JF-Expert Member
- Jan 23, 2014
- 596
- 878
Hakika nakuambia ukiwapa waTz 10 hata wenye hiyo elimu ya fedha Mil.60 baada ya miaka 4 ukija kuwathaminisha ni 1 au wawili ndio watakuwa na angalau 10Mil kwenye akaunti zao.Watanzania tunahitaji kubadili mentality na kuondoa uoga kuhusu kufanya biashara. Mtu anafanya kazi posta anaanza ujenzi Madale, akimaliza nyumba anahamia kwake, anaanza kuendesha gari kilometer 60 kwenda kazini na kurudi, wastani wa mafuta ya elfu 25 Kwa siku na masaa manne njiani kwenda na kurudi. Wakati huo ana familia, mke na watoto wawili wanaosoma English medium. Unakuta nyumba na gari vimemcost kati ya milioni 40 hadi 60, kama angepata ushauri na kuwa na elimu nzuri kuhusu uwekezaji na financial management ya kutosha. Hiyo pesa ndani ya miaka miwili anakuwa anaongea story tofauti. Lakini unakuta vijana wengi wana nyumba nzuri na usafiri, ila kiuhalisia wamekwama kiuchumi kila mwisho wa mwezi unamkuta na madeni. Sababu ya haya yote ni tunaishi kwa kuigana na kutafuta status kwenye jamii. Kwa watanzania walio wengi ni bora aishi kwenye nyumba yake yenye thamani ya milioni 50 hata kama hana kazi, ila kwangu mimi ni bora kuishi nyumba ya kupanga ila nina akaunti iliyonona na nina biashara inayozungusha pesa na nina backup ya pesa kwenye akaunti kulinda/au kuanzisha biashara nyingine wakati wowote. Mleta mada upo sahihi sana.
Hizi biashara tuheshimu pia, siyo rahisi kihivyo..kila siku watu wanateketeza mitaji.Mmeshasahau ya Kkoo na TRA ??
Kikubwa ni kuchukua maamuzi yenye mantiki na tija kwa muda huo.Mfano wapo amabo kujenga ni uamuzi sahihi zaidi kwa wakati huo na wapo ambao kununua gari na wapo ambao ni kuwekeza.