Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

Ukijenga nyumba kwa lengo ya kua dhamana au security bank hapo ndo umeferi kabisa bora unge tunza zile pesa ndo zikusaindie kupanua biashara yako Bank za Tz ni wezi ma lengo yao sio kukuinua but kukufilisi nyumba ya 200m itadhamini mkopo wa 30m au 50m ndo watakupa mkopo hiyo njia imefilisi wafanya biashara wengi.......kwahiyo ni vizuri kutunza cash kuliko kuiweka kwenye nyumba liquidity ni muhimu kuliko solid assets kwasbb na benki zinahitaji faida lazima wakufilisi.
Sio kweli sidhani kama uko sahihi dhamana ya milioni 200 upewe 50 hakuna kitu kama hicho
 
Ukijenga nyumba kwa lengo ya kua dhamana au security bank hapo ndo umeferi kabisa bora unge tunza zile pesa ndo zikusaindie kupanua biashara yako Bank za Tz ni wezi ma lengo yao sio kukuinua but kukufilisi nyumba ya 200m itadhamini mkopo wa 30m au 50m ndo watakupa mkopo hiyo njia imefilisi wafanya biashara wengi.......kwahiyo ni vizuri kutunza cash kuliko kuiweka kwenye nyumba liquidity ni muhimu kuliko solid assets kwasbb na benki zinahitaji faida lazima wakufilisi.
Sina hakika kama unafanya biashara usinielewe vibaya lakini kwa nia njema tu mfano biashara yako yahitaji mtaji wa kuzungusha (working capital) tuseme milioni 100 uta-save kwa muda gani uje uziingize kwenye biashara yako? Kingine nani alikwambia nia na madhumuni ya bank ni kukufilisi mbona biashara nyingi zimeinuka na kufanikiwa kwa kukopa labda kama hujawahi kufanya biashara na hujawahi kwenda taasisi za fedha.
 
Ukikopa mil 100, ukaiweka UTT , baada ya miaka 5 unakua na zaidi ya mil 300. lakini ukijenga nyumba ya mil 100 baada ya miaka 3 nyumba hiyo itakua na dhamani ha mil 50
Una uhakika mkuu?? Huko UTT ROI yao ni 1.2 to 1% ya mtaji wako, means kwa mwaka utapata mil 12, kwa miaka 5 utapata mil 60, hyo 300m umeipata kwa hesabu gani??
 
Kujenga nao Ni muhimu Sana mwak 2015 nilkuwa na access ya kujenga nikaona wacha niwekeze kwenye biashra aloo acha kbsa biashra bongo hazitabirikii kwa ujumlaaa
Uko sahihi 'uncertainties' zipo za kutosha kwenye biashara zetu za kibongo haitabiriki leo hiki kesho kile kuusoma upepo muhimu kwenye biashara bongo wengi wametoka nje ya reli.
 
Kujenga nyumba, kununua gari hayo yote ni mahitaji muhimu kwa mwanadamu wala sio utajiri.
Kuoa ni maamuzi pia ila kujenga extra yaani kuzidi kipato chako huo ni uzuzu, tumieni akili basi unafanya kazi posta unajenga madale.....

Jenga madale pangishia afu ile kodi lipia hapo hapo mjini, imeisha hiyo....
 
Hatima ya hivi vyote ni nini iwe kujenga au mtaji wa biashara?

Unapofanya chochote kile ndani ya hivyo kuna faida na hasara sasa sijui wewe unadhani maisha yataishi kwako tu na siyo kwa wanaondeleza kikazi chako.

Fanya mambo kwa upeo mkubwa hasa kuacha kizazi chako katika hali ya juu kimaisha,maisha siyo fedha bali mipango na kumbuka vyoote utaviacha duniani na je kizazi chako ni bora ukiachie biashara isiyo na kinga au mahali pa kuishi pa kudumu?
 
Naamini sisi watumishi ndio tunaongoza kutishana kuhusu biashara tunapeana vitisho vingi kweli sijui TRA,kila rais akiingia madarakani ana vipengele vyake,c mnawaona wafanya biashara wa k/koo wanavyohangaika.
Mwisho wa siku tunastaafu pesa inaisha ndio tunapata akili ya kufanya biashara, biashara ktk umri mkubwa baadae biashara hiyo hiyo inakupiga kofi mpaka kaburini
 
Shida ipo kwenye Mashirika yetu NHC, Watumishi Housing, TBA kama wangefanya kazi yao Watanzania wangekuwa mabilionea. Tunafurahi kwaa Dodoma maelfu ya majumba wanayojenga mtu huna haja ya kupoteza mamilioni kujenga wakati nyumba za Shirika zipo.
 
Mkuu haya kuyaongea kama motivational speaker ni rahisi ila kwenye vitendo kibongo bongo ni habari nyingine. Ila una mawazo mazuri
Shukrani ndugu.
Ila haya nimeyaandika kiuharisia kabisa na hali hairisi za maisha yetu ya Ki Tanzania.

Kuna baadhi ya vitu tukiviacha tutafika mbali.
Mfano: Kupoteza muda kwenye mambo ya kijifurahisha wenyewe ilihari hayana maana yeyote.

Angalia baadhi ya mafundi ujenzi na wengine wenye fani mbali mbali wanafanya kazi kwa kujituma laki ikifika jioni pesa anaipeleka kwa mchepuko au baa, kesho anaamka tena kutafuta kisha anaipoteza tena. Mwisho wa siku wa huyu mtu anaishia kwenye umaskini tu.

Kiukweli sisi wa Africa tunapoteza muda mwingi na utajiri kwenye mambo yasio na maana.

Angalia wenzetu nchi zilio endelea mfano China, hutokuta wadada wamejiongeza mashepu, wameridhika na maisha yao, na wanafanya kazi kwa kujituma.
Njoo sasa huku kwetu Africa kila kukicha tunawaza kuongeza mashepu, wanaume nao wanaongoza kutamani kuongeza miili yao na nguvu pia. Kiufupi fahamu zetu zimelala hapo. Hata tukipata pesa tumejitahidi sana tunakimbilia kujenga na kununua ki IST au Vitz, hapo tunaona tumesha fanikiwa kumbe tunahitaji kuwekeza kwa muda mrefu ili watu tujikwamue na umaskini.

Ndiyo maana nchi zetu za ki Africa tunaishia kuwa wachawi/roho mbaya tu, kwa maana hakuna tunachokiwaza zaidi ya mambo ya ajabu tu, hats ikitokea mmoja kafanikiwa lazima ashusshwe tu, wakati inabidi tumtiye moyo na kumuuliza kafikaje ili tujifunze lakini wapi.

Wadada/Wakaka wa Hong Kong wanaolewa/kuoa wakiwa na umri mkubwa, si kwamba hawana mihemko ila fahamu zao mda mwingi wanawaza maendeleo. Ndiyo maana zama hizi midoli ya uume au uke wa bandia zipo nyingi kwasababu wameweka ubusy mwingi kwenye mambo ya maana, miemko ikiinuka tu wanajimaliza wenyewe, ni kama kitu kizuri ila ni kibaya sana kiafya, ila wanatamani kuwa matajiri. Africa kwa hapa tumeshinda tunaoa mapema na kuishinda miemko yetu, sasa jambo la kufanya ni.

Kubadilisha fahamu zetu, tujikite haswa kwenye uwekezaji, kujifunza mbinu mbali mbali za kujikombowa kutoka katika maisha tuliyo nayo, nakuhakikisha kila kata ikiwa na vijana hata 50 wanaojitambua ndani ya mwaka 1 kuna vijana 100 wataongezeka, mwisho wa siku Africa yetu na Tanzania tutakuwa mbali sana.

Usikimbilie kujenga na kununua magari bali jifunze kuwekeza kwanza. Fanya uwekezaji kwenye mambo ya msingi ambayo utayamudu, baada ya hapo jenga na nunua vitu vya thamani uvipendavyo hapa utakuwa umesha wapa vijana wenzio motisha na wao pia watatamani kuwa kama wewe. Vinginevyo tutakuwa na vijana wa hovyo ambao wanatamani majumba mazuri na magari, ilihari hawajuwa kanuni ya kuvipata, tutakacho zidi kukizalisha ni mambo ya ajabu kwa vijana wetu.
 
Kwa maoni yangu, kumiliki nyumba na gari ya kutembelea ni kati ya mahitaji ya msingi (basic needs). Ukishakuwa na hivi vitu unakuwa na utulivu wa akili wa kufanya mambo ya maana ikiwemo uwekezaji.

Usifananishe na Ulaya. Huko, usafiri wa umma ni wa uhakika. Kila baada ya dakika kadhaa kuna chombo cha usafiri, mfano treni (tram) inapita, hivyo usafiri wa uhakika kwa muda muafaka unapatikana.

Sasa nenda pale Kkoo, Posta au Makumbusho saa 12 jioni, utasimama kituoni zaidi ya saa 1 au 2 unasubiri daladala, tena ya kupanda kwa kupambana, halafu kwa kuwa hizo daladala zinafuata ruti za kupangiwa bila kujali kama kuna foleni kali, unaweza kuchukua masaa mengine kadhaa hadi ufike. Ndiyo sababu kama uwezo unaruhusu unanunua gari Ili kupata ufanisi.

Kumiliki nyumba kunakupa security, hasa kama unaishi na wategemezi.
 
Watanzania tunahitaji kubadili mentality na kuondoa uoga kuhusu kufanya biashara. Mtu anafanya kazi posta anaanza ujenzi Madale, akimaliza nyumba anahamia kwake, anaanza kuendesha gari kilometer 60 kwenda kazini na kurudi, wastani wa mafuta ya elfu 25 Kwa siku na masaa manne njiani kwenda na kurudi. Wakati huo ana familia, mke na watoto wawili wanaosoma English medium. Unakuta nyumba na gari vimemcost kati ya milioni 40 hadi 60, kama angepata ushauri na kuwa na elimu nzuri kuhusu uwekezaji na financial management ya kutosha. Hiyo pesa ndani ya miaka miwili anakuwa anaongea story tofauti. Lakini unakuta vijana wengi wana nyumba nzuri na usafiri, ila kiuhalisia wamekwama kiuchumi kila mwisho wa mwezi unamkuta na madeni. Sababu ya haya yote ni tunaishi kwa kuigana na kutafuta status kwenye jamii. Kwa watanzania walio wengi ni bora aishi kwenye nyumba yake yenye thamani ya milioni 50 hata kama hana kazi, ila kwangu mimi ni bora kuishi nyumba ya kupanga ila nina akaunti iliyonona na nina biashara inayozungusha pesa na nina backup ya pesa kwenye akaunti kulinda/au kuanzisha biashara nyingine wakati wowote. Mleta mada upo sahihi sana.
Watu wanafukia sana hela hii nchi
 
Habari,

"Tafuta kiwanja, Jenga, Oa/Olewa, nunua mkoko", njia hii na mawazo haya yamekuwa kwa vijana wengi wanaoanza maisha, hususani waliobarikiwa kupata ajira au biashara zao binafsi ambazo zinawapa kipato flani cha kuendesha maisha yao. Kwa uzoefu wangu hii imekuwa kati ya sababu moja kubwa zinazosababisha watu kuwa maskini na kushindwa kufikia uhuru wa kifedha.

Lakini tujiulize swali la msingi, kwanini watu wengi wameamua kuchagua njia hii ya maisha. Nimefanikiwa kuwahoji watu wengi kidogo kuhusu hili na majibu niliyoyapata mengi yalikuwa kama ifuatavyo:

  • Gharama ya kupanga nyumba ziko juu sana, ni bora kujenga ya kwako.
  • Nyumba ni asset.
  • Usafiri ni shida sana eneo niliko jenga ni bora kuvuta gari yangu.
  • Mama/baba mwenye nyumba ana gubu sana.
  • Nikiwa na kwangu nakuwa na uhuru mkubwa sana.
  • Siku nikifukuzwa kazi au biashara ikiyumba nibaki na pakulala na familia yangu.

Sababu hapo juu nyingi ni za maana kabisa ila tatizo ni kwamba njia zilizotumika kutatua hizo changamoto zinaongeza changamoto zaidi, kivipi?. Ngoja tujadili mambo machache kuhusiana na maisha ya watu wengi hususani mijini (e.g. Dar):

- Wengi wananunua viwanja maeneo ya mbali kutoka mahali wanapofanyia shughuli zao zinazowapa kipato.
- Baadhi ya hayo maeneo yana changamoto za miundombinu ya maji, umeme, barabara na hata kiusalama.
  • Wengi wanajenga kwa kuunga unga sana, unaweza jenga nyumba hata miaka sita au zaidi. Kuna msemo wanasema "nyumba haiishi".
  • Nyumba nyingi wanazojenga watu kukaa zinakuwa ni kubwa na za kifahari bila kukumbuka lengo la mwanzo lilikuwa ni makazi tu na sio jengo la maonesho (Hapo utajibiwa kuwa tunajenga mara moja ya kuzeekea)

Kuzingatia hizo hoja hapo juu, yafuatayo yanakuwa ni matokeo ya gharama za maisha baada ya huyu mtu kuhamia kwake:

  • Gharama za usafiri au mafuta zinakuwa juu ukilinganisha na awali.
  • Mazingira yanakuwa sio rafiki kwa familia kuishi, maana nyumba nyingi zinakuwa bado hazijaisha (Wengine wanasema unakuwa unaishi site).
  • Kama una gari, gharama za matengenezo zinakuwa juu kwa sababu ya pengine barabara kuwa mbaya, lakini kwa kuwa unasafiri umbali mrefu kila siku, basi hata service ya gari utafanya mara nyingi zaidi.
  • Pia kama una gari utalazimika kuendesha gari umbali mrefu kila siku, hii si nzuri kwako kiafya.
  • Gharama za umeme na maji pia zinaweza kuongezeka kwa kuwa nyumba ni kubwa sasa na pengine maji hayajafika.
  • Maeneo mengine hata watu hawajahamia wengi hivyo hata usalama unakuwa hatarini.
  • Mara nyingi unaweza ukajikuta mbali na huduma bora za kijamii ikiwemo hospitali, shule, n.k.

***NOTE: Gharama zinaweza kuongezeka ukilinganisha na mwanzo.

Kwanini kuna hofu ya kuwekeza hizo pesa?

Tujiulize swali hili la msingi. Ni kweli baadhi ya watu wanatamani sana kuffanya biashara, lakini wengi wanasema, BIASHARA HAZITABIRIKI. Ni kweli kabisa, lakini ukweli ni kwamba hilo sio tatizo la watu kutokuwekeza.
SHIDA KUBWA NI WATU KUTOKUWA NA ELIMU YA FEDHA. Hili ni jambo la muhimu sana kwa vijana kupata elimu. kwanza kabisa sio kweli kwamba ukitaka kuwekeza ni lazima ukafanye biashara fulani kama kuuza nguo, vinywaji au duka la mangi. Unaweza ukafanya uwekezaji kwa njia nyingi sana ambazo hazitahitaji your active time kuweza kusimamia ila mwisho wa siku ukaja kuwa na uchumi mkubwa kabisa. Uwekezaji huu ni kama mifano ifuatayo:

  • Kununua viwanja na mashamba (Kumba muda unavyokwenda ardhi inapanda thamani lakini nyumba inashuka thamani)
  • Kununua hisa za makampuni
  • Tressury Bonds and Bills
  • Mifuko ya uwekezaji ya pamoja (e.g. UTTAMIS)
  • Fixed deposits accounts
  • Kuwekeza kwenye elimu (Hii sio lazima zile za darasani, inaweza kuwa hata kujiendeleza katika fani flani)
  • N.k.

La muhimu ni kupata elimu sahihi ya mambo ya fedha ili ujue jinsi ya kufanya maamuzi ni vipi utumie pesa yako.


Ngoja nitoe mfano halisi mmoja ulio hai kabisa kwa lengo la kupata uhalisia wa ninacho kisema:

Mwaka 2013 niliajiriwa mahali na tulikuwa kama waajiriwa sita wapya katika hiyo kampuni, mwenzetu mmoja alikuwa na uelewa mkubwa sana wa mambo ya fedha, na mara nyingi alikuwa anatushauri kuhusu haya mambo lakini tulikuwa tunamuona kama kachanganyikiwa: Mimi na wenzangu wengine wa tano tulikwenda mahali tukanunua viwanja na kuanza kujenga kwa kasi sana na badae tukachuku na mikopo kuongeza kasi hiyo. Kwa haraka haraka kwa wastani tuliweza kutenga kama milioni moja kwa mwezi kila mmoja wetu kwa ajiri ya miradi ya ujenzi. Mungu si athumani baada ya miaka mitatu paka minne wote watano tukawa tumehamia kwenye site zetu huku tukiendelea na finishing.

Jamaa alikuwa kila mwezi anaweka milioni moja kwenye mfuko mmoja wa uwekezaji wa pamoja na alikuwa anapata average interest kama ya 11.85% kwa mwaka. Badae akawa ananunua na bond za serikali pamoja na mambo ya kununua mashamba mbali kidogo na mji yakichangamka anakata na kuyauza. Kiufupi jamaa ana zaidi ya milioni 200 kwenye mfuko anaoweka pesa pamoja na kuwa na asset ya viwanja na mashamba na benki ana pesa chafu.

Turudi kwetu tuliojenga na sasa tuna mikoko yetu, umbali wa kwenda na kurudi nyumbani ni 50 Km kila siku. Na pia siwezi pata picha ile hofu ya kwamba nikiachishwa kazi bado ipo maana siwezi nikala nyumba.

Kwa ajili ya muda niishie hapa kwa leo, nipate mawazo ya watu wengine pia. Kiufupi mimi naona kuna mitaji mingi ya biashara na uwekezaji inapotea kwa huu mwamvuli wa kujenga na kununua hii mikoko.

Ahsanteni!!!
Kila mtu ajue namna ya kutumia pesa aliyoitafuta.
 
Back
Top Bottom