Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Fanya ujinga wote na ujuaji wote , lakni swala la kujenga halipingiki , tena Jenga mapema kabisa iwezekanavyo ,Habari,
"Tafuta kiwanja, Jenga, Oa/Olewa, nunua mkoko", njia hii na mawazo haya yamekuwa kwa vijana wengi wanaoanza maisha, hususani waliobarikiwa kupata ajira au biashara zao binafsi ambazo zinawapa kipato flani cha kuendesha maisha yao. Kwa uzoefu wangu hii imekuwa kati ya sababu moja kubwa zinazosababisha watu kuwa maskini na kushindwa kufikia uhuru wa kifedha.
Lakini tujiulize swali la msingi, kwanini watu wengi wameamua kuchagua njia hii ya maisha. Nimefanikiwa kuwahoji watu wengi kidogo kuhusu hili na majibu niliyoyapata mengi yalikuwa kama ifuatavyo:
- Gharama ya kupanga nyumba ziko juu sana, ni bora kujenga ya kwako.
- Nyumba ni asset.
- Usafiri ni shida sana eneo niliko jenga ni bora kuvuta gari yangu.
- Mama/baba mwenye nyumba ana gubu sana.
- Nikiwa na kwangu nakuwa na uhuru mkubwa sana.
- Siku nikifukuzwa kazi au biashara ikiyumba nibaki na pakulala na familia yangu.
Sababu hapo juu nyingi ni za maana kabisa ila tatizo ni kwamba njia zilizotumika kutatua hizo changamoto zinaongeza changamoto zaidi, kivipi?. Ngoja tujadili mambo machache kuhusiana na maisha ya watu wengi hususani mijini (e.g. Dar):
- Wengi wananunua viwanja maeneo ya mbali kutoka mahali wanapofanyia shughuli zao zinazowapa kipato.
- Baadhi ya hayo maeneo yana changamoto za miundombinu ya maji, umeme, barabara na hata kiusalama.
- Wengi wanajenga kwa kuunga unga sana, unaweza jenga nyumba hata miaka sita au zaidi. Kuna msemo wanasema "nyumba haiishi".
- Nyumba nyingi wanazojenga watu kukaa zinakuwa ni kubwa na za kifahari bila kukumbuka lengo la mwanzo lilikuwa ni makazi tu na sio jengo la maonesho (Hapo utajibiwa kuwa tunajenga mara moja ya kuzeekea)
Kuzingatia hizo hoja hapo juu, yafuatayo yanakuwa ni matokeo ya gharama za maisha baada ya huyu mtu kuhamia kwake:
- Gharama za usafiri au mafuta zinakuwa juu ukilinganisha na awali.
- Mazingira yanakuwa sio rafiki kwa familia kuishi, maana nyumba nyingi zinakuwa bado hazijaisha (Wengine wanasema unakuwa unaishi site).
- Kama una gari, gharama za matengenezo zinakuwa juu kwa sababu ya pengine barabara kuwa mbaya, lakini kwa kuwa unasafiri umbali mrefu kila siku, basi hata service ya gari utafanya mara nyingi zaidi.
- Pia kama una gari utalazimika kuendesha gari umbali mrefu kila siku, hii si nzuri kwako kiafya.
- Gharama za umeme na maji pia zinaweza kuongezeka kwa kuwa nyumba ni kubwa sasa na pengine maji hayajafika.
- Maeneo mengine hata watu hawajahamia wengi hivyo hata usalama unakuwa hatarini.
- Mara nyingi unaweza ukajikuta mbali na huduma bora za kijamii ikiwemo hospitali, shule, n.k.
***NOTE: Gharama zinaweza kuongezeka ukilinganisha na mwanzo.
Kwanini kuna hofu ya kuwekeza hizo pesa?
Tujiulize swali hili la msingi. Ni kweli baadhi ya watu wanatamani sana kuffanya biashara, lakini wengi wanasema, BIASHARA HAZITABIRIKI. Ni kweli kabisa, lakini ukweli ni kwamba hilo sio tatizo la watu kutokuwekeza.
SHIDA KUBWA NI WATU KUTOKUWA NA ELIMU YA FEDHA. Hili ni jambo la muhimu sana kwa vijana kupata elimu. kwanza kabisa sio kweli kwamba ukitaka kuwekeza ni lazima ukafanye biashara fulani kama kuuza nguo, vinywaji au duka la mangi. Unaweza ukafanya uwekezaji kwa njia nyingi sana ambazo hazitahitaji your active time kuweza kusimamia ila mwisho wa siku ukaja kuwa na uchumi mkubwa kabisa. Uwekezaji huu ni kama mifano ifuatayo:
- Kununua viwanja na mashamba (Kumba muda unavyokwenda ardhi inapanda thamani lakini nyumba inashuka thamani)
- Kununua hisa za makampuni
- Tressury Bonds and Bills
- Mifuko ya uwekezaji ya pamoja (e.g. UTTAMIS)
- Fixed deposits accounts
- Kuwekeza kwenye elimu (Hii sio lazima zile za darasani, inaweza kuwa hata kujiendeleza katika fani flani)
- N.k.
La muhimu ni kupata elimu sahihi ya mambo ya fedha ili ujue jinsi ya kufanya maamuzi ni vipi utumie pesa yako.
Ngoja nitoe mfano halisi mmoja ulio hai kabisa kwa lengo la kupata uhalisia wa ninacho kisema:
Mwaka 2013 niliajiriwa mahali na tulikuwa kama waajiriwa sita wapya katika hiyo kampuni, mwenzetu mmoja alikuwa na uelewa mkubwa sana wa mambo ya fedha, na mara nyingi alikuwa anatushauri kuhusu haya mambo lakini tulikuwa tunamuona kama kachanganyikiwa: Mimi na wenzangu wengine wa tano tulikwenda mahali tukanunua viwanja na kuanza kujenga kwa kasi sana na badae tukachuku na mikopo kuongeza kasi hiyo. Kwa haraka haraka kwa wastani tuliweza kutenga kama milioni moja kwa mwezi kila mmoja wetu kwa ajiri ya miradi ya ujenzi. Mungu si athumani baada ya miaka mitatu paka minne wote watano tukawa tumehamia kwenye site zetu huku tukiendelea na finishing.
Jamaa alikuwa kila mwezi anaweka milioni moja kwenye mfuko mmoja wa uwekezaji wa pamoja na alikuwa anapata average interest kama ya 11.85% kwa mwaka. Badae akawa ananunua na bond za serikali pamoja na mambo ya kununua mashamba mbali kidogo na mji yakichangamka anakata na kuyauza. Kiufupi jamaa ana zaidi ya milioni 200 kwenye mfuko anaoweka pesa pamoja na kuwa na asset ya viwanja na mashamba na benki ana pesa chafu.
Turudi kwetu tuliojenga na sasa tuna mikoko yetu, umbali wa kwenda na kurudi nyumbani ni 50 Km kila siku. Na pia siwezi pata picha ile hofu ya kwamba nikiachishwa kazi bado ipo maana siwezi nikala nyumba.
Kwa ajili ya muda niishie hapa kwa leo, nipate mawazo ya watu wengine pia. Kiufupi mimi naona kuna mitaji mingi ya biashara na uwekezaji inapotea kwa huu mwamvuli wa kujenga na kununua hii mikoko.
Ahsanteni!!!
Uko sahihi. Ukihesabu pesa inayopita mkononi mwa waajiriwa halafu tunastaafu kwa nyumba na gari na makelele mengi eti watoto wetu hawana ajira ni umbumbumbu. Kama wazee wetu walishakosea inabidi kizazi hiki kibadilike kitambue asset (vitegauchumi) ni nini na liability ni nini.Waajiriwa tunawaza kujenga na kununua gari tu. Hapo tunaona malengo tumetimiza...then tunasubir kufa.. watoto watapambana wenyewe kivyao
Tatizo ni pale unapomaliza kujenga geto kali la 25M na kibarua kikaota nyasi wakati mwenzako alitumia 10M kununua ekari 5 na kufuga mbuzi/ kondoo/kitimoto halafu na yeye kibarua kikaota nyasi. Kuna mtu atalia kimoyomoyo ila kuna mwingime atapiga yowe.Ni kweli,ingekua rahisi hivo ukiwekeza unapata wafanyabiashara kariakoo wasingekua wanalia vile km ni rahisi
Mtu akipata pa kuhifadhi familia kwanza inasaidia kupata akili ya Mambo mengine
Yaani ndugu una akili kubwa sana na unaona mbali sana.Tatizo ni pale unapomaliza kujenga geto kali la 25M na kibarua kikaota nyasi wakati mwenzako alitumia 10M kununua ekari 5 na kufuga mbuzi/ kondoo/kitimoto halafu na yeye kibarua kikaota nyasi. Kuna mtu atalia kimoyomoyo ila kuna mwingime atapiga yowe.
Yaani acha tu, akili zetu naona kama haziangalii mbali. Tuna shidwa kuwekeza ili vizazi vijavyo viendeleze uwekezaji na kujikwamua kwenye uchumi hapo baadae, tunaendekeza kuridhika na nyumba na gari.Uko sahihi. Ukihesabu pesa inayopita mkononi mwa waajiriwa halafu tunastaafu kwa nyumba na gari na makelele mengi eti watoto wetu hawana ajira ni umbumbumbu. Kama wazee wetu walishakosea inabidi kizazi hiki kibadilike kitambue asset (vitegauchumi) ni nini na liability ni nini.
Hatujakataa ila jenga ukiwa umeshafanya uwekezaji wa kutosha. Mfano umeajiriwa, umechukuwa mkopo na ukajenga au umejichanga kwa miaka 5-10 ukajenga baada ya kumaliza kazi au kuachichwa kazi lazima tu hiyo nyumba utaiuza/kuikopea mkopo ujikimu, mwisho wa siku maisha yako yanakuwa yanarudi pale pale kwenye hali ya utumwa.Fanya ujinga wote na ujuaji wote , lakni swala la kujenga halipingiki , tena Jenga mapema kabisa iwezekanavyo ,
Unaweza ukasema hivyo ndugu lakini kuna watu walinunua mashamba mvuti, msongola na maeneo mengine miaka 5 - 8 iliyopita wakati huo ilikuwa poli, lakini huwezi kuamini leo hii mashamba hayo yalikatwa katwa vipande vidogo vidogo, kila kipande Milioni 2.5, mtu anaheka zake tatu kila heka katowa vipande 8 na kila heka moja aliinunua laki 1, leo hii kapata faida nyingi sana.Ardhi huwa haiongezeki thamani ila pesa hupungua thamani tu.
Kiwanja tupu siyo uwekezaji ni kutupa hela kwa mategemeo ya kuiokota baadae.
Kununua ardhi bila kuiboresha na kuwa chanzo cha pesa ni sawa na kumkopesha hela mtu asiye na uwezo wa kulipa.
Hili nilishaliona kitambo, nikalifanyia kazi.Tatizo ni pale unapomaliza kujenga geto kali la 25M na kibarua kikaota nyasi wakati mwenzako alitumia 10M kununua ekari 5 na kufuga mbuzi/ kondoo/kitimoto halafu na yeye kibarua kikaota nyasi. Kuna mtu atalia kimoyomoyo ila kuna mwingime atapiga yowe.
Kuwekeza kwenye siyo kununua ardhi pekee mpaka ardhi husika iboreshwe ndiyo utakuwa uwekezaji.Unaweza ukasema hivyo ndugu lakini kuna watu walinunua mashamba mvuti, msongola na maeneo mengine miaka 5 - 8 iliyopita wakati huo ilikuwa poli, lakini huwezi kuamini leo hii mashamba hayo yalikatwa katwa vipande vidogo vidogo, kila kipande Milioni 2.5, mtu anaheka zake tatu kila heka katowa vipande 8 na kila heka moja aliinunua laki 1, leo hii kapata faida nyingi sana.
Baadhi ya viongozi duniani wanawekeza sana kwenye ardhi, si kwamba wajinga ila wanajuwa kibaruwa kikiota nyasi basi ardhi itakuwa suluhisho la kusonga mbele.
Tunatolea mfano ardhi kwa sababu unaweza kufanyia mambo mengi, unaweza usiize ila ukawa unalima mihogo, karanga, kufugia na n.k, pia ni uwekezaji.
Hapa sio kwaoBoss una mawazo positive sana and for addin up wahindi na arabs especially wahindi wanafanya sana hizo mambo
Umesema vyema sanaUlitumia miaka mitatu kujenga means by 2016 ulikuwa umemaliza. Kuanzia 2016 hadi leo miaka zaidi ya sita bado haujawa stable, kama ulijenga kwa miaka mitatu imagine hii miaka sita ungekuwa makini ungesave kiasi gani!! Inaonekana ni wewe ndio mwenye shida.
Kujenga bongo ni rahisi sana, na ni risky sana kufanya biashara au kuinvest hilo halipingiki (of course ukitoboa umetoboa).. hizi principle za usijenge invest kwanza zinafaa Marekani na Ulaya ambako kujenga ni ghali sana. Bongo ukipata pesa jenga uepushe aibu za hapa na pale.
Nakazia.Usijenge nyumba kwa fedha za mkopo wa mshahara.. kama uta ndoto za kuwa tajiri
Kuwekeza kwenye siyo kununua ardhi pekee mpaka ardhi husika iboreshwe ndiyo utakuwa uwekezaji.
Ardhi haipandi thamani bila kuboreshwa bali kinachotokea ni pesa kushuka thamani tu.
..mkuu upo sahihi kama umenunua maeneo yanayochelewa..lakini tumeshuhudia watu wakiuza plots zaidi ya 2B kariakoo miaka ya karibuni ambayo ilikuwa kwa miaka ya 1990 walinunua kwa malaki tu...maeneo kama mbweni miaka ya 2000 yalikuwa mapori watu wakinunua kwa 1-2m ila leo kiwanja kinaenda hadi 250m....so ni kununua maeneo ambayo unaona kuna potential inakuja ndani ya 10yrs lazima upate faida kubwa sana kwenye ardhiKuwekeza kwenye siyo kununua ardhi pekee mpaka ardhi husika iboreshwe ndiyo utakuwa uwekezaji.
Ardhi haipandi thamani bila kuboreshwa bali kinachotokea ni pesa kushuka thamani tu.
Tusidanganyane kibongo bongo kama una familia nyumba muhimu sana, Utakufa uache majanga huku nyumaUsijenge nyumba kwa fedha za mkopo wa mshahara.. kama uta ndoto za kuwa tajiri
What if ukizeeka na huna hela ya kulipa kodi, au mambo yakenda komboUnajenga ukizeeka nyumba ni pagale na huna pesa..