Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Majanga gan? Jitahid uache asset mkuu. Ukifa na hawana kitu,hata hyo nyumba wataiweka sokoni.Tusidanganyane kibongo bongo kama una familia nyumba muhimu sana, Utakufa uache majanga huku nyuma
SIku hazifanani tafuta asset ukiwa Kwako no body knows about tomorrow...Majanga gan? Jitahid uache asset mkuu. Ukifa na hawana kitu,hata hyo nyumba wataiweka sokoni.
Ni bora ni keshe bar na mademu wa kila aina sijui maswala ya kujenga sijui kununua gari ya kazi gani??Habari,
"Tafuta kiwanja, Jenga, Oa/Olewa, nunua mkoko", njia hii na mawazo haya yamekuwa kwa vijana wengi wanaoanza maisha, hususani waliobarikiwa kupata ajira au biashara zao binafsi ambazo zinawapa kipato flani cha kuendesha maisha yao. Kwa uzoefu wangu hii imekuwa kati ya sababu moja kubwa zinazosababisha watu kuwa maskini na kushindwa kufikia uhuru wa kifedha.
Lakini tujiulize swali la msingi, kwanini watu wengi wameamua kuchagua njia hii ya maisha. Nimefanikiwa kuwahoji watu wengi kidogo kuhusu hili na majibu niliyoyapata mengi yalikuwa kama ifuatavyo:
- Gharama ya kupanga nyumba ziko juu sana, ni bora kujenga ya kwako.
- Nyumba ni asset.
- Usafiri ni shida sana eneo niliko jenga ni bora kuvuta gari yangu.
- Mama/baba mwenye nyumba ana gubu sana.
- Nikiwa na kwangu nakuwa na uhuru mkubwa sana.
- Siku nikifukuzwa kazi au biashara ikiyumba nibaki na pakulala na familia yangu.
Sababu hapo juu nyingi ni za maana kabisa ila tatizo ni kwamba njia zilizotumika kutatua hizo changamoto zinaongeza changamoto zaidi, kivipi?. Ngoja tujadili mambo machache kuhusiana na maisha ya watu wengi hususani mijini (e.g. Dar):
- Wengi wananunua viwanja maeneo ya mbali kutoka mahali wanapofanyia shughuli zao zinazowapa kipato.
- Baadhi ya hayo maeneo yana changamoto za miundombinu ya maji, umeme, barabara na hata kiusalama.
- Wengi wanajenga kwa kuunga unga sana, unaweza jenga nyumba hata miaka sita au zaidi. Kuna msemo wanasema "nyumba haiishi".
- Nyumba nyingi wanazojenga watu kukaa zinakuwa ni kubwa na za kifahari bila kukumbuka lengo la mwanzo lilikuwa ni makazi tu na sio jengo la maonesho (Hapo utajibiwa kuwa tunajenga mara moja ya kuzeekea)
Kuzingatia hizo hoja hapo juu, yafuatayo yanakuwa ni matokeo ya gharama za maisha baada ya huyu mtu kuhamia kwake:
- Gharama za usafiri au mafuta zinakuwa juu ukilinganisha na awali.
- Mazingira yanakuwa sio rafiki kwa familia kuishi, maana nyumba nyingi zinakuwa bado hazijaisha (Wengine wanasema unakuwa unaishi site).
- Kama una gari, gharama za matengenezo zinakuwa juu kwa sababu ya pengine barabara kuwa mbaya, lakini kwa kuwa unasafiri umbali mrefu kila siku, basi hata service ya gari utafanya mara nyingi zaidi.
- Pia kama una gari utalazimika kuendesha gari umbali mrefu kila siku, hii si nzuri kwako kiafya.
- Gharama za umeme na maji pia zinaweza kuongezeka kwa kuwa nyumba ni kubwa sasa na pengine maji hayajafika.
- Maeneo mengine hata watu hawajahamia wengi hivyo hata usalama unakuwa hatarini.
- Mara nyingi unaweza ukajikuta mbali na huduma bora za kijamii ikiwemo hospitali, shule, n.k.
***NOTE: Gharama zinaweza kuongezeka ukilinganisha na mwanzo.
Kwanini kuna hofu ya kuwekeza hizo pesa?
Tujiulize swali hili la msingi. Ni kweli baadhi ya watu wanatamani sana kuffanya biashara, lakini wengi wanasema, BIASHARA HAZITABIRIKI. Ni kweli kabisa, lakini ukweli ni kwamba hilo sio tatizo la watu kutokuwekeza.
SHIDA KUBWA NI WATU KUTOKUWA NA ELIMU YA FEDHA. Hili ni jambo la muhimu sana kwa vijana kupata elimu. kwanza kabisa sio kweli kwamba ukitaka kuwekeza ni lazima ukafanye biashara fulani kama kuuza nguo, vinywaji au duka la mangi. Unaweza ukafanya uwekezaji kwa njia nyingi sana ambazo hazitahitaji your active time kuweza kusimamia ila mwisho wa siku ukaja kuwa na uchumi mkubwa kabisa. Uwekezaji huu ni kama mifano ifuatayo:
- Kununua viwanja na mashamba (Kumba muda unavyokwenda ardhi inapanda thamani lakini nyumba inashuka thamani)
- Kununua hisa za makampuni
- Tressury Bonds and Bills
- Mifuko ya uwekezaji ya pamoja (e.g. UTTAMIS)
- Fixed deposits accounts
- Kuwekeza kwenye elimu (Hii sio lazima zile za darasani, inaweza kuwa hata kujiendeleza katika fani flani)
- N.k.
La muhimu ni kupata elimu sahihi ya mambo ya fedha ili ujue jinsi ya kufanya maamuzi ni vipi utumie pesa yako.
Ngoja nitoe mfano halisi mmoja ulio hai kabisa kwa lengo la kupata uhalisia wa ninacho kisema:
Mwaka 2013 niliajiriwa mahali na tulikuwa kama waajiriwa sita wapya katika hiyo kampuni, mwenzetu mmoja alikuwa na uelewa mkubwa sana wa mambo ya fedha, na mara nyingi alikuwa anatushauri kuhusu haya mambo lakini tulikuwa tunamuona kama kachanganyikiwa: Mimi na wenzangu wengine wa tano tulikwenda mahali tukanunua viwanja na kuanza kujenga kwa kasi sana na badae tukachuku na mikopo kuongeza kasi hiyo. Kwa haraka haraka kwa wastani tuliweza kutenga kama milioni moja kwa mwezi kila mmoja wetu kwa ajiri ya miradi ya ujenzi. Mungu si athumani baada ya miaka mitatu paka minne wote watano tukawa tumehamia kwenye site zetu huku tukiendelea na finishing.
Jamaa alikuwa kila mwezi anaweka milioni moja kwenye mfuko mmoja wa uwekezaji wa pamoja na alikuwa anapata average interest kama ya 11.85% kwa mwaka. Badae akawa ananunua na bond za serikali pamoja na mambo ya kununua mashamba mbali kidogo na mji yakichangamka anakata na kuyauza. Kiufupi jamaa ana zaidi ya milioni 200 kwenye mfuko anaoweka pesa pamoja na kuwa na asset ya viwanja na mashamba na benki ana pesa chafu.
Turudi kwetu tuliojenga na sasa tuna mikoko yetu, umbali wa kwenda na kurudi nyumbani ni 50 Km kila siku. Na pia siwezi pata picha ile hofu ya kwamba nikiachishwa kazi bado ipo maana siwezi nikala nyumba.
Kwa ajili ya muda niishie hapa kwa leo, nipate mawazo ya watu wengine pia. Kiufupi mimi naona kuna mitaji mingi ya biashara na uwekezaji inapotea kwa huu mwamvuli wa kujenga na kununua hii mikoko.
Ahsanteni!!!
[emoji3][emoji3] Ponda mali kufa kwajaaaaa....!!!Ni bora ni keshe bar na mademu wa kila aina sijui maswala ya kujenga sijui kununua gari ya kazi gani??
Watu siku hizi wanakufa mapema sana.
Ni wekeze alafu ela zangu aje kula bwege mmoja hata simjui.
Au niache pesa zangu waje kuuana bure ya kazi gani.
Watoto wangu waje kurogwa ya kazi gani.
Mimi sijazaa machizi bana nimezaa watoto wazima wa akili sitaki hata mmoja aje kuwa chizi.
Nakula bata kwanzia January mpaka disemba.
Kazi nafanya tena kwa umahiri mkubwa sana.
Tena nikiwa tungi na hakuna anayejua.
Nalala na pombe nahamka na pombe.
Sina stress za maisha sijui nijenge wapi ili iweje.
Ninunue gari la nini wakati na miguu.
Kwanza mjini hakuna raha ya kuendesha gari.
Mwisho wa siku nitalipark alafu lipate kutu kwenye engine.
Nasema hivi bata tu bata tu bata
Mpaka kuku aone wivu.
Mangi shangali hapa cha pombe.
Napenda pombe sana yani asilimia 75% ya mwili wangu ni alcohol water.
Pombe yenyewe yesu aliibariki
Hakika Kuna Jambo la kujifunza kutoka kwenye huu Uzi.Hongera Sana mkuu kwa elimu yako nzuriKwenye kuwekeza kuna mawili
1)win
2)loss
Wekeza taratibu,huku ukijenga usipeleke mtaji wote kwenye kuwekeza
Kweli bwashee[emoji3][emoji3] Ponda mali kufa kwajaaaaa....!!!
Kula bia kula bata na watoto vifaranga wakeNi bora ni keshe bar na mademu wa kila aina sijui maswala ya kujenga sijui kununua gari ya kazi gani??
Watu siku hizi wanakufa mapema sana.
Ni wekeze alafu ela zangu aje kula bwege mmoja hata simjui.
Au niache pesa zangu waje kuuana bure ya kazi gani.
Watoto wangu waje kurogwa ya kazi gani.
Mimi sijazaa machizi bana nimezaa watoto wazima wa akili sitaki hata mmoja aje kuwa chizi.
Nakula bata kwanzia January mpaka disemba.
Kazi nafanya tena kwa umahiri mkubwa sana.
Tena nikiwa tungi na hakuna anayejua.
Nalala na pombe nahamka na pombe.
Sina stress za maisha sijui nijenge wapi ili iweje.
Ninunue gari la nini wakati na miguu.
Kwanza mjini hakuna raha ya kuendesha gari.
Mwisho wa siku nitalipark alafu lipate kutu kwenye engine.
Nasema hivi bata tu bata tu bata
Mpaka kuku aone wivu.
Mangi shangali hapa cha pombe.
Napenda pombe sana yani asilimia 75% ya mwili wangu ni alcohol water.
Pombe yenyewe yesu aliibariki
Sjaelewa unaposema wanasiasa kama mawaziri wanapata pesa kutokana na mifumo isiyo rasmi... mifumo isiyorasmi ni ipi inayowapatia pesa hawa watu?Aridhi anapanda thamani ila aridhi ni sehemu ndogo ya nyumba kwa jumla kwa mfano nyumba yote ni 100m lakini aridhi uliipata kwa 10m, kwahiyo ni 10% ya nyumba yote upandaji wake hauwezi kuzidi ile gharama ya nyumba kijumla.
Nyumba kwa kweli liability ukiwa mtumishi wakawaida sio rahisi kutoboa maisha kwa kuwekuza kwenye nyumba kwanza,
Wanasiasa na watumishi wa juu kama mawaziri wakurugenzi wanajenga kwasbb wenyewe wana pata pesa nje ya mifumo rasimi.
Wizi wa mari za ummahSjaelewa unaposema wanasiasa kama mawaziri wanapata pesa kutokana na mifumo isiyo rasmi... mifumo isiyorasmi ni ipi inayowapatia pesa hawa watu?
Nmekuleta site kwangu uone hatua niliyofika umekuja kutangaza hukuKuna jamaa yangu Kaenda jenga bonge la mjengo mbondole. Katumia pesa nyingi sana kupambania mjengo ule. Kazi anafanyia posta. Jamaa kashindwa kabisa kuhamia mjengoni badala yake kamuweka mtu amtizamie.
Angetumia ile pesa kuinvest angekuwa mbali. Sasa hivi analalamika maisha yanamchapa anashindwa kula bata kumbe pesa alikopa na anakatwa pesa ndefu ya mkopo.
..mkuu upo sahihi kama umenunua maeneo yanayochelewa..lakini tumeshuhudia watu wakiuza plots zaidi ya 2B kariakoo miaka ya karibuni ambayo ilikuwa kwa miaka ya 1990 walinunua kwa malaki tu...maeneo kama mbweni miaka ya 2000 yalikuwa mapori watu wakinunua kwa 1-2m ila leo kiwanja kinaenda hadi 250m....so ni kununua maeneo ambayo unaona kuna potential inakuja ndani ya 10yrs lazima upate faida kubwa sana kwenye ardhi
mkuu mm nimeishi kariakoo miaka ya mwanzoni ya 90s nikiwa mdogo wakati ambapo nyumba nyingi zilikuwa za tope na mawe..enzi hizo kariakoo baadhi ya maeneo yalikuwa uswahilini sana na barabara mbovu sana..hizo nyumba zilikuwa squata na wenyeji wake walikuwa wazaramo&wandengereko..kuna maeneo laki tisa yaliuzwa hasa uelekeo wa jangwani...maeneo ya katikati ya kariakoo kama DDC & msimbazi yalikuwa bei ya juu maana yalishachangamka!Ni uongo kusema Kariakoo mwaka 1990 kiwanja kilikuwa kinauza laki.
Viwanja yombo vituka viliuzwa kwa laki mbili mpaka tatu mwaka 1988..
Baba yangu alinunua kiwanja enzi hizo yombo.. sasa why useme kariakoo mwaka 90 viwanja vilikuwa laki.
Viwanja vya kariakoo mpaka mwaka 1961 tunapata uhuru..tayari vilikuwa havigusiki...
Kariakoo na posta ni mjini kitambo
Word[emoji106]1.) Tungekuwa tunapanga nyumba za serikali hapo sawa LAKINI nyumba ya mstaafu kilasiku anaikagua na kunisimulia alivyojibana kujenga hapana aisee... Nasasa huwezi kujenga town center inabidi utoke kidogo
2.) Usafiri wa daladala kugombania,kushika bomba na kucheleweshwa job kilasiku huku umeulamba nayo haifai ntatafuta kagari kakunilinda mjini.
3.) Biashara inaweza kukuchomesha ukafukuzwa hadi nyumba yakupanga kwakukosa Kodi ukadhalilika na familia yako ama ukajikuta umechanganyikiwa unaingia kwakila mganga mpaka ukakosa pakuchanjwa!!
Kilamtu ajiangalie Aishi Kwa maarifa na uelekeo unaomfaa hatuwezi kuigana wooote tuanze na biashara/uwekezaji!! Wengine tutakuja baadae tukishajiweka kimkakati.
Hongera mkuu somo zuri.Habari,
"Tafuta kiwanja, Jenga, Oa/Olewa, nunua mkoko", njia hii na mawazo haya yamekuwa kwa vijana wengi wanaoanza maisha, hususani waliobarikiwa kupata ajira au biashara zao binafsi ambazo zinawapa kipato flani cha kuendesha maisha yao. Kwa uzoefu wangu hii imekuwa kati ya sababu moja kubwa zinazosababisha watu kuwa maskini na kushindwa kufikia uhuru wa kifedha.
Lakini tujiulize swali la msingi, kwanini watu wengi wameamua kuchagua njia hii ya maisha. Nimefanikiwa kuwahoji watu wengi kidogo kuhusu hili na majibu niliyoyapata mengi yalikuwa kama ifuatavyo:
- Gharama ya kupanga nyumba ziko juu sana, ni bora kujenga ya kwako.
- Nyumba ni asset.
- Usafiri ni shida sana eneo niliko jenga ni bora kuvuta gari yangu.
- Mama/baba mwenye nyumba ana gubu sana.
- Nikiwa na kwangu nakuwa na uhuru mkubwa sana.
- Siku nikifukuzwa kazi au biashara ikiyumba nibaki na pakulala na familia yangu.
Sababu hapo juu nyingi ni za maana kabisa ila tatizo ni kwamba njia zilizotumika kutatua hizo changamoto zinaongeza changamoto zaidi, kivipi?. Ngoja tujadili mambo machache kuhusiana na maisha ya watu wengi hususani mijini (e.g. Dar):
- Wengi wananunua viwanja maeneo ya mbali kutoka mahali wanapofanyia shughuli zao zinazowapa kipato.
- Baadhi ya hayo maeneo yana changamoto za miundombinu ya maji, umeme, barabara na hata kiusalama.
- Wengi wanajenga kwa kuunga unga sana, unaweza jenga nyumba hata miaka sita au zaidi. Kuna msemo wanasema "nyumba haiishi".
- Nyumba nyingi wanazojenga watu kukaa zinakuwa ni kubwa na za kifahari bila kukumbuka lengo la mwanzo lilikuwa ni makazi tu na sio jengo la maonesho (Hapo utajibiwa kuwa tunajenga mara moja ya kuzeekea)
Kuzingatia hizo hoja hapo juu, yafuatayo yanakuwa ni matokeo ya gharama za maisha baada ya huyu mtu kuhamia kwake:
- Gharama za usafiri au mafuta zinakuwa juu ukilinganisha na awali.
- Mazingira yanakuwa sio rafiki kwa familia kuishi, maana nyumba nyingi zinakuwa bado hazijaisha (Wengine wanasema unakuwa unaishi site).
- Kama una gari, gharama za matengenezo zinakuwa juu kwa sababu ya pengine barabara kuwa mbaya, lakini kwa kuwa unasafiri umbali mrefu kila siku, basi hata service ya gari utafanya mara nyingi zaidi.
- Pia kama una gari utalazimika kuendesha gari umbali mrefu kila siku, hii si nzuri kwako kiafya.
- Gharama za umeme na maji pia zinaweza kuongezeka kwa kuwa nyumba ni kubwa sasa na pengine maji hayajafika.
- Maeneo mengine hata watu hawajahamia wengi hivyo hata usalama unakuwa hatarini.
- Mara nyingi unaweza ukajikuta mbali na huduma bora za kijamii ikiwemo hospitali, shule, n.k.
***NOTE: Gharama zinaweza kuongezeka ukilinganisha na mwanzo.
Kwanini kuna hofu ya kuwekeza hizo pesa?
Tujiulize swali hili la msingi. Ni kweli baadhi ya watu wanatamani sana kuffanya biashara, lakini wengi wanasema, BIASHARA HAZITABIRIKI. Ni kweli kabisa, lakini ukweli ni kwamba hilo sio tatizo la watu kutokuwekeza.
SHIDA KUBWA NI WATU KUTOKUWA NA ELIMU YA FEDHA. Hili ni jambo la muhimu sana kwa vijana kupata elimu. kwanza kabisa sio kweli kwamba ukitaka kuwekeza ni lazima ukafanye biashara fulani kama kuuza nguo, vinywaji au duka la mangi. Unaweza ukafanya uwekezaji kwa njia nyingi sana ambazo hazitahitaji your active time kuweza kusimamia ila mwisho wa siku ukaja kuwa na uchumi mkubwa kabisa. Uwekezaji huu ni kama mifano ifuatayo:
- Kununua viwanja na mashamba (Kumba muda unavyokwenda ardhi inapanda thamani lakini nyumba inashuka thamani)
- Kununua hisa za makampuni
- Tressury Bonds and Bills
- Mifuko ya uwekezaji ya pamoja (e.g. UTTAMIS)
- Fixed deposits accounts
- Kuwekeza kwenye elimu (Hii sio lazima zile za darasani, inaweza kuwa hata kujiendeleza katika fani flani)
- N.k.
La muhimu ni kupata elimu sahihi ya mambo ya fedha ili ujue jinsi ya kufanya maamuzi ni vipi utumie pesa yako.
Ngoja nitoe mfano halisi mmoja ulio hai kabisa kwa lengo la kupata uhalisia wa ninacho kisema:
Mwaka 2013 niliajiriwa mahali na tulikuwa kama waajiriwa sita wapya katika hiyo kampuni, mwenzetu mmoja alikuwa na uelewa mkubwa sana wa mambo ya fedha, na mara nyingi alikuwa anatushauri kuhusu haya mambo lakini tulikuwa tunamuona kama kachanganyikiwa: Mimi na wenzangu wengine wa tano tulikwenda mahali tukanunua viwanja na kuanza kujenga kwa kasi sana na badae tukachuku na mikopo kuongeza kasi hiyo. Kwa haraka haraka kwa wastani tuliweza kutenga kama milioni moja kwa mwezi kila mmoja wetu kwa ajiri ya miradi ya ujenzi. Mungu si athumani baada ya miaka mitatu paka minne wote watano tukawa tumehamia kwenye site zetu huku tukiendelea na finishing.
Jamaa alikuwa kila mwezi anaweka milioni moja kwenye mfuko mmoja wa uwekezaji wa pamoja na alikuwa anapata average interest kama ya 11.85% kwa mwaka. Badae akawa ananunua na bond za serikali pamoja na mambo ya kununua mashamba mbali kidogo na mji yakichangamka anakata na kuyauza. Kiufupi jamaa ana zaidi ya milioni 200 kwenye mfuko anaoweka pesa pamoja na kuwa na asset ya viwanja na mashamba na benki ana pesa chafu.
Turudi kwetu tuliojenga na sasa tuna mikoko yetu, umbali wa kwenda na kurudi nyumbani ni 50 Km kila siku. Na pia siwezi pata picha ile hofu ya kwamba nikiachishwa kazi bado ipo maana siwezi nikala nyumba.
Kwa ajili ya muda niishie hapa kwa leo, nipate mawazo ya watu wengine pia. Kiufupi mimi naona kuna mitaji mingi ya biashara na uwekezaji inapotea kwa huu mwamvuli wa kujenga na kununua hii mikoko.
Ahsanteni!!!
Kupanga ni kuchagua1.) Tungekuwa tunapanga nyumba za serikali hapo sawa LAKINI nyumba ya mstaafu kilasiku anaikagua na kunisimulia alivyojibana kujenga hapana aisee... Nasasa huwezi kujenga town center inabidi utoke kidogo