Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

Hakika nakuambia ukiwapa waTz 10 hata wenye hiyo elimu ya fedha Mil.60 baada ya miaka 4 ukija kuwathaminisha ni 1 au wawili ndio watakuwa na angalau 10Mil kwenye akaunti zao.
Hizi biashara tuheshimu pia, siyo rahisi kihivyo..kila siku watu wanateketeza mitaji.Mmeshasahau ya Kkoo na TRA ??

Kikubwa ni kuchukua maamuzi yenye mantiki na tija kwa muda huo.Mfano wapo amabo kujenga ni uamuzi sahihi zaidi kwa wakati huo na wapo ambao kununua gari na wapo ambao ni kuwekeza.
 
Too theoretically, Ila kwa ground watu wanajua biashara sio rahisi na ni game ngumu kuwin unaweza kuangukia pua mazima...Na hizo sijui hati fungani ,Fixed account lazima uwe na pesa ndefu ili kupata ROI kubwa angalau kwa mwaka.

Unaposema kuhusu gharama maisha kama kutumia usafiri binafsi wakati unakaa mbali upo sahihi , Gari linatesa kama utaenda kama linavyotaka basi utalia bado preventive maintenance mara sijui kubadili oil mara sijui nn na hapo hujapata ajali ,Pia tambua unalipia bima kwa mwaka.

Ishu ya biashara isikie mdomoni tu ,Asili ya mzunguko wa pesa za kibiashara hairuhusu watu wote kuwin sana sana kwa wanaoanza hawa wanapata tabu sana ... Biashara inaweza kukulaza tajiri ukaamka maskini kosa dogo unaanza upya .
 
inaonekana alichukua deni la mda mrefu
 
Mkuu najua hizi nondo umezipata kwenye kitabu cha ROBERT KIYOSAKI (RICH DAD & POOR DAD) bila shaka 💯
 
Nashkuru umenielewa mkuu maana wabongo ukiwaambia hiv watakutukana
Wanaosave pesa ndio wanaopoteza kwa Dunia ya Sasa

Wangapi wanaweza kufutika Milioni 100 na RoI ni asilimia ngapi?

By the way hata majengo ni biashara vile vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…