Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

Ukikopa mil 100, ukaiweka UTT , baada ya miaka 5 unakua na zaidi ya mil 300. lakini ukijenga nyumba ya mil 100 baada ya miaka 3 nyumba hiyo itakua na dhamani ha mil 50
Haya ni mawazo nadharia yaani theoretical..

1. Hizo Mil 100 za kuweka UTT anapata wapi ??

2. Fine, umesema anakopa hizi Mil.100..Je, anapata wapi dhamana ya kukopa Mil.100??

3. Sawa, Akikopa Mil.100, anakuwa na jukumu la kurejesha riba around 15 ~ 18% kwa mwaka.Let's say ni 15%, hapo anakuwa analipa 2.3Mil rejesho (na hii ji kwa redusing balance). Rejesho hili linalipwa na hela ipi ??

4.ROI kwa UTT ni around 10~13% kwa mwaka na at best wanalipa semi annually..so miezi 6 unapewa 6,500,000.Hapo una marejesho ya around Mil.13.8 kwa kipindi hicho hicho..Ukikurupuka utajua hujui..

Anyway..hizi mambo ukiwa kwenye karatasi ni rahisi sababu ni theory tuu ila uhalisia unahitaji utoshelezi wa mapato na umakini wa hali ya juu sana...Kutoboa at minimum ni kuwa na njia mbadala za mapato zaidi ya 2.
 
Mkuu umeleta mada nzuri sana ya kuelimisha, lakini haya mambo inategemeana na mtu yaani ukiizingatia na background ya mtu husika! Kijana ukifika karibia miaka 28/30 jambo la haraka Huwa ni kuwa na familia....na Kwa uzoefu, wengi hupata ajira kwenye miaka 25 na kuendelea, baada ya muda mfupi tu wengi tunaanza kuwa na familia zetu Kwa maana ya mke na watoto...(usisahau wategemezi) Kwa asilimia kubwa sana wengi lazima tuwaze makazi ya kudumu na Wala si biashara. Hii ni kwasababu ukishakuwa na familia ya watu 3.. kuendelea kuishi kwenye nyumba za kupanga Huwa Kuna ugumu wa Aina yake ukizingatia Life span na job security. Alafu uwaze business risk.....lazima uanze kujenga kwanza kinyume na hapo uwe na support ya maana kutoka kwenye familia yako. Jenga kwanza biashara ije baadae kma unatoka kwenye familia zetu za ki-Afrika.
 
Ukikopa mil 100, ukaiweka UTT , baada ya miaka 5 unakua na zaidi ya mil 300. lakini ukijenga nyumba ya mil 100 baada ya miaka 3 nyumba hiyo itakua na dhamani ha mil 50
Hii ni uongo bhna....

Riba ya mkopo wa 100M sio chini ya 20% kwa mwaka

Ukinunua bonds faida sio zaidi ya 10% kwa mwaka

Ni sawa na kuchota maji mtoni na kuweka baharini
 
Hii ni uongo bhna....

Riba ya mkopo wa 100M sio chini ya 20% kwa mwaka

Ukinunua bonds faida sio zaidi ya 10% kwa mwaka

Ni sawa na kuchota maji mtoni na kuweka baharini
Asante mkuu..Ndicho nilichokuwa nashangaa na mimi pia.Hiki anachoongelea mtoa mada ni cha nadharia tu na siyo uhalisia.

Mtaani hata kukopesheka hiyo Mil.100 ni kipengele.Kati ya wabongo 1,000 ni mmoja au wawili wana dhamana na biashara/cashflow ya kuweza kukopa Mil.100..
 
Mada ngumu sana hii coz ugumu wake una aspect mbili ambazo ukizingatia zote ni muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu.

1. Economically

●Economically tunasema nyumba na gari ni liabilty ( kwamba ni vitu ambavyo sio vizalisha pesa bali vitumia pesa) unless upangishe ikupe pesa au iwe gari ya biashara(ubber,bolt n.k).

●Kwaiyo economically kuwekeza hela yako
kwnye liabilty ni hasara na kunakufanya uwe na maisha magumu zaid kwa sababu hela uliyowekeza kwenye izo vitu haizalishi badala yake ina demand more money from you for maintenance , service etc.

● Hivyo kiuchumi hapa kipaumbele kinabadilika ukipata pesa ni lazima ujikite kuwekeza kwenye assets ie. vile vitu vitakavyokuzalishia uwe na pesa mingi zaid na zaid na hatimae kuachive economic freedom katika maisha yako.

● Sasa mwishoni hapa swala lina kuja ambalo kila mtu ana jibu lake binafsi. ARE YOU RISK TAKER??? maana unapofanya investment yoyote kama biashara n.k lazima ukubali kua risk taker. Kuna muda unaweza pata faida nono[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39] na kuna muda unaweza pata hasara[emoji852][emoji852]( hamna mtu anataka kusikia hasara na downfall )
Sasa kama risk taker lazima uwe tayari kwa yote? Je upo tayari??? na hapo ndio mitazamo tunapotofautiana wadau and where kipengele no. 2 kinapoingia.

2. WELFARE
● Welfare ni hali halisi ya maisha yako tunaongelea ile raha, burudani, faraja, ufahari, unayokua nayo katika maisha yako after investment. Ipo social, ipo economical welfare.

● Tuchambue taratibu ukijenga nyumba yako, ukakaa na familia yako, husumbuliwi kodi na mtu au mtu kukuaibisha kwenye jamii kisa haujamlipa kodi yake au mwingine anakutolea vyombo nje( its real humiliating infront of ua family) hii inaleta heshima, furaha kwnye maisha yako licha hata kama unakula mchicha ndani.

● Ukinunua gari jamn upo na mkoko wako hutembei ukapigwa na jua, ukiwa na mgonjwa unamuwaisha hosptali mwenyewe badala ya kusumbuwa watu wenye magari usiku, hunyeshewi na mvua, unatoka na familia yako umepakia wanao na mke wako, unaenda usiku kwenye masherehe bila stress za kuwachunga wenye magari wasikuache[emoji23][emoji23][emoji23]n.k na kurudi muda unaotaka, yaan kuna raha unaipata katika maisha.

●Kwaio vitu hiv vinawafanya watu waishi kwa raha, heshima na ufahari katika jamii.
Hiv imagine izo biashara zako ambazo hamna mtu anazijua kuzifanya unakufa ghafla hujajenga hata nyumba familia yako unaiachaje( mke na watoto wako) wakihaa mtaani hawana pa kwenda.

●kwaio ndio maana watu wengi wanaopt option ya WELFARE zaidi kuliko economical.
Je ndio uoga wa maisha? apo kila mtu ana jibu lake kutokana na uwezo wa wa KUTAKE RISK.

Ila mm nashauri vyote vifanyike ila hakikisha assets unakua nazo nyingi kuliko liabilty. haya maisha hayaepukiki bila kuna na nyumba na vitu vingine ambvyo vifnaya mtu afurahie maisha. Hatujaumbwa kuteseka afterall[emoji3][emoji3]
 
Unachokizungumzia kiko sahihi, lakini tukumbuke bila uwekezaji kwaji, utajikuta taratibu unauza nyumba, gari na vinginevyo kisha unaanza upya tena.

Uwekezaji uanze mambo mengine yafuata, ila tu ukiwa ndani ya umri wa 18 - 50, zaidi ya hapo wewe Jenga na utulie na familia yako. Ogopa kulaulika katika umri wa kuanzia 50 na kuendelea, hakika unaweza ukumbuka ujana wako, ulikuwa unafanya nini. Starehe zipo tu na hazitaisha.
 
Ukikopa mil 100, ukaiweka UTT , baada ya miaka 5 unakua na zaidi ya mil 300. lakini ukijenga nyumba ya mil 100 baada ya miaka 3 nyumba hiyo itakua na dhamani ha mil 50
Kwamba unamaanisha ardhi haipandi thamani inashuka kila iitwayo siku au mimi ndio sikujakuelewa vizuri? Yani ujenge leo jengo lako la thamani ya milioni 100 halafu baada ya maka 5 thamani ishuke mpaka milioni 50 hiyo ardhi haipandi thamani?
 
Katika swala la nyumba kuwa 'liability' nafikiri inategemeana na aina ya ajira ambayo muhusika yuko nayo mfano kama amejiajiri na anafanya biashara nyumba huwezi kuiweka kama 'liability' kwake bali inakuwa 'asset' kwake maana yaweza tumika kama dhamana (security) mathalani anahitaji mkopo wa biashara kutoka taasisi ya fedha (bank) ili apanue biashara yake. Mathalani nyumba yake ina thamani ya milioni 200 inakuwa ni ahueni kwake akitaka mfano mkopo wa milioni 150 kwaajili ya bishara zake na kufanya marejesho katika muda husika kwahiyo kwa wafanyabiashara/waliojiajiri dhamana (Security) ni kitu cha muhimu Sana kama sio cha lazima kwa ustawi wa biashara yako. Wito kwa vijana wasisite kujenga hasa wale waliojiajiri maana ni dhamana katika biashara zako hasa yale maeneo yaliyopimwa na yenye hati.
 
Aridhi anapanda thamani ila aridhi ni sehemu ndogo ya nyumba kwa jumla kwa mfano nyumba yote ni 100m lakini aridhi uliipata kwa 10m, kwahiyo ni 10% ya nyumba yote upandaji wake hauwezi kuzidi ile gharama ya nyumba kijumla.
Nyumba kwa kweli liability ukiwa mtumishi wakawaida sio rahisi kutoboa maisha kwa kuwekuza kwenye nyumba kwanza,
Wanasiasa na watumishi wa juu kama mawaziri wakurugenzi wanajenga kwasbb wenyewe wana pata pesa nje ya mifumo rasimi.
 
Kwa kada ya wafanyabiashara kuwa na nyumba ni jambo la muhimu kama sio la lazima maana yaweza kutumika kama dhamana (security) pindi unapohitaji kupanua/kuongeza mtaji wako wa biashara (working capital) kutoka taasisi ya fedha (benki)
 
Ukijenga nyumba kwa lengo ya kua dhamana au security bank hapo ndo umeferi kabisa bora unge tunza zile pesa ndo zikusaindie kupanua biashara yako Bank za Tz ni wezi ma lengo yao sio kukuinua but kukufilisi nyumba ya 200m itadhamini mkopo wa 30m au 50m ndo watakupa mkopo hiyo njia imefilisi wafanya biashara wengi.......kwahiyo ni vizuri kutunza cash kuliko kuiweka kwenye nyumba liquidity ni muhimu kuliko solid assets kwasbb na benki zinahitaji faida lazima wakufilisi.
 
Basi sawa. Wacha tujenge na tununuwe magari.
Wewe zungusha hela mpaka ipate kizunguzungu!
 
Kuna uhakika gani ange invest angekua mbali?

Usiwaze tu kua mbali kuna kupoteza
Una uhakika gani kama angejenga nyumba isingeungua au isingebomoka au kiwanja kisingekuwa na mgogoro?

Ni kwa kuzingatia angelipa bima ya nyumba na angetumia mwanasheria kununua kiwanja vitu vinavyoongeza gharama. Hivyo hivyo kwa uwekezaji kuna baadhi ya investments zina guarantee kubwa, mfano huyo rafiki yao aliyenunua t. bills kwa 11% ana uhakika wa kupata hiyo hela. Tanzania haijawahi default, hata Kenya last month ilifikia hatua haijalipa mishahara ila haiwezi kwepa kulipa hilo deni.
 
Kama tayari una familia basi nyumba iwe kitu cha kwanza.
Hapo ndo unaongeza umasikini kabisa, kwanza wekeza sehemu ya kuongeza kipato ndo uanze ujenzi, mtumishi anae pokea take home 1.5m itamchukulia miezi 60 kujenga nyumba ya wastani wa 50m hapo kajibana tayari ni miaka 5. Kwahiyo akiwa 35yrs tayari ataingia miaka 40, nyumba imuingizie chochote ila analazimika kusafiri umbali mkubwa ili aishi kwenye hiyo nyumba yake, kama anako fanyia kazi ni mbali na aliko jenga, wengi wanastafu bila kitu zaidi yanyumba nayenyewe anaigawa aishi na wapangaji kupata pesa ya kulipia utulities. Tafuta mahara pakuwekeza kabla ya kujenga nyumba kama wataka kutoboa haya maisha.
 
Kama una familia nyumba iwe kipaumbele mkuu.

Si kila mtu ni mjuzi wa kufanya biashara.
 
Kama una familia nyumba iwe kipaumbele mkuu.

Si kila mtu ni mjuzi wa kufanya biashara.
Sawa mkuu hiyo pesa ya kujenga nyumba residential utaipata wapi labda kama wasema kijenga shelter au kibanda, wanao jenga residential lazima awe na biashara inao support, mkopo haujengi nyumba ndungu yangu utaishi maisha ya dhiki na upate magonjwa kabla ya wakati wako au ufe mapema, kwa mfano mwenye mshahara 1.5m kulipia nyumba ya 150k kwa mwenzi inampa fursa ya kubakiza 1.35m kuwekeza kwenye hisa kwa miaka mitatu atatunza 30m anaweza kukuza mtaji kdgo mpaka atakapo jenga bila kuumiza maisha yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…