Kukatika umeme Uwanja wa Mkapa: Serikali yawasimamisha watendaji kadhaa; yaomba radhi
Wakina Karia ndio wanakaa kwenye Vikao vya kutoa gharama za Uwanja harafu mnakuja kuwalaumu watu wadogo wasio na maamuzi hii dhambi inaendelea kuwatafuna ,meneja wa Uwanja gani anaeweza kununua generator mpya au kukodisha hiyo kitu bila ya ruhusu ya hao wapiga hela kwa kutumia vikao...
 
Wizara pia iwajibike ni uzembe kutohakikisha kilichoshauriwa na watalaam. Ilitakiwa wizara ishuhudie usiku mmoja hayo majenereta yakiwa yamewashwa kwa msaa hata mawili ili kuangalia kama ushauri wa watalaam uko sawa.
 
huu uzembe upo kila mahali kipi hasa kinatustua kama sio unafiki …mara ngapi umeme unakatika ghafla maeneo nyeti kama Hospital na watu kupoteza maisha au kupata madhara wakiwa kwny vyumba vya upasuaji ?

nashangaa wanaoshangaa tukio hili na kujifanya kustuka

Umeme kukatika bila ya taarifa wala sababu maalum ni jambo la kawaida sana.

mie kinachonishangaza ni hawa Tanesco na Wizara kutoa ufafanuzi wa haraka ndani ya robo saa wakati mambo mengi ya msingi kuliko hili huwa wanapiga kimya

nahisi Mama alikuwa anacheki Game na akakerwa na ufala huu wa hawa stupid ndio sababu kila Mamlaka zimetoa maelezo haya mara moja
 
Kutokana na kujirudia kwa hali ya kukatika umeme katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ( Uwanja wa Taifa DSM) ikianza 28 Machi, 2023wakati wa mechi baina ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya timu ya
Taifa ya Uganda (Uganda the Cranes) kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)...​
Wakwanza kusimamishwa kazi alitakiwa awe waziri mwenyewe kwa kuchelewa kuchukua hatua sahihi kwa wakati sahihi na huo ni uzembe.

Tatizo hili la kuhujumu taifa limejirudia mara ya mara nyingine ndani ya takribani mwezi mmoja.

Huwenda kama hatua stahiki zingechukuliwa mapema aibu hii isingejirudia tena ila kwa sababu waziri na watu wake walichukulia powa na kwa vile wanafahamiana na watendji ndio tunakutana na aibu mbele ya macho ya dunia.

Hili sio la meneja tu ni la waziri mwenye dhamana na katibu mkuu wake.

Na kwa nini awe kaimu meneja kwa muda wote huo? Meneja yuko wapi?

Yawezekana mtu kakaimu madaraka kwa kipindi kirefu hivyo bado kunawakati anashindwa kufanya mamuzi sahihi nankwa wakati sahii kwa sababu yeye amemshikia mtu dhamana hivyo haoni uzito wa jukumu mabegani mwake.

Matamko ya kusimamishana hayaji mpaka afe mtu?

Uwanjani giza, je ulinzi na usalama wa mashabiki na maofisa wa mechi ingekuwaje?

Mi nadhani rungu lianzie juu sio chini!
 
Back
Top Bottom