Kukatika umeme Uwanja wa Mkapa: Serikali yawasimamisha watendaji kadhaa; yaomba radhi
Hapo wataenda kuitwa stupid yeshee.

Watarudi kukata umeme.
 
Wakwanza kusimamishwa kazi alitakiwa awe waziri mwenyewe kwa kuchelewa kuchukua hatua sahihi kwa wakati sahihi na huo ni uzembe.

Tatizo hili la kuhujumu taifa limejirudia mara ya mara nyingine ndani ya takribani mwezi mmoja.

Huwenda kama hatua stahiki zingechukuliwa mapema aibu hii isingejirudia tena ila kwa sababu waziri na watu wake walichukulia powa na kwa vile wanafahamiana na watendji ndio tunakutana na aibu mbele ya macho ya dunia.

Hili sio la meneja tu ni la waziri mwenye dhamana na katibu mkuu wake.

Na kwa nini awe kaimu meneja kwa muda wote huo? Meneja yuko wapi?

Yawezekana mtu kakaimu madaraka kwa kipindi kirefu hivyo bado kunawakati anashindwa kufanya mamuzi sahihi nankwa wakati sahii kwa sababu yeye amemshikia mtu dhamana hivyo haoni uzito wa jukumu mabegani mwake.

Matamko ya kusimamishana hayaji mpaka afe mtu?

Uwanjani giza, je ulinzi na usalama wa mashabiki na maofisa wa mechi ingekuwaje?

Mi nadhani rungu lianzie juu sio chini!
Kama hata hujui kwanini kuna kaimu na sio meneja kamili then kuna safari ndefu ya kukuelewesha, mengine tafuta kidogo usisubiri kulishwa tu
 
Give reasons?
hawajapewa fursa ya kusikilizwa

inawezekana wanaosimamisha wenzao ndio wanapaswa kusimamishwa

uchunguzi huru wa watu wa nje ya Wizara ndio wanaweza kutenda haki

Kama Waziri na Katibu hawakufanyia kazi mapendekezo ya kitaalam wanaweza kweli kujihukumu ?
 
Hii ilitakiwa iwe kwenye mechi ya Tanzania vs Uganda. Kuwaachia waendelee na majukumu ni kuwapa nafasi kufanya kile kilichotokea leo. Waziri Pindi Chana ungewajibika wewe kwanza.

Najua hizi ni hujuma za wazi ili Simba ikose nafasi ya Ushiriki wa Michuanonya CAF Super Cup kwa kukosa uwanja wa nyumbani.
Serikali inayoundwa na wezi wa kura haiwezi kuwa na ufanisi katika lolote
 
Mechi ya kimataifa halafu mnaomba radhi watanzania pekee?
Nchi zingine kwny mambo ya kipuuzi kama haya hakuna kuombana radhi kuna kulipana fidia kwa usumbufu na uzembe uliotokea

sie ndio Wazee wa '…Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza ' na ngoma inaishia hapo …nani kishawahi kuishitaki Tanesco kwa shoti zinazounguza Majumba ya watu na mali zingine kwa katika katika na ya kihabithi ya Umeme ?
 
Waziri Pindi Chana Ndio mawaziri wanawake walio onekana wanafaa kupewa wizara.

Kuna mwingine yuko Tamisemi nako Halmashauri zimeoza.

Kuna mwingine yuko kazi na ajira nako kumeoza.

Kuna mwingine kapewa magogoni Leo Msikilizeni huko Mei Mosi muone na mjifunze kuwa wanawake wakipewa nchi ni nini matokeo yake.
 
Wakina Karia ndio wanakaa kwenye Vikao vya kutoa gharama za Uwanja harafu mnakuja kuwalaumu watu wadogo wasio na maamuzi hii dhambi inaendelea kuwatafuna ,meneja wa Uwanja gani anaeweza kununua generator mpya au kukodisha hiyo kitu bila ya ruhusu ya hao wapiga hela kwa kutumia vikao...
Heri ungekaa kimya tu maana haufahamu muundo na mifumo ya utendaji serikalini, ndio maana unadhani Karia ndiye anayepanga makato ya uwanja wakati na yeye taasisi yake inagawiwa tu
 
Heri ungekaa kimya tu maana haufahamu muundo na mifumo ya utendaji serikalini
Nchi ina watu wa hovyo hii harafu mnajifanya kujua...makato ya TFF ya gharama za uwanja na muundo wako vinahusiana nini kununua generator nako kunahitaji muundo aisee Nchi ina watu wenye fikra za kimasikini sana hii
 
Bajeti ya July, yenyewe inategemea mkopo kutoka Bank ya Dunia.
Nchi hii ngumu sana utawalaumu hao waliosimamishwa bure.
Nchi nzima tunategemea uwanja mmoja maraisi wanapita tu hakuna anayewaza kujenga uwanja mpya.
 
Amewaonea tu. Uongozi umeingiliwa na wanasiasa. Kina January ndio wanahusika na hayo matatizo.
 
Nchi ina watu wa hovyo hii harafu mnajifanya kujua...makato ya TFF ya gharama za uwanja na muundo wako vinahusiana nini kununua generator nako kunahitaji muundo aisee Nchi ina watu wenye fikra za kimasikini sana hii
Sasa kwa akili yako unadhani Karia ndio anamaintain miundombinu ya Uwanja wa Mkapa? Au nikukumbushe ulichoandika?
Wakina Karia ndio wanakaa kwenye Vikao vya kutoa gharama za Uwanja harafu mnakuja kuwalaumu watu wadogo wasio na maamuzi hii dhambi inaendelea kuwatafuna ,meneja wa Uwanja gani anaeweza kununua generator mpya au kukodisha hiyo kitu bila ya ruhusu ya hao wapiga hela kwa kutumia vikao...
 
Sasa kwa akili yako unadhani Karia ndio anamaintain miundombinu ya Uwanja wa Mkapa? Au nikukumbushe ulichoandika?
Faza ishu ya generator ni ndogo sana wala sio Big deal naomba tuishie hapa kweli tumedumaa tupo busy tunajadili umeme wa Taa tuu ..
 
Back
Top Bottom