Kukithiri mauaji nchini: Waziri Masauni kukutana na viongozi Polisi kujadili. Aagiza wanaosajilia watu laini za simu wasakwe

Kukithiri mauaji nchini: Waziri Masauni kukutana na viongozi Polisi kujadili. Aagiza wanaosajilia watu laini za simu wasakwe

wapelekeni Polisi shule kwanza acheni mikwara Polisi wana njaa,shule hawana wakimkamata mtu wanachowaza ni namna gani atatoa hela na kumbambikia kesi basi ....
Shule kwa zile grades?
 
Mpaka sasa polisi wameshasababisha taharuki na vipo vingi sana kuliko Freeman Aikaeli Mbowe na wenzake!

NB: Masauni kwa lugha nyingine anajitahidi kufanya damage control baada ya vitengo vya polisi kubainika ni useless.
 
Sina imani na hili taifa mwenendo wake .
 
wapo watu ambao wanajadili mambo ambayo yapo kinyume na maadili, desturi za watanzania
nchi inafuata utawala wa sheria, sio utawala wa desturi za watanzania

eti wanaenda kukamata wanaojadili mambo yaliyo kinyume na maadili na desturi za Watanzania....

desturi za Kitanzania za kujadili ni zipi, jando, tambiko, ngoma na silaha za jadi ???

sheria gani zimeorodhesha desturi zinazoruhusiwa? waheshimiwa sana wanaongea rubbish sana
 
Anachojaribu kufanya ni ''damage control' baada ya Jeshi kuchafuka kwa kashfa ya Mtwara.

Mh Masauni anataka kuwaondoa watu katika mjadala mpana wa utendaji wa Jeshi la Polisi.

Waziri anataka kulifanya ''jeshi la kisasa'' kana kwamba jeshi ni tatizo na si watendaji wake

KUTOKANA na mauaji ya kijamii yanayoendelea nchini, Waziri amepanga kukutana na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi ili kupokea taarifa ya matukio pamoja na kujadili jinsi ya kudhibiti mauaji hayo.
Kuna vituko sana. Masauni yupo wizara hiyo kwa muda mrefu kama sikosei.
Wasiojulikana na yale tunayoyasikia anayajua. Hakuna hata siku moja alijadili hili hadi tunapozungumzia kashfa ya uchafu wa Jeshi Mtwara
Waziri Masauni amesema katika kikao hicho pia kitajadili jinsi ya kulifanya Jeshi la Polisi kuwa la kisasa katika kudhibiti matukio mbalimbali kiuhalifu nchini
Waziri hajui 'Wasioujulikana'? atawadhibiti 'kisasa' kwa njia gani
“Nitakua na kikao na Viongozi wa Jeshi la Polisi na IGP pale Wizarani kwa ajili ya kupitia matokeo ya kazi ya uchunguzi... kuweza kuhakikisha mauaji tunaweza tukayapunguza katika siku za usoni,” alisema Masauni.
Mauaji hayapunguzwi, yanadhibitiwa. Masauni hujui huu ni mwendelezo wa mbegu ya watu kupotea , kuumizwa , kuokotwa mitaroni na hata Polisi kudai wanaletwa na Bahari.
Masauni alizungumzia kuhusu uhalifu wa kimtandao ambapo aliliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka wanaosajilia watu laini za simu, wanaochafua viongozi na wanaosambaza picha chafu mitandaoni.
Hii ni kazi ya Wizara ya habari na mawasiliano, unaongeaje na Polisi bila wadau?
Uhalifu wa kimtandao limekuwa kubwa katika siku hizi ... Wapo watu wakitumia mitandao kudhalilisha watu wengine, wengine kufanya wizi na uitapeli.. wanajadili mambo kinyume na maadili, desturi za watanzania
Mh Waziri tatizo la mitandaoni lipo siku nyingi inashangaza unaliona leo.

Si kazi ya Jeshi la Polisi kujadili mila na desturi za Watanzania. Tuna makabila 120 Masauni anataka kutuaminisha tuna mila moja na kwamba ni kazi ya Wizara yake! phwee

Hili unalipa kipaumbele ili kuondoa Umma katika hoja, ukatili uliofanywa na Jeshi Mtwara

Mauaji ya Mtwara ni dalili ya matatizo ya muda mrefu sana.
Wananchi wamelalamikia Jeshi la Polisi kufumbia macho matukio mengi ya kihalifu kama ya watu kupotea, kuumizwa n.k.. Jeshi la Polisi limekuwa kimya au kutoa majibu yasiyoridhisha.

Jeshi kama chombo halina tatizo, tatizo tulilonalo ni uongozi wa Jeshi na Wizara
Waziri na IGP wajitathmini kama Umma una imani na utendaji wao

Mh Rais ''ametoa vifaa na kuboresha Masilah'' akitarajia utendaji mzuri, siyo masikitiko
Rais aliapa kulinda watu na mali zao, yanayotokea ni kumbebesha lawama bure, mjitathmini kama mnamtendea haki kwa uwepo wenu katika nafasi hizo.

Mna namna ya kumsaidia, si vikao bali kumpa Mh Rais nafasi ya kutafuta wasaidizi

Pascal Mayalla JokaKuu Tindo
 
Suala hapo ni kujiuliza, kwanini kipindi cha JPM haya matukio yalipungua sana na kwanini sasa hivi yameibuka sana. Hilo tu!
 
Wanazunguka kweli mbona hajazungumzia mauaji ya polisi kwa Raia maana ikitokea ishu moja upo uwezekano wa nyingine nyingi ila hatuna taarifa ila damu ni nzito nao watakuja kukamatwa kwa ishu nyingine kabisa Mungu ni mwema sana...
 
Suala hapo ni kujiuliza, kwanini kipindi cha JPM haya matukio yalipungua sana na kwanini sasa hivi yameibuka sana. Hilo tu!

Hayakupungua bali vyombo vya habari havikuwa vinaruhusiwa kutangaza, kwa kisingizio ya kuwa havina maslahi kwa taifa.
 
Kuna hili Masauni litakuharibia.

Hawa lazima ni police sio ccm hawa
20220130_101433.jpg
 
Yaani badala ya kuanza kuwawajibisha, unaenda kujadili na kuletewa report tena kutoka kwa walewale, ambao wanatuhumiwa kwenye matatizo yenyewe..... kaazi kwelikweli unayo waziri...
Inasikitisha sana
 
Waziri wangu acha UONGO,acha siasa na fanya kazi,sajili watanzania wote na wawe kwenye system's inayoongea nchi zima(including finger prints)na toa IDs kwa raia wako na id number inakua kama jina yaani unazaliwa nayo na kufa nayo.Waziri wangu mshauri President aigawe wizara hii na kuwa mbili,wizara ya polisi(usalama wa raia na mali zao)na Home Affairs (raia na immigrations)na President afutulie mbali wizara ambazo sio muhimu kwa Taifa.
Mbona zote zinafanya Kazi sawa ya kudili na usalama wa raia
 
Back
Top Bottom