Anachojaribu kufanya ni ''damage control' baada ya Jeshi kuchafuka kwa kashfa ya Mtwara.
Mh Masauni anataka kuwaondoa watu katika mjadala mpana wa utendaji wa Jeshi la Polisi.
Waziri anataka kulifanya ''jeshi la kisasa'' kana kwamba jeshi ni tatizo na si watendaji wake
KUTOKANA na mauaji ya kijamii yanayoendelea nchini, Waziri amepanga kukutana na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi ili kupokea taarifa ya matukio pamoja na kujadili jinsi ya kudhibiti mauaji hayo.
Kuna vituko sana. Masauni yupo wizara hiyo kwa muda mrefu kama sikosei.
Wasiojulikana na yale tunayoyasikia anayajua. Hakuna hata siku moja alijadili hili hadi tunapozungumzia kashfa ya uchafu wa Jeshi Mtwara
Waziri Masauni amesema katika kikao hicho pia kitajadili jinsi ya kulifanya Jeshi la Polisi kuwa la kisasa katika kudhibiti matukio mbalimbali kiuhalifu nchini
Waziri hajui 'Wasioujulikana'? atawadhibiti 'kisasa' kwa njia gani
“Nitakua na kikao na Viongozi wa Jeshi la Polisi na IGP pale Wizarani kwa ajili ya kupitia matokeo ya kazi ya uchunguzi... kuweza kuhakikisha mauaji tunaweza tukayapunguza katika siku za usoni,” alisema Masauni.
Mauaji hayapunguzwi, yanadhibitiwa. Masauni hujui huu ni mwendelezo wa mbegu ya watu kupotea , kuumizwa , kuokotwa mitaroni na hata Polisi kudai wanaletwa na Bahari.
Masauni alizungumzia kuhusu uhalifu wa kimtandao ambapo aliliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka wanaosajilia watu laini za simu, wanaochafua viongozi na wanaosambaza picha chafu mitandaoni.
Hii ni kazi ya Wizara ya habari na mawasiliano, unaongeaje na Polisi bila wadau?
Uhalifu wa kimtandao limekuwa kubwa katika siku hizi ... Wapo watu wakitumia mitandao kudhalilisha watu wengine, wengine kufanya wizi na uitapeli.. wanajadili mambo kinyume na maadili, desturi za watanzania
Mh Waziri tatizo la mitandaoni lipo siku nyingi inashangaza unaliona leo.
Si kazi ya Jeshi la Polisi kujadili mila na desturi za Watanzania. Tuna makabila 120 Masauni anataka kutuaminisha tuna mila moja na kwamba ni kazi ya Wizara yake! phwee
Hili unalipa kipaumbele ili kuondoa Umma katika hoja, ukatili uliofanywa na Jeshi Mtwara
Mauaji ya Mtwara ni dalili ya matatizo ya muda mrefu sana.
Wananchi wamelalamikia Jeshi la Polisi kufumbia macho matukio mengi ya kihalifu kama ya watu kupotea, kuumizwa n.k.. Jeshi la Polisi limekuwa kimya au kutoa majibu yasiyoridhisha.
Jeshi kama chombo halina tatizo, tatizo tulilonalo ni uongozi wa Jeshi na Wizara
Waziri na IGP wajitathmini kama Umma una imani na utendaji wao
Mh Rais ''ametoa vifaa na kuboresha Masilah'' akitarajia utendaji mzuri, siyo masikitiko
Rais aliapa kulinda watu na mali zao, yanayotokea ni kumbebesha lawama bure, mjitathmini kama mnamtendea haki kwa uwepo wenu katika nafasi hizo.
Mna namna ya kumsaidia, si vikao bali kumpa Mh Rais nafasi ya kutafuta wasaidizi
Pascal Mayalla JokaKuu Tindo