MziziMkavu• Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma. hili tatizo nimegundua ndi alilonalo mtoto wangu kwani hata akihema akiwa hajalala unasikia ule muungurumo au mlio wa pumzi ikipita kuingia au kutoka,sasa akilala ndio unakuta anakoroma,mbaya zaidi sasa hivi ameshikwa na mafua yaani anakoroma mpaka naogopa,naomba unisaidie hapa tafadhali.