Kukoroma usingizini: Fahamu chanzo na tiba yake

Crashwise hizo mada za MziziMkavu hata mimi nilishawahi kuzisoma,tatizo hapa ni umri wa huyu mtoto naona kama yeye ameanza mapema mno ndio maana nimetaka kujua kuwa ni hali ya kawaida,amerithi au inaweza kuwa ana matatizo ya kiafya!
 
Last edited by a moderator:
Dawa ya kukoroma Fanya hivi: Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma

na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.Mkuu.@
big s Ukipona nipe Feedback
 
Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea

watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma

huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya

wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati.

Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi?

Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile:

• Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma.

• Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma.

• Kuwa na misuli minene ya koo. Hii ni kwa wale watu wanene ambao hata nyama zao za koo pia hunenepa na kupanuka na suala hilo husababisha kukoroma, Pia watoto wenye tonsesi kubwa na adenoids baadhi ya wakati hukoroma.

• Kuwa na kilimi kikubwa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha kukoroma. Kilimi kirefu kinaweza kuzuia koo na pale kinapotikisika wakati hewa inapita kwa msukumo husababisha kukoroma.

• Sababu nyinginezo zinazoweza kumsababishia mtu akorome anapolala ni kuwa na umri mkubwa au uzee, imeshuhudiwa kuwa watu wa makamo na wazee hukoroma, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri unayoongezeka. Vilevile wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake. Kukoroma pia kunaweza kuwa ni tatizo la kurithi. Pombe, kuvuta sigara na matumizi ya baadhi ya dawa pia husababisha misuli ya koo ilegee na hivyo hupelekea mtu akorome. Kulala vibaya pia husababisha kukoroka kama vile kulala kichalichali, kwani hufanya nyama za koo zilegee na kuziba hewa.

Je, Dawa ya kukoroma ni nini?

Swali hilo limeulizwa sana na mimi katika kulijibu ningependa kusema kuwa, kujua sababu inayosababisha mtu akorome na kuitatua au kuiondoa sababu hiyo ndiko kunakotibu

kukoroma. Sote tunajua adha inayotokana na kukoroma, na sauti hiyo inavyosumbua hasa iwapo anayekoroma ni mtu wako wa karibu kama vile mumeo, mwenzi wako au

yoyote yule inayekubidi ulale naye karibu au katika kitanda kimojana hata chumba kimoja. Kukoroma pia huathiri usingizi wa mkoromaji kwani anayekoroka humbidi aamke mara kadhaa usingizini akijua au bila kujua kutokana njia zake za hewa kufunga kwa sekunde

kadhaa ambapo usingizi pia hukatika. Wanaokoroma pia hushindwa kulala vizuri suala linalopelekea asubuhi wawe wamechoka na kutofanya majukumu yao vyema, na pia wale wanaolala nao karibu hupatwa na matatizo kama hayo. Vilevile tunapaswa kujua kuwa

kukoroma kuna athari za kiafya za muda mrefu kwa mtu anayekoroma hivyo si jambo la kufanyia mzaha na ni tatizo ambalo linapaswa kushughulikiwa na kutatuliwa.
Wataalamu wanatuambia kuwa ili kujua kukoroma kwako kunasababishwa na nini ni bora

ushirikiane na mwenzi wako au yoyote unayelala naye ili akuchunguze pale unapolala na kujua jinsi mwili wako unavyokuwa pale unapokoroma. Ni bora aandae orodha na kuchunguza yafuatayo:

1. Kufunga mdomo na kukoroma kunaonyesha kuwa kuna matatizo ya ulimi.

2. Kufungua mdomo na kukoroma kunaonyesha unaweza kuwa na tatizo katika misuli au nyama za koo.

3. Kukoroma unapolala kichalichali kunaonyesha kuwa pengine kwa kubadilisha namna unavyolala kukoroma nako kunaweza kwisha.

4. Kukoroma wakati unapolala kwa kila mlalo kunaonyesha kwamba tatizo lako ni kubwa na pengine kunahitajia tiba kubwa zaidi.

Iwapo umebadilisha namna unavyolala na haikusaidia, unashauriwa ujaribu yafuatayo:

 Punguza uzito

 Safisha njia yako ya hewa. Kuwa na pua iliyoziba hufanya kupumua kuwe kugumu na

kusababisha kukoroma. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia dawa za kusaidia kupumua

kwa urahisi (nasal decongestants) zinazopatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa.

 Wacha kuvuta sigara.

 Lala mapema na pata usingizi wa kutosha kila mara huku ukijiepusha na kuchoka sana.

Kunyanyua kichwa kwa nchi 4 huweza kupunguza kasi ya kupumua na kusaidia ulimi na

taya kwenda mbele hali ambayo hupunguza kukoroma. Fanya hilo kwa tumia mito

maalum ya kupunguza kukoroma au lala bila mto.

Wataalamu pia wanasema kwamba unaweza kupunguza kukoroma kwa kutokula baadhi

ya vyakula au dawa kabla ya kulala ambavyo huongeza kukoroma. Vitu hivyo ni kama vile

o Kutokula mlo mkubwa kabla ya kulala.

o Kutokula vyakula vinavyotokana na maziwa au maziwa ya soya.

o Kutokunywa pombe kabla ya kulala.

o Kutotumia dawa aina ya antihistamines.

o Kutotumia vyakula au vinjwaji venye kafeini.

Vilevile wanaokoroma wanashauriwa kufanya mazoezi ya koo ambayo ni pamoja na

kuimba, kusoma kwa kurudia rudia voweli (a,e,i,o,u) kwa nguvu kwa dakika tatu mara

kadhaa kwa siku, kuweka ncha ya ulimi chini ya meno ya mbele na kurudisha ulimi nyuma

kwa dakika 3 kila siku au huku mdomo ukiwa wazi pelekea taya yako upande wa kulia na

wacha ibakie katika hali hiyo kwa sekunde 30. Huku mdomo ukiwa wazi, kaza misuli ya

nyuma ya koo na rudia kitendo hicho kwa sekunde thelathini. Unaweza kutizama kwenye

kioo na kuona jinsi kilimi kinavyokwenda juu na chini.

Iwapo kukoroma hakutoisha kwa kutumia njia hizo tofauti zilizoelezwa, usife moyo jaribu

kumuona daktari na akupe ushauri wa kitiba kuhusiana na tatizo hilo. Madakatari

wataalamu wa magonjwa ya pua, masikio na koo au ENT wanaweza kukusaidia zaidi

kutatua tatizo hilo. Siku hizi kuna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa mahospitalini ili kuondoa

kukoroma kama vile kifaa kinachowekwa kwenye meno, CPAP, kidude kinachowekwa

mdomoni au hata kufanyiwa operesheni ili kuondoa tatizo hilo.

hope itakuwa msaada kwako na wengine

MziziMkavu• Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma. hili tatizo nimegundua ndi alilonalo mtoto wangu kwani hata akihema akiwa hajalala unasikia ule muungurumo au mlio wa pumzi ikipita kuingia au kutoka,sasa akilala ndio unakuta anakoroma,mbaya zaidi sasa hivi ameshikwa na mafua yaani anakoroma mpaka naogopa,naomba unisaidie hapa tafadhali.
 
Mkuu stephot Pole ningelikushauri umpeleke mwanao Hospitali kuan wataalam wa wagonjwa wa watoto wataweza kumsaidia inshallah atapona.
 
habari za sikukuu wana mmu? my hope that you are all good!

jamani nisiwachoshe,

kama kichwa kinavyojieleza, hiyo ni habari ambayo mama mmoja anailalamikia kwamba mume wake anayo kwa muda

mrefu sana sasa. yani anashindwa kulala usiku pale mume wake anapoanza kukoroma, na ukweli ni kwamba, kwa jinsi

anavyosema, hata mtu akiwa nje, anaweza kumsikia kabisa mume wake akiwa katika kukoroma. je, tatizo hili

linasababishwa na nini na dawa yake hasa ni nini wakuu?

jamani mimi nimeshindwa kumpa ushauri katika hili tatizo kwa sababu sina ujuzi nalo.

wana mmu, nina imani kwamba mtatoa mwanga juu ya hili tatizo! nina imani kwamba nitapata majibu mema!

heri ya sikukuu ya christmas na mwaka mpya!

1510782_562996287118165_853570530_n.jpg
 
ila niliwahi kusikia wazee wakisema kwamba mtu akikoroma muite kwa jina ambalo silo lake. mfano kama anaitwa juma unaweza muita joseph kama akiitika basi hata koroma tena(imani za kijadi hizo) sijawahi jaribu
 
mmh..

mtu anapokuwa usingizini najua kwa asilimia fulani anakuwa hajitambui.

that means, ukimuita tu hata kwa jina lolote ataitika tu.

btw, thank you, tutajaribu!
 
haa haa haaa hiyo ni kiimana zaidi. bila kuamini hakuna kupona
mmh..

mtu anapokuwa usingizini najua kwa asilimia fulani anakuwa hajitambui.

that means, ukimuita tu hata kwa jina lolote ataitika tu.

btw, thank you, tutajaribu!
 
kama anatumia mto mwambie aache,asile chakula kingi wakati wa usiku kabla ya kulala,awe anakunywa maji mengi kila siku,kama ni mnene au mzito kupita kiasi-basing on body mass index BMI ambayo ni uwiano wa urefu wake na uzito wa mwili- afanye mazoezi akae kwenye BMI inayotakiwa,asilimia kubwa wenye body mass index kubwa wana tatizo la kukoroma. Afanye hayo ila kama atakua bado amuone daktari atamsaidia.
 
ahsante sana mpendwa!!

you have shown me some way!
 
Lakini Kama mtu wako Kama mumeo mwanzo kero lakini mwisho unamzowea,na ukimkosa usingizi huupati....
 
mwambie ampe njiti ya kiberiti aing'ate kama wavuta sigara. hatakoroma, ila hiyo si dawa ya kutibu, ni kwa kuzuia tu palepale.
 
Back
Top Bottom