Kukoroma usingizini: Fahamu chanzo na tiba yake

Kukoroma usingizini: Fahamu chanzo na tiba yake

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati.

Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi?

Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile:

• Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma.

• Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma.

• Kuwa na misuli minene ya koo. Hii ni kwa wale watu wanene ambao hata nyama zao za koo pia hunenepa na kupanuka na suala hilo husababisha kukoroma, Pia watoto wenye tonsesi kubwa na adenoids baadhi ya wakati hukoroma.

• Kuwa na kilimi kikubwa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha kukoroma. Kilimi kirefu kinaweza kuzuia koo na pale kinapotikisika wakati hewa inapita kwa msukumo husababisha kukoroma.

• Sababu nyinginezo zinazoweza kumsababishia mtu akorome anapolala ni kuwa na umri mkubwa au uzee, imeshuhudiwa kuwa watu wa makamo na wazee hukoroma, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri

unayoongezeka. Vilevile wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake. Kukoroma pia kunaweza kuwa ni tatizo la kurithi. Pombe, kuvuta sigara na

matumizi ya baadhi ya dawa pia husababisha misuli ya koo ilegee na hivyo hupelekea mtu akorome. Kulala vibaya pia husababisha kukoroka kama vile kulala kichalichali, kwani hufanya nyama za koo zilegee na kuziba hewa.

Je, Dawa ya kukoroma ni nini?

Swali hilo limeuliwa sana na mimi katika kulijibu ningependa kusema kuwa, kujua sababu inayosababisha mtu akorome na kuitatua au kuiondoa sababu hiyo ndiko kunakotibu kukoroma. Sote tunajua adha inayotokana na kukoroma, na sauti hiyo

inavyosumbua hasa iwapo anayekoroma ni mtu wako wa karibu kama vile mumeo, mwenzi wako au yoyote yule inayekubidi ulale naye karibu au katika kitanda kimojana hata chumba kimoja. Kukoroma pia huathiri usingizi wa mkoromaji kwani anayekoroka humbidi aamke mara kadhaa usingizini akijua au bila kujua kutokana njia zake za hewa kufunga kwa sekunde

kadhaa ambapo usingizi pia hukatika. Wanaokoroma pia hushindwa kulala vizuri suala linalopelekea asubuhi wawe wamechoka na kutofanya majukumu yao vyema, na pia wale wanaolala nao karibu hupatwa na matatizo kama hayo. Vilevile tunapaswa kujua kuwa kukoroma kuna athari za kiafya za muda mrefu kwa mtu anayekoroma hivyo si jambo la kufanyia mzaha na ni tatizo ambalo linapaswa kushughulikiwa na kutatuliwa.

Wataalamu wanatuambia kuwa ili kujua kukoroma kwako kunasababishwa na nini ni bora ushirikiane na mwenzi wako au yoyote unayelala naye ili akuchunguze pale unapolala na kujua jinsi mwili wako unavyokuwa pale unapokoroma. Ni bora aandae orodha na kuchunguza yafuatayo:

1. Kufunga mdomo na kukoroma kunaonyesha kuwa kuna matatizo ya ulimi.
2. Kufungua mdomo na kukoroma kunaonyesha unaweza kuwa na tatizo katika misuli au nyama za koo.
3. Kukoroma unapolala kichalichali kunaonyesha kuwa pengine kwa kubadilisha namna unavyolala kukoroma nako kunaweza kwisha.
4. Kukoroma wakati unapolala kwa kila mlalo kunaonyesha kwamba tatizo lako ni kubwa na pengine kunahitajia tiba kubwa zaidi.

Iwapo umebadilisha namna unavyolala na haikusaidia, unashauriwa ujaribu yafuatayo:
 Punguza uzito
 Safisha njia yako ya hewa. Kuwa na pua iliyoziba hufanya kupumua kuwe kugumu na kusababisha kukoroma. Unaweza

kufanya hivyo kwa kutumia dawa za kusaidia kupumua kwa urahisi (nasal decongestants) zinazopatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa.
 Wacha kuvuta sigara.
 Lala mapema na pata usingizi wa kutosha kila mara huku ukijiepusha na kuchoka sana. Kunyanyua kichwa kwa nchi 4 huweza kupunguza kasi ya kupumua na kusaidia ulimi na taya kwenda mbele hali ambayo hupunguza kukoroma. Fanya hilo kwa tumia mito maalum ya kupunguza kukoroma au lala bila mto.

Wataalamu pia wanasema kwamba unaweza kupunguza kukoroma kwa kutokula baadhi ya vyakula au dawa kabla ya kulala ambavyo huongeza kukoroma. Vitu hivyo ni kama vile
o Kutokula mlo mkubwa kabla ya kulala.
o Kutokula vyakula vinavyotokana na maziwa au maziwa ya soya.
o Kutokunywa pombe kabla ya kulala.
o Kutotumia dawa aina ya antihistamines.
o Kutotumia vyakula au vinjwaji venye kafeini.

Vilevile wanaokoroma wanashauriwa kufanya mazoezi ya koo ambayo ni pamoja na kuimba, kusoma kwa kurudia rudia voweli (a,e,i,o,u) kwa nguvu kwa dakika tatu mara kadhaa kwa siku, kuweka ncha ya ulimi chini ya meno ya mbele na

kurudisha ulimi nyuma kwa dakika 3 kila siku au huku mdomo ukiwa wazi pelekea taya yako upande wa kulia na wacha ibakie katika hali hiyo kwa sekunde 30. Huku mdomo ukiwa wazi, kaza misuli ya nyuma ya koo na rudia kitendo hicho kwa sekunde thelathini. Unaweza kutizama kwenye kioo na kuona jinsi kilimi kinavyokwenda juu na chini.

Iwapo kukoroma hakutoisha kwa kutumia njia hizo tofauti zilizoelezwa, usife moyo jaribu kumuona daktari na akupe ushauri wa kitiba kuhusiana na tatizo hilo. Madakatari wataalamu wa magonjwa ya pua, masikio na koo au ENT wanaweza

kukusaidia zaidi kutatua tatizo hilo. Siku hizi kuna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa mahospitalini ili kuondoa kukoroma kama vile kifaa kinachowekwa kwenye meno, CPAP, kidude kinachowekwa mdomoni au hata kufanyiwa operesheni ili kuondoa tatizo hilo.

hope itakuwa msaada kwako na wengine nimeipata baada ya kugoogle


source: mziziMkavu https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/187812-dawa-ya-kukoroma.html
 
Au tumia Dawa hii itakusaidia Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma

na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.
 
mzizi mkavu mie nakoroma ara chache na mara nyingi wakati wa kulala nimekuwa nikihisi kimeo kujisogeza karibu na njia ya hewa amabapo nikipumua na hisi muwambo flani wa sauti kwa mbali...........jee hii na yo unaielezeaje?
 
Baby wangu nae ana tatizo hili, mzizimkavu umenisaidia, nitajaribu kumwambia afanye hayo mazoezi
 
Au tumia Dawa hii itakusaidia Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma

na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.

asante sana dr.kwa maelezo mazuri.nimekupata..i will work on them
 
Za kwenu,wandugu,nina katatizo kangu kadogo katika home theatre hasa speaker kubwa ya subwoofer,baada ya kuwaka kama dkk 2 hivi inaanza kukoroma kama vile inataka kupiga shoti,nimejaribu kufungua mara kadhaa,ila hamna wire iliyo loose,nimebadilisha plug,hadi socket lakini wapi,bado tu inakoroma,tafadhali mnisaidie,na mimi nifurahie xmass na kelele kidogo.
 
kwa suala hilo linasumbua sana subwoofer zilizo na channel 2.1 kama inaspecification hiyo kuna kifaa kimoja ambacho wale mafund wazur wanacho hasa kwa masupplier wakubwa wa elektronik ndo wanavyo ni kwa ajil ya kupima tech.parameter zote na systems if ukipata pesa nyingine jitahid uchek channel 5.1 kama kuna more tuma uz mwingine...acha kuonganisha na deki ambayo ina self powered amplifier kwan unadistabo kapasit.
 
Hopefully, wewe ni fundi ktk mambo hayo maana umekuwa ukiifungua mara kadhaa. If so jaribu njia hiyo aliosema mwenzetu hapo juu uone kama itasaidia. Ila kama sio fundi, mimi nakushauri uwatafute mafundi wanaoaminika wakusaidie. Inaweza kuwa tatizo hata sio kubwa kivile.

Mimi yangu ilikuwa na tatizo la kupiga vizuri ninapoiwasha ila baada ya muda inakata kibes ikawa inalia kwenye vispika vidogo tu, nilipeleka kwa fundi akarekebisha, mpaka sasa ni mwaka sasa haijasumbua tena.
 
tumia mingo atleast zinadum dum ...kwa sasa kariakoo zinauzwa kwenye 75000 lakini pia hiyo ni 2.1 channel
 
Ahsanteni,je hicho kifaa kinaitwaje? Na je ukitumia laptop ina effect yoyote
 
Binafsi nachukia sana kuwa chumba kimoja na mtu anayekoroma akilala, Karibuni kila nikilala na mtu chumba kimoja, analalamika kuwa mi nakoroma sana. Nini hasa sababu ya kukoroma usingizini?
 
Matatizo yanayosababisha mtu kukoroma wakati wa kulala ni mengi lakini hasa usababishwa zaidi na matatizo yanayohusiana na mfumo wa hewa, je huwa unastuka pindi unapolala?
 
Asante sana bwana Mzizi Mkavu.Nami ni mmoja wa nabingwa wa kukoroma nitayafanyia kazi maelekezi yako na nitatoa maelekezo yake hapa kwa faida ya wengine.
 
FOREIGN BODY;PIA nilitaka kusahau.,,.jamaa alikuwa ameoa,na waliishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili.Mama alilijua tatizo za mumewe na alilivumilia. kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo mama uvumilivu ilipozidi kumshinda,kwani aligundua kuwa mkoromo wa mumewe ni sawa na mtu anayepuliza filimbi sauti ambayo sio kawaida ukilinganisha na ya mikoromo mingine.
Hivyo akaamua kumrekodi bila kumpa taarifa.Baadaye wakiwa kwenye hali ya utulivu ndipo akampa taarifa na kumuwekea ile sauti.

jamaa kusikia hali ilivyo akakosa raha kabisa,.na kuamua kutafuta tiba ya tatizo.Alipokuja kwetu,tukaoda X-ray kwanza.Picha ya kifua mapaka usawa wa koo .Picha ilipotoka ilionekana kuwa na kimvuli cha duara juu ya shingo. Nilipoenda kuitoa ilikuwa ni shilingi yenye mwengei likuwa imegeuka rangi na kuwa ya kijani.
Jamaa alipoamka na kupatiwa hiyo shilingi yake ,ndipo kumbukumbu zikamjia kuwa alipokuwa mtoto aliweka shilingi mdomonina aliimeza bahati mbaya.
aliporipoti tukio kwa wazazi wake,wakamwambia kuwa itatoka kwa njia ya haja kubwa hivyo asiwe na wasi wasi. tangu siku aliyoumeza huo mwenge mpaka siku aliyoripoti tukio,hakuwahi kuwa na matatizo ya ziada,si kwenye kifua wala kupumua.
Shilingi ilitolewa miaka 25 baada ya kuimeza,na tangu ilipotolewa ndio ikawa mwisho wake wa kukoroma.


hahahahahahaha hii post ni gossip ila ni nzuri inapunguza stress baada ya kuambiwa kukoroma huenda ikawa ni ngoma na mwana JF Bawa Mwamba hapo kati
 
Wadau mimi nina tatizo linaloni-boa sana la kukoroma,nimejaribu kulala milalo ya kila aina lakini ninaambiwa kuwa bado nakoroma,nafuu yangu ni pale ninapolalia tumbo ndio sipati hilo tatizo,sina uzito mkubwa sana kwani nafanya sana mazoezi na nimejaza kimazoezi kwa hiyo kwa swala la weight sina wasiwasi.Tujuzane wanajamii kama kuna dawa ili niepukane na hili.
 
fanya zoezi la kutoa ulimi nje kwa mde mrefu (stretch ur tongue to the max as long as u can) mpaka uchoke\
Hii inasaidia kulegeza misuli iliyopo kwenye kinywa inayosababisha ukorome. Huna haja ya kutumia dawa.

If this works Mshukuru Mwenyezi mungu kwa kutupa uzima na afya
 
fanya zoezi la kutoa ulimi nje kwa mde mrefu (stretch ur tongue to the max as long as u can) mpaka uchoke\
Hii inasaidia kulegeza misuli iliyopo kwenye kinywa inayosababisha ukorome. Huna haja ya kutumia dawa.

If this works Mshukuru Mwenyezi mungu kwa kutupa uzima na afya

Will try that
 
Back
Top Bottom