Kukoroma usingizini: Fahamu chanzo na tiba yake

Kukoroma usingizini: Fahamu chanzo na tiba yake

kuna watu wanakoroma kama simba na vyura na mashine ya kuranda mbao pamoja, khah!

hahahaha usinikumbushe we kuna day nlikwenda msiban basi ucku kulikuwa kama kuna mashindano ya kukoroma.nilishangaa sana
 
Farkhina, umenifanya niangue kicheko! Niliwahi kupata mgeni nyumbani wakati sipo. Mkwe wangu (mume wa mpwa wangu). Next day nampigia maid namuuliza kama mgeni yuko comfortable, akanijibu 'he is comfortable ila anakoroma!' Bedrooms zao zilikuwa mbali. Hadi leo nikimuona mkwe wangu najichekelesha tu!
 
umeona eee?
 
Sasa baba Mtambuzi, kama mke na mume wote wanakoroma ina maana ndoa inakuwa salama zaidi?
 
Last edited by a moderator:
Hii nimeiba kuleeee!
NAMNA YA KUMALIZA TATIZO LA KUKOROMA
Habari za kazi mheshimiwa Michuzi,nilipitia hapa kwenye blog yako nikakuta bwana Chumaka wa Korogwe akiomba msaada wa namna ya kutatua tatizo lake la kukoroma ambalo linamnyima mkewe usingizi.Majibu mengine niliyoyasoma yalikua ya ajabu na pia hayakuweza kumsaidia bwana Chumaka.Na vifaa vingi vilivozungumzwa kwa mtu aliyopo Korogwe sidhani angevipata kwa urahisi. Kwakua kulikua na comments zaidi ya 35 nikahisi nikiweka na yangu pale wengi hawataiona,naomba uiweke peke yake ili iweze kusaidia watu kama mimi ilivyonisaidia.Niliwahi kusafiri na mzee wa kijapani kwenda mikoani kikazi na katika safari zetu kuna siku ilibidi tulale kwenye mji mdogo ambao tulikosa vyumba na kupata kimoja tu ambacho kilikua na vitanda viwili.Watu wengi walishaniambia kuwa nakoroma sana nilalapo usiku.Siku ya pili tulipokua tunapata kifungua kinywa yule mzee akaniambia nina tatizo la kukoroma na atanifundisha namna ya kulitatua bila kutumia dawa,mbinu ambayo wanaitumia kwao.Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma.Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.Mzee huyu aliniambia mtu anaekoroma mwili wake haupati mapumziko ya kutosha na mara nyingi huamka huku bado akihisi uchovu na husababisha watu wengine kunenepa sana na wengine kukonda ikitegemea mwili wa muhusika na homoni zake. Tatizo langu liliisha kabisa baada ya wiki 2 lakini naendelea na mazoezi hata mara mbili kwa wiki ili misuli isilegee tena.Kwakua naishi peke yangu ilibidi nimchukue waifu wa siku 2-3 anihakikishie sikoromi kabisa.Nikiamka siku hizi sihisi uchovu ule wa zamani.Mdau Ibrahim,D'salaam.

Ushauri huu nimeupenda sana, nitafanya hivyo mara kwa mara nione nini kitatokea naamini tatizo langu litaisha wife wangu huniambia hili lkn sikuwa na jibu lkn naamini muarobaini umepatikana.
Asante kwa somo hili.
 
Sasa baba Mtambuzi, kama mke na mume wote wanakoroma ina maana ndoa inakuwa salama zaidi?

hapo mke atavuta khaaaaaaaaaammmmmmmmmmsssssssssiiiiiinnnnnnnnn kwa sauti ya 3 na mme atavuta MMMMMMMMMIIIIIIIIIIIIIIIIIIAAAAAAAAAAA kwa sauti ya nne.
 
Kuna jamaa mmoja alishikwa ugoni kwa ajili ya kukoroma kwani alikuwa akiunguruma utafikiri simba.
 
dah kumbe ndoa yangu ipo mashakani naombeni wadau mnisaidie dawa niondokane na hilo pepo linalonyemelea ndoa yangu manake huyu mzee anakoroma kama anapuliza tarumbeta wakati ni usiku.
 
dah kumbe ndoa yangu ipo mashakani naombeni wadau mnisaidie dawa niondokane na hilo pepo linalonyemelea ndoa yangu manake huyu mzee anakoroma kama anapuliza tarumbeta wakati ni usiku.
Asnam halafu wewe unatafutwa...........LOL
 
Last edited by a moderator:
kwa kweli kulala na mkoromaji ni ngumu mno! kha! kuna watu wanakoroma kama generator aaarrrggg, kwakweli yakera! babu Mtambuzi heshima yako!
 
Last edited by a moderator:
Wanajamii, naombeni msaada juu ya tendo hili la kukoroma. Nini sababu za kukoroma wakati wa kulala na nini kifanyike ili mtu aache kukoroma awapo usingizini. AHSANTENI
 
Wanajamii, naombeni msaada juu ya tendo hili la kukoroma. Nini sababu za kukoroma wakati wa kulala na nini kifanyike ili mtu aache kukoroma awapo usingizini. AHSANTENI

Nami pia nauliza kwani kwa kawaida huwa sikoromi, ila ninapokuwa na ujauzito basi huo ndio mpango mzima sijui kuna siri gani hapo, twaomba wataalam mtuelimishe.
 
Back
Top Bottom