Kulalamika tumeibiwa kura za kwenye mabegi huku hamuendi Mahakamani, tuwaeleweje?


We kilaza rudi shule ukajifunze kuandika. Sasa hivi elimu ni bure, na madarasa wezi wa kura wamesema wataongeza 1,000.
 
Nani apoteze muda wake kwenda mahakamani?
Tunasubiri meko atoke
Madarakani mahamaka iwe huru ndio tukadai haki yetu.
Its not over.
Wewe endelea kukejeli tu
 
Nakumbuka upinzani wa enzi za kina Lamwai (rip) walikuwa hawatoi visingizio kama mnavyotoa sasa hivi, walikuwa wanabwaga watu mahakamani ile mbaya. Sasa hivi chadema imebakiza porojo tu

Wakati huo wa kina Lamwai uliwahi kumuona rais akiwa na majaji na mahakimu hadharani akiwatishia kuwa ana taarifa zao zote? Uliwahi kusikia marais wa wakati huo wakiwaagiza majaji waendesha kesi haraka ili hizo fine awape waendeshee shughuli za mahakama? Usichanganye nyakati hizo kukiwa na marais waliokuwa wanajua cheo ni dhamana, na hawa walevi wa madaraka wanaohisi urais ni uungu.
 
Mbona Wassira alishendwa na Ester Bulaya mahakamani?
Wakati ule mahakama ilikuwa bado ina majaji wenye taaluma walioteuliwa na Kikwete na Mkaoa. Huyu wa sasa anawateua makada wa CCM kuwa majaji. Anawateua makada wa CCM kuwa wakurugenzi. Kila mahali anawajaza makada, tena wale makada wenye akili ndogo, ambao wana uwezo wa kusifia kila jambo analolifanya yeye.

Hakuna mwenye akili anayeweza kupoteza muda kufungua kesi ya uchaguzi kwenye hizi mahakama bandia zinazosimamiwa na Juma ambaye anapokea maagizo toka kwa Bashiru na Polepole.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka upinzani wa enzi za kina Lamwai (rip) walikuwa hawatoi visingizio kama mnavyotoa sasa hivi, walikuwa wanabwaga watu mahakamani ile mbaya. Sasa hivi chadema imebakiza porojo tu
Jaji mkuu alikuwa nani wakati ule ?
 
Kama kuna jambo ambalo halininyimi raha ni Chadema ya Mbowe kutiwa adabu na Polepole. Mbowe alijisahau sana na kujiona yeye ndiye mpiga kura pekee na mwenye uchungu kuliko watanzania wote. Kumbe bagi alizovuta miaka ya 80 bado iko kichwani.

Hua namshangaa sana na Lisu.
Bado hajajitambua kuwa yeye ni Mtanzania anayetaka kupata kura za watanzania. Bado anasiasa za matukio. Bado ana siasa za kuongea ongea tu . Sio kila jambo mtu anatakiwa kulirukia na kuliongelea. Kuna mambo mtu anapaswa kuyakwepa na kukaa kimya. Chadema haitakuja kuinuka tena chini ya Mbowe na siasa za kuropoka ropoka bila ushahidi.
Na Mbowe kamwe hatakuja tena kupata Ubunge. Ujinga walioufanya kule bungeni umewafanya watanzania waachane na Mambo ya upinzani.

Haiwezekani majimbo yote nchi pasiwe na jimbo hata moja ambalo kuna fact za kutosha kwenda mahakamani. Vinginevyo hicho chama hakina maana yoyote ya kuwa na viongozi.

Yani Mwenyekiti Mhuni Mbowe anaudanganya ulimwengu kuwa Mahakama hazitendi haki lakini wakati huo huo wanawapeleka Viongozi wenzao wa Chadema walioteuliwa kwa nafasi maalumu za wanawake.
Mbowe na wahuni wenzake withamekimbilia mahakamani kwa Chadema wenzao na kuwaacha CCM halafu kuna wapambe bado tu hawaelewi mradi wa Mbowe ni kuua upinzani nchi.
 
Mimi nadhani Chadema wamestuka kuwa wakienda tu Mahakamani watapewa ushindi wa ubunge katika maeneo kadhaa ili kosa la kutokuwa na upinzani lifunikwe. Watu kama Askofu wa Birmingham wanaweza kutolewa kafara. Aidha kuna vijana wanaweza kulamba ubunge wakijua tu kuwa mbeleni wataunga juhudi. Inaelekea CDM wamewastukia.

Ningekuwa mimi ningeshauri TLP na wenzake wakate rufaa ili angalau wapatikane wabunge wa upinzani.

Amandla...
 
Haahaa kwa mahakama zipi? Bora wakalime watavuna kuliko kupeleka kesi za kisiasa zinazoihusu ccm na serikali
 
Mahakama inaendeshwa kwa remote na Meko mwenyewe. Kwa nini wapoteze muda kupeleka kesi ya tumbili kwa nyani?
 
AG yaani Attorney General
DPP yaani Director of Public Prosecution
IGP yaani Inspector General of Police
CJ yaani Chief Justice
JK yaani Judge Kiongozi
Kama hao waliona hakuna wizi wa kura, unadhani kuna mtu mwenye akili timamu kama hao CHADEMA akaenda kufungua kesi
Muda wa siasa umekwisha tuchapeni kazi tujenge nchi tulipe kodi wabunge walipwe vizuri
 
Vile vile, kujichukulia sheria mkononi ni kosa kisheria. Kwa nini hawakuchukuliwa hatua za kisheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…