Kuliko kuajiri mfanyakazi wa ndani tuwe na utaratibu wa kuchukua watoto wa ndugu kwa nia ya kuwaendeleza

Wale watoto walizaliwa mtoni kwa sasa wamerudi mtoni huko maisha safi tu sie ndio tunapambana na bongo yetu
 
Tatizo wanamajungu sana. Wakae huko huko kwao tutatuma tu hizo ada.
 
Wakae tu kwao!
 
Yaani hiyo shida ndio siitaki.
Watoto wangu waache kuangalia movie kwa ajili yake.
Tuendelee na huu utaratibu wa wasichana wa kazi ili tuwe na amani kwenye nyumba zetu!
 
Ukileta kijana pia kuna uwezekano akawapa ujauzito mabinti wako. Ni muhimu kuwaelimisha wote
 
Ukitaka kujitafutia lawama na ugomvi nyumbani kwako chukua mtoto wa ndugu ndio utajua dunia inaelekea wapi.
Ndugu wengi wamefarakana kwasababu ya watoto unakuta mtoto wa mama Mkubwa au wa shangazi kaenda kwa mama mdogo lakini haamki asubuhi wewe umeamka SAA kumi na mbili yeye anaamka SAA,mbili akute umempikia chai na kudeki na bado vikombe mezani ukaondoe wewe mwenyenyumba. Ukimgombesha anapiga simu kwao kwamba unamnyanyasa hata kupika haingii jikoni sasa ukimuachia mtoto ndio kabisa ni mvivu hawezi kukulishia mtoto .

Mkuu nakuambia sio ndugu wote wazuri na ndio maana serikali imewawezesha wadau wengi kufungua vituo vya kulelea watoto wachanga au wadogo yaani Day care center. Kuliko uchukue ndugu aje kukulelea mtoto ni bora umpeleke mtoto Day care ukitoka kazini unampitia unaenda naye nyumbani. Hapo utakuwa na amani hao ndugu wasaidie wakiwa kwao maana ukiwaendekeza ukawaleta warundikane kwako utajuta unaweza kuhisi virusi vipya vya corona vimeingia ndani kwako.
 
Kabla hujamchukua unakaa na wazazi wake pamoja na mhusika unawaelewesha unayotarajia kutoka kwake. Kwanza mtoto mwenye nidhamu hawezi kumuona mkubwa anaosha vyombo wakati yeye amekaa.
 
Kabla hujamchukua unakaa na wazazi wake pamoja na mhusika unawaelewesha unayotarajia kutoka kwake. Kwanza mtoto mwenye nidhamu hawezi kumuona mkubwa anaosha vyombo wakati yeye amekaa.
Watoto wa Siku hizi ni wale waoliozaliwa kichwa chini wakikuchungulia makalio..yaani watoto walivyo utafikiri waliozaliwa wanaona miguu ya mama zao..eti unapanda bodaboda anakutongoza..

Cha ajbu kimoja tu kule
 
Hili ni sawa na kilimo cha WhatsApp!
Tuliojaribu ndugu kama ndugu, hatutarudia huo upuuzi. Majungu na ubaya wote na lawama zote usubirie zikuangukie.
Dharau na vitimbi hapana!

Waje kutembea na kurudi makwao, msaada wataupatia huko makwao.

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…