Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

Vipi wale askari warefu wenye bunduki ni watanzania kweli? Maana hakuna watanzania warefu kama wale
Hakuna watanzania warefu??wewe jamaa kuishi kwako huko milima ya urugulu usidhani ndio umeimaliza tz nzima...nenda kanda ya ziwa ukakutane na milingoti ya watu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ameonekana rais Samia katika safari zake.

Angalia Kilimanjaro Arusha. Barabara yote iligeuka private road na shughuli zote kusimama. Uchumi kiasi gani ulipotea?



Angalia idadi ya magari, watu na madege. Ama kwa hakika yote hii ni pesa na si ndogo ambayo ingeweza kuokolewa bila kupungukiwa na lolote.

Nini umuhimu wa ziara hizi ambazo matumizi yake yangeweza kujenga mashule, madarasa nk tukiachana na mikopo isiyo ya lazima na tozo za miamala na sasa za benki kwa majina ya uzalendo?

Serikali si ipo kote kutokea kwa mtendaji wa kijiji, kata, DC, RC, Mawaziri hadi hao top tatu? TAKUKURU na wasiojulikana wapi wasipokuwapo?

Tuweni wazalendo, ziara za hivi bila kudhibitiwa hazina tija!

Pumzika kwa amani mzalendo #1:

Mwalimu Nyerere aliipenda nchi siyo CCM
 
Ndo maana kaenda fasta kwa wananzengo apewe cheo cha uchifu mkuu, maana chifu mara zote yupo sahihi na hatakiwi kuhojiwa.........
 
Hili swali linawahusu TISS, na kwa bahati mbaya hawawezi kukujibu.

Lakini mkuu hawq walinzi wapo tu hata wqsipomlonda rais wanalipwa, je wakimlinda wewe unakereka nini?

Hoji mambo ya maana achana na huu ushuzi.
Hujui kuna mishahara na posho??
 
Huyu Rais ni "SULUHU" ya wa-Tanzania, ameingia madarakani katika kipindi ambacho wa-Tanzania tayari wameshajeruhiwa, tena vibaya sana. Kwa maoni yangu mimi kama layman, huyu ndiye Rais anayehitaji ulinzi wa hali ya juu na makini zaidi kupita ma-Rais wengine wote, waliopita na watakaofuata baada ya yeye
Mimi nilipata shida kidogo kwenye siku ile alipokuwa anakabidhiwa mwenge, alipoushika ukiwa unawaka moto kwa sekunde kadhaa, huku akiwa peke yake amesimama kwenye kijukwaa/ ngazi! Hata hivyo mambo mengine ni yao wataalamu wenyewe, wao wanajua zaidi
 
Hujui kuna mishahara na posho??
Mkuu, misafara ya viongozi siku zote ina hawa watu, huwa wengine hatuwatambui sababu wako kwa nguo za kiraia, so posho huwa zinaliwa tu.
Pili jinsi posho zinavyotolewa zinachangamsha mzunguko wa pesa mtaani pia
 
Mkuu, misafara ya viongozi siku zote ina hawa watu, huwa wengine hatuwatambui sababu wako kwa nguo za kiraia, so posho huwa zinaliwa tu.
Pili jinsi posho zinavyotolewa zinachangamsha mzunguko wa pesa mtaani pia
Lands nikueleweshe... Wale watu wa usalama unaoona kwenye gwanda na wasio na gwanda kwenye msafara ni mbali na wale walio au wanafanya uchunguxi wa kiusalama kabla hivyo idadi inavyokua kubwa kimtazamo pia hata kimfumo huongezeka... Tunachosema mbona kuna utofauti mkubwa na zamani japo mambo hubadilika lakini mbona kwa ukubwa huu??

Kuhusu kuimarisha uchumi kwa style hii ni kishusha thamani ya shinlingi
 
View attachment 1977510Wale walioko Arusha na viunga vyake leo tumeshuhudia/kuona Mh. Raisi mama Samia Suluhu Hassan kaongezewa ulinzi mara dufu, tofouti na tulivyozoea na msafara wake umekuwa na ulinzi mkali na idadi kubwa ya askari na usalama wa taifa kitengo cha ulinzi.

Pia msafara wake una magari zaidi ya 70 kutoka 20 ya awali kama tulivyokwisha zoea, msafara huu umeambatana na helikopta mbili kama tulivyokuwa tukiona enzi za Hayati John Pombe Magufuli.

Cha kushangaza amekuwa akisisitiza kauli kama ile ya Hayati John Pombe Magufuli ya kwamba “aombewe”, kulikoni?

Je, hii misafara mikubwa sio janja janja ya baadhi ya watumishi wakubwa kujilipa posho kubwa kubwa ilihali, wananchi wanalia maisha magumu katika awamu hii ya sita?

Tujadili.
Yes kumuombea ni muhimu. Anashika dola.Hafurashi kila mtu. Wezi wanataka kupiga 1.3 trillion. Asipojipanga watamzingua
 
Don't live in a lie

JWTZ ndo kila kitu ama ndo Final, hao unaowasema hawana ishu hata kidogo kwa dunia ya sasa, sababu wamekua associated na chama kulicho na dola na in the end wamekosa uadilifu na umakini.
JWTZ unafahamu uhusiano wao na ulinzi wa amiri jeshi? Unafahamu Kwa kiwango gani? Unayafahamu vipi mahusiano yao na hao unaosema hawana ishu? Ni mahusiano ya kiwango gani?
 
Ni noma mkuu,nilihesabu magari,yalikua zaidi ya 50! Siku hizi ana ambulance mbili kwenye msafara wake!
Nimeamini kweli kwamba Watanzania tumekosa kazi ya kufanya,kweli mtu na akili zako unakaa barabarani kuhesabu magari, hiyo nikazi ya watotto wanaojifunza kuhesabu wao hata akipita kwenye mwembe huhesabu hata maembe. Ushageuka mtoto sasa.
 
Pia kuna wale wenye mabunduki ya kivita warefu pua zao zimechongoka kama wanyarwanda, kuishi kwangu Tanzania sijawahi kuona watu warefu kama wale, je ni wa vitego pia ama ni kutoka nchi za jirani? Maana hata huku mtaani hawaonekani kabisa wale watu warefu wenye mabunduki ya kivita
Tanzania inawatu warefu, labda ujatembelea Singida, mikoa ya kända ya ziwa. Na wana pua ndefu. Tusijenge hoja kuwa kila mrefu na pua anatoka kwa jirani.
Usukumani, ujitani, ukuryani, kuna mijitu imeshiba na imepanda hewani.
 
WE UNASHANGAA ULINZI WA MAMA YETU? UNAUFAHAMU ULINZI WA RAIS WA MAREKANI? USHAWAHI KUJIULIZA KUHUSU LILE BRIEFCASE ANAYATEMBEA NAYO? IDADI YA HELICOPTA NA HATA GARI ANALOPANDA RAIS WAO. UNAUFAHAMU MTAMBO WANAOTEMBEA NAO WENYE UWEZO WA KUINGILIA NA KUKATA MAWASILIANO POPOTE ANAPOKUWEPO RAIS WAO? HAYO NI MACHACHE NINAYOYAJUA MIMI? SIYO MPK MAMA YETU YAMKUTE MAJANGA NDIPO TUIMARISHE MIFUMO YA ULINZI KWA RAIS WETU.TUMIA AKILI KTK KUFIKIRI, USITUMIE MATA_O KAMA KICHWA CHAKO
 
Ukiona hivi tunakuwa na mashaka basi kuna kaukweli mama alitembeza sumu kwa mtangulizi wake coz watu wakilalamika kuhusu sumu ndipo ulinzi ulipoongezeka??!!kuna namna hapa
 
Kuna hela ieseeeh hii nchi inayo helaaa
1. Tozo na Kodi kibao zinaingiza hela
2.Tumechukua juzi mkomo IMF hizo zote ni hela
 
Back
Top Bottom