Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

View attachment 1977510Wale walioko Arusha na viunga vyake leo tumeshuhudia/kuona Mh. Raisi mama Samia Suluhu Hassan kaongezewa ulinzi mara dufu, tofouti na tulivyozoea na msafara wake umekuwa na ulinzi mkali na idadi kubwa ya askari na usalama wa taifa kitengo cha ulinzi.

Pia msafara wake una magari zaidi ya 70 kutoka 20 ya awali kama tulivyokwisha zoea, msafara huu umeambatana na helikopta mbili kama tulivyokuwa tukiona enzi za Hayati John Pombe Magufuli.

Cha kushangaza amekuwa akisisitiza kauli kama ile ya Hayati John Pombe Magufuli ya kwamba “aombewe”, kulikoni?

Je, hii misafara mikubwa sio janja janja ya baadhi ya watumishi wakubwa kujilipa posho kubwa kubwa ilihali, wananchi wanalia maisha magumu katika awamu hii ya sita?

Tujadili.
Nchi ni lazima imlinde kwa nguvu zote AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA....

Dunia imebadilika sana.....

Maadui ni wengi mno.....

SIEMPRE JMT
 
Nchi ni lazima imlinde kwa nguvu zote AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA....

Dunia imebadilika sana.....

Maadui ni wengi mno.....

SIEMPRE JMT
Sawa sawa, je kuna tishio la kiusalama kwa mama yetu, maana mabadiliko ya ulinzi wake imekuwa ghafla mbona mwanzo hakuwa na walinzi wengi kiasi hiki?
 
Hapa inaleta mantiki kidogo kwa ninavyo watambua watanzania sidhani kama wana uthubutu wa kumshambulia kiongozi yoyote mkubwa, huwenda hawa wanajiongeza ili kupiga pesa. Asante kwa maelezo yako boss
Hana makuu hofu ya nn,ulinzi pekee ni kuwatendea watu mema.
Mwingi na JK hata kariakoo wanaweza katiza salama kabisa bila hata mlinzi, sababu waliwekeza kwenye wema
 
Ameshajua kuna kundi flani lina mind sana! Kumbuka siku ana waapisha wale majaji na wateule wengine,alisema anapotengua watu,sio anawatengua sababu ya kabila lao, anatengua sababu ya kushindwa kwao kazi! Sasa hii kauli ni nzito sana kutolewa na head of the State! Ukute Pamba FC, wame mind sana watu wao kuliwa vichwa!
acha kupotosha,hata jpm mbona alikuwa Mara kadhaa akisema MNIOMBEE!!??,mbona hukusema ni kundi flani linamuandama jpm,pumbavu ...,samia huenda kwa Sasa amegundua ikulu sio pa mchezo Panahitaji moyo wa chuma na ujasiri wa kutosha. huwezi kukosa maadui ,Wala huwez kukosa marafiki,lakini pia ikulu usimwamini mtu hata Kama ni mkeo au mumeo.muda wowote mtu wako wa karibu unayemwamini anaweza kuwa adui yako !!!
 
Itakuwa anaogopa mishalena mikuki ya Wamasai...

Unampeleka Morani wetu jela miaka 30? Na kama hiyo hamjaridhika, mnatuambia eti bado ana kesi zingine!!
 
Back
Top Bottom