Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

Kuna tishio gani Tanzania hadi kuwe na ule Ulinzi?? Kipindi cha Jakaya akiwa President uliwahi ona msafara wake ukiwa kama huu wa Magu au Samiya??
Wa Magufuli naona ulikuwa na uafadhali maana nakumbuka hata helikopita ilikuwa ni moja ila huu wa mama una helikopita zaidi ya mbili.

Sijajua kwanini wanafanya aerial surveillance huu ulinzi unastajabisha kwa kweli?
 
Hiki kikosi kumbe ni maalamu kipo chini ya Mh. Rais ama wapi? Maana katika kumbukumbu zangu sijawahi ona combat za namna ile hata vimo vyao ni tofouti na hawa askari wetu wa kawaida ama ni kikosi maalamu ambacho hata ajira zao zinakuwa za siri tofouti na majeshi yetu na basement yao itakuwa wapi?
Nakujibu kiufupi ,,,raisi ana kikosi cha ulinzi cha idara ya usalama WA Taifa ......wao ndo wanajua aishi vip
 
Kuna tishio gani Tanzania hadi kuwe na ule Ulinzi?? Kipindi cha Jakaya akiwa President uliwahi ona msafara wake ukiwa kama huu wa Magu au Samiya??
Jeshi linalomlinda samia ndilo jeshi lililomlinda JK. PsU

Raisi hajipangii walinzi, yeye ni mwanasiasa na kiongozi.
 
Una habari kama Jakaya ndiyo alikua anapata attempt nyingi sana?? Gari ya Jakaya aliyokua kapanda iliwahi chomoka tairi,sema ilikua ndiyo imefika eneo la tukio!

Gari aliyokua kapanda Jakaya,iliwahi kataa kuchange gear,hadi wakamshusha akapanda gari nyingine,tena hii ilikua Mbezi kama sijakosea!

Jakaya akiwa Bunda au Tarime,kuna askari mmoja aliupoteza msafara wa Jakaya! Je baada ya hizo mishe uliona wapi msafara wake ukiwa na heavy and tights security??
Hapa sasa umenikaribisha kwenye hadithi za vijiweni. Leta story maisha yaendelee.
 
Watanzania unawatambua unaishi nao wote? Nchi unaiona imetulia sababu ya hao hao wanaoamua ulinzi wa raisi uwe wa kiwango gani.
Kwa hiyo wakiamua kupunguza huo ulinzi kwake pia ni sawa?
 
Anafuata slogan ya;
"Dont trust anyone even your shadow escape it during the sunset"
 
Swali uliloliuliza ni la msingi na Kwa bahati mbaya hatuezi kujibiwa ,wakiamua kufanya hivyo wao ndo wanajua ,,,,1,sababu 2.ilikuwaje 3 ,nini kifanyike 4.na lini kifanyike ,5 Kwa nini kifanyike......Kiufupi nchi inafanyiwa tathimini na idara ya usalama WA Taifa Kwa hyoo. Kimsingi tuwaamini tuuu
Asante kwa maelezo mazuri boss
 
Kwa hiyo wakiamua kupunguza huo ulinzi kwake pia ni sawa?
Ni sahihi. Yeye ni mwanasiasa na kiongozi, hawezi jipangia ulinzi wake mwenyewe uweje. Kuna wataalam. Ni sawa na kusema daktari ajifanyie operation, haiwezekani.
 
Raisi wa nchi hajipangii ulinzi. Nchi ina taratibu zake za kumlinda kiongozi wake.
Huwa wanasema kauli ya Rais ni amri ikitokea akisema haitaji ulinzi mkubwa kama huu wa leo je? hao wanaopanga ulinzi watakubaliana nae ama watakataa?
 
Nakujibu kiufupi ,,,raisi ana kikosi cha ulinzi cha idara ya usalama WA Taifa ......wao ndo wanajua aishi vip
Hao wanajeshi weusi na warefu ni sehemu ya kikosi hicho?
 
Huwa wanasema kauli ya Rais ni amri ikitokea akisema haitaji ulinzi mkubwa kama huu wa leo je? hao wanaopanga ulinzi watakubaliana nae ama watakataa?
Kauli ya raisi ni amri anapotoa maagizo ya kisiasa na kiutawala yanayohusu nchi na si ulinzi wake au afya yake. Kama ilivyo kwa kauli ya daktari kwa mgonjwa wake, daktari hawezi agiza manesi wamletee visu ili ajifanyie operation.
 
Wapuuzi hawa wanapiga kodi na tozo zetu kupitia mambo ya hovyo
 
Una habari kama Jakaya ndiyo alikua anapata attempt nyingi sana?? Gari ya Jakaya aliyokua kapanda iliwahi chomoka tairi,sema ilikua ndiyo imefika eneo la tukio!

Gari aliyokua kapanda Jakaya,iliwahi kataa kuchange gear,hadi wakamshusha akapanda gari nyingine,tena hii ilikua Mbezi kama sijakosea!

Jakaya akiwa Bunda au Tarime,kuna askari mmoja aliupoteza msafara wa Jakaya! Je baada ya hizo mishe uliona wapi msafara wake ukiwa na heavy and tights security??
Hii ilikuwa zaidi ya hatari hao waliokuwepo walisalia katika nafasi zao ama walivuliwa wote maana kupoteza msafari si tukio dogo hata kidogo?
 
Jeshi linalomlinda samia ndilo jeshi lililomlinda JK. PsU

Raisi hajipangii walinzi, yeye ni mwanasiasa na kiongozi.
Hii PSU iko wapi? Na hao wanajeshi ni sehemu ya hiyo psu
 
Huwezi jua! Fuatilia ndiyo utajua! Na huyo askari alijipiga risasi,sasa elewa alijipigaje risasi akiwa ndani ya mahabusu, sijui mahabusu hua wanaruhusiwa kuingia na bunduki ndani!!
Halafu ikawaje baada ya risasi sasa? Mm hayo sijui ndo nakusikiliza hapa. Leta story mwana.
 
Back
Top Bottom