Kulikuwa na uhalali gani kwa Chief Mkwawa kutambulika kama 'Shujaa?

Mpaka sasa bado dunia haijui Hitler alitowekaje duniani. Kuna wanaodai aidha USA au USSR kuna mmoja aliwahi kumkamata kisha akamficha...
Kaka tafadhali anza kusoma vitabu vya historia! Hitler alijiua. Taarifa ya askari waliokuwepo ziko.
Alijiua mnamo 30 Aprili 1945 saa tisa na nusu alasiri; alikaa kwenye handaki iliyoimarishwa chini ya ikulu yake mjini Berlin. Wakati ule jeshi jekundi (Warusi) waliwahi kuingia Berlin tayari walikuwa takriban mita 200-300 ilhali mapigano yaliendelea. Asubuhi ya 30 Aprili aliwaruhusu wote ambao bado walikuwa naye kwenye handaki waweze kuondoka. Yeye alijifunga ndani ya chumba kimoja pamoja na Eva Braun (aliyemwoa tar 29 Aprili). Baada ya kusikia mlio wa bastola askari 3 waliingia katika chumba wakakuta maiti za Hitler na Braun ; Braun alikuwa amemeza sumu, Hitler alijiua kwa bastola yake ya modeli Walther PPK 7.65. Afisa wa SS Otto Günsche alimkuta, alinuka harufu ya sumu kwa Braun akaona damu kweny ekichwa cha Hitler. Jinsi alivyoambiwa kabla ya tendo hili, alipeleka maiti nje akawatupa katika shimo kwenye bustani (kreta kutokana na mlipuko wa bomu iliyowahi kuanguka pale) akaagiza maiti yamwagwe mafuta na kuchomwa. Kundi la watu zaidi ya 8 ambao bado walikuwa wamebaki kwenye handaki walitazama.
Soma yote na historia ya masalia yake (yalikusanywa, kufanyiwa utafiti, kufichwa na jeshi la Kirusi hadi 1970, mwishoni mifupa yalisagwa na kutupwa kwenye mto Biederitz, pale Ujerumani.

Basi jisomee hapa Death of Adolf Hitler lakini usilalamike tena ni mengi. Ni hitimisho fupi, kuna vitabu vingi juu ya swali hilo.
 
Kamwe Shujaa huwa hajiui. Kwangu wala siyo Shujaa, ila nikiambiwa Watu kama akina Tundu Lissu, Mchungaji Msigwa na Freeman Mbowe ni Mashujaa nitakubali na Kuamini upesi mno.
 
Za chini ya kapeti zinadai Mkwawa alidedishwa na Mjerumani kwa kukatwa kichwa, ili kutunza hadhi ndio wakadai kajiua
Kwa hiyo kwa mawazo yako, nani aliyeweka kumbukumbu? Ikiwa ni wajerumani wakachukua uwongo wa waafrika wakautunza?????
 
Gadaffi pia alikuwa na teknolojia duni mbele ya NATO. Wahehe walikuwa empire ndani ya taifa gani?
 
Unapajua Kalenga na Tosamaganga wajeruman walijipanga zaida ya Mara mbili kuuweza mtiti wa Mkwawa wa leo hata mabomu ya machozi huwezi himili halafu unauliza ushujaa wa Mkwawa
wabishani kama huyu bwana ni wa kupuuza anachobisha kuhusu ushujaa wa mkwawa hata haeleweki sijui alitaka anyongwe kizembe na wajerumani ndio aonekane wa maana?
 
Msiwe mnajiita majina ambayo hamjui maana yake hujui chochote kuhusu kanuni za kivita tena sikutarajia wew kuuliza kitu Kama hichi kujiua n moja ya kanuni za kishujaa ili wanajeshi wako wasione ukiteswa kwa sababu utawavunja moyo
 
Kwa hiyo wale majasusi wanaojiangamiza baada ya kushtukiwa nao siyo mashujaa?

Siyo kweli... nipo tofauti na wewe kwenye hili...
 
Msiwe mnajiita majina ambayo hamjui maana yake hujui chochote kuhusu kanuni za kivita tena sikutarajia wew kuuliza kitu Kama hichi kujiua n moja ya kanuni za kishujaa ili wanajeshi wako wasione ukiteswa kwa sababu utawavunja moyo
Hiyo sababu ni ya uoga na kitoto sana
 
Una maono na hoja nzuri sana ila kwa hili, nikuulize tu inadhani pale kwenye kimfuko kidogo upande wa kushoto wa kombati, ile sumu tunayowekewa pale tuingiapo uwanja wa medani ni ya shoo, au ni ya kujipaka kama urembo na kuingia nayo nyuma ya keyboard za page ya jamii forum kuperuzi, unapozidiwa unalamba sumu unapunguza mengi, kua mateka kusikie tu kwenye muvi za kihindi kijana. Nimesoma tu heading nikaandika aina haja ata ya kusoma main point, askari wote we are born tu die . Mhudumu nigee safari lager kubwa
 
Samahani mkuu Siri gani wakati vikosi vyake vilishindwa?
 
Shujaa wa kihehe unamshusha hivyo.
Subiri Wahehe waanze kujinyonga kisa wewe
 
Zaid ya kutoa shutuma kuhus Israel but mbona kama umebadiri tu maneno but mantiki nilioisema ni hiyo hiyo na wewe umeirudia? Binafsi naoana mi na wewe tunao mtazamo 1 wa Mkwawa kujiua ( though bado nasisitiza kwamba suala la Mkwawa kujiua is still debatable cause we are not sure ) hi hilo hilo tu
 
Hivi hatuwezi kufungua mashitaka mahakama za kimataifa kuwashitaki hawa wajerumani kwa Uvamizi na mauaji ya watanganyika? Navyojua mimi kosa haliishi kama ni kwa karne 100 utalikuta lipo palepale hata kama muhusika utakufa.

Huu ulikuwa ni uhalifu dhidi ya binadamu - RIP Mkwawa!!
 
bila shaka ulieandika sio muafrika. au una weza kua sio pan Africanist au unaweza kua puppet wa mbuzi dume
 
bila shaka ulieandika sio muafrika. au una weza kua sio pan Africanist au unaweza kua puppet wa mbuzi dume
Hiyo hekima gani?? Mtu anayeuliza swali (ambalo hupendi) anahitaji ktukanwa ("puppet")???

Sikubaliani na mwanzilishaji wa tredi lakini kama hupo tayari kuheshimu wengine wanaochangia heri uondoke haraka.-
 
Shujaa ni mtu yeyote aliyewatetea watu wake walipokabiliwa na adui au janga.
Kwa mantiki hiyo kuna watu wanamuona Kinjekitile ni shujaa wao pia.
Kwanza kabla ya huu mjadala tupate maana halisi ya neno SHUJAA ili tujue kuwa tunamjadili kwa sifa zipi....??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…