Kulikuwa na uhalali gani kwa Chief Mkwawa kutambulika kama 'Shujaa?

Mungu unayemuabudu wewe, na yule aliyeabudiwa na wakoloni hakuwa mungu wa Mkwawa. Ungemuuliza Mkwawa mambo gani mungu wake anayakubali au kuyakataa ungeshangazwa sana na majibu yake.
Kujiua ni uoga wa maisha mkuu na waoga kamwe hawatauona ufalme wa Mungu. Mzalendo hajiua hata siku moja.
 
Shujaa ni mtu yeyote aliyewatetea watu wake walipokabiliwa na adui au janga.
Kwa mantiki hiyo kuna watu wanamuona Kinjekitile ni shujaa wao pia.
Kwani shujaa ni lazima awatete watu wengine? Vp kama akijitetea yeye mwenyewe, hawezi kuitwa shujaa? Samson alipambana na Simba mpaka akafanikiwa kumuua. Je, yeye sio shujaa? Can't he be declared a hero of his own sphere?
 
Mungu unayemuabudu wewe, na yule aliyeabudiwa na wakoloni hakuwa mungu wa Mkwawa. Ungemuuliza Mkwawa mambo gani mungu wake anayakubali au kuyakataa ungeshangazwa sana na majibu yake.
Umejuaje kama hakuwa Mungu wa Mkwawa. Ulimuuliza mkuu? Lini? Wapi? Muda gani? Twenda logically sasa.
 
Kwanza jiulize, why mkwawa alipigana?
Ni pride tu, kuwa yeye hawezi kutawaliwa na wazungu kamwe.
Na ngozi yake kamwe haitokuja guswa na Mzungu.
Ko kiufupi kwa hatua aliyokuwa amefikia ( aliwatandika wajerumani kwenye phase 1) ni shujaa tayari.
Na lengo lake lilitimia, mkwawa hajawahi guswa na wageni akiwa hai.
Mkwawa hakuwahi lipa kodi kwa wakoloni Bali aliitoza misafara ya vibaraka wao.
Mkwawa alijiua akiwa bado kazungukwa na askari wake wawili ( bodyguards) so hakulazimishwa ni option aliyoona inafaa kulinda Heshima yake, na heshima aliipata mpaka Leo hii mimi na wewe tunamjadili, why tusimjadili chief Mangungu
 
Mkwawa alijiua akiwa bado kazungukwa na askari wake wawili ( bodyguards) so hakulazimishwa ni option aliyoona inafaa kulinda Heshima yake, na heshima aliipata mpaka Leo hii mimi na wewe tunamjadili
Kujiua ni heshima mkuu? Vijana wanakata tamaa za maisha na kushindwa kuendelea kupambana nao unashauri wajiue ili walinde heshima zao?...
 
Hii pia hufanywa na wale wapiganaji shupavu wa Tamil Tigers akina Syvalassan ambao walikuwa wanatembea na vidonge vya sumu pindi wanapokamatwa hula kidonge ili waepuke kushurutishwa kutoa siri.
 
alipata matatizo ya akili mwishoni, akawa na paranoia, akahisi mtu yoyote anaweza kumsaliti. uwezo alikua nao mkubwa sana, historia uliyonayo wewe ni ndogo sana, fuatilizia zaidi
 
mkuu hebu tutolee mfano shujaa kwako ni nani?
 
Maswali yako mepesi sana.
Kwani shujaa ni lazima awatete watu wengine? Vp kama akijitetea yeye mwenyewe, hawezi kuitwa shujaa? Samson alipambana na Simba mpaka akafanikiwa kumuua. Je, yeye sio shujaa? Can't he be declared a hero of his own sphere?
 
Ushujaa wa Mkwawa hatuuangilii kwenye kifo chake angalia alivyowatoa jasho la sehemu za siri alimaarufu kama '' kantyentye ( Lufufu ) wajerumani kwa mfumo ule wa vita ya kuvizia ni dhahili alikua shujaa ila we Infantry Soldier we mjeda bhana
 
Huu ni muktadha tofauti, muktadha wa Vita mkuu.
Ni kawaida kwa warriors na wapambanaji kujiua kwa sababu wanazozijua wao na kwao hii ni heshima kubwa.
Mkuu, hivi unajua ya kuwa maisha pia ni vita na changamoto zake ndio adui yetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…