Kumbe Adamu alikuwa na mke zaidi ya Hawa?

Kumbe Adamu alikuwa na mke zaidi ya Hawa?

Aisee Mzee wa Upako amekuwa mlopokaji ni balaa! Atupe vitabu tusome anachosema.
 
Wakuu hii ni kwa mujibu wa nguli wa mambo ya imani mzee wa upako.

Anasema huyo mama yetu aliumbwa sambamba na Adamu

Jina lake aliitwa Lilith

Baadaye alizinguana na Adamu akasepa zake kwenda kuanzisha life yake solo nje ya bustani ya Eden.

Ndio ikabidi aumbwe Hawa kutoka ubavu wa Adamu

Sasa najiuliza mbona huku kitaa hatuambiwi habari hizi kwa uwazi na ukubwa wake kwanini habari hizi zinafichwafichwa kama bangi? shida nini hasa?

Na kwa wajuvi mtujuze huyu mama yetu wa mwanzo Lilith aliishia/alienda wapi?

Kumbe haya mambo ya watu kuzinguana yalianza toka dunia inaanza?

View attachment 3050156
mzee wa upako yupo sahihi kabisa according to holy bible.
 
Kamba tu hizo.
Mwanzo 1:27-28

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
 
mzee wa upako yupo sahihi kabisa according to holy bible.
Acheni upotoshaji. Huyo Mzee wa upako siku zake zimefika ndio maana anaropoka tu. Mara Yesu sio Mungu, mara Biblia sio neno la Mungu, mara make wa kwanza wa Adam hakuwa Hawa, endeleeni kupotoshwa.
 
Hivi ni lini akili zenu zitafuata logic? Evolution ndio logical explanation yenye ushahidi unaoonekana wazi wazi (evidence based).
 
Mwanzo 1:27-28

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Ukisoma biblia kama kasuku unaweza changanyikiwa.

Ndio maana makanisa yanayojitambua yanafundisha theology na kuna mpaka PHd.

Soma Biblia in a literal way na sio strict interpretation.
 
Acheni upotoshaji. Huyo Mzee wa upako siku zake zimefika ndio maana anaropoka tu. Mara Yesu sio Mungu, mara Biblia sio neno la Mungu, mara make wa kwanza wa Adam hakuwa Hawa, endeleeni kupotoshwa.
kwa hyo mke wa kwanza wa adam ni hawa?
 
Wewe ndio u some kwa kutulia. Acheni kupotosha maandiko.
kama biblia mwanzo 1 inasema Mungu alimuumba mwanadamu, mwanaume na mwanamke waliumbwa, mwanzo 2 inasema mwanamke alitoka ubavuni mwa mwanaume, na baada ya adam kukabidhiwa demu wake anashukuru na kusema "huyu sasa........." kama hakuwepo mwingine mwanzo kwa nn aseme huyu sasa.

upotoshaj uko wapi hapo?
 
Mwanzo 1:27-28

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
mwambie asome na mwanzo 2
 
Si kila Habari waambiwe watu wote only wanaofika level za juu tu za ujuzi na maarifa ili kuibalance dunia.
Hata hii Biblia ni Roman Catholic ndio walioamua kipi upewe wewe wa chini thus vitabu vingine vyenye siri mbali mbali vimefichwa maktaba za Vatican utakiwi wewe masikini kuzijua.
Unajua kitabu cha Enoko,unajua kuhusu miaka 18 ya Yesu iliyopotea kwann waliitoa wakakuachia only injili,
Kuna zaidi ya vitabu 300 havipo kwenye Biblia waliona yaliyomo ndio yanafaa vitabu vyote vingewekwa kwenye Biblia isingetosha na isingebebeka.
 
Ukisoma biblia kama kasuku unaweza changanyikiwa.

Ndio maana makanisa yanayojitambua yanafundisha theology na kuna mpaka PHd.

Soma Biblia in a literal way na sio strict interpretation.
kwa hyo biblia iliandikwa kwa ajili ya wanatheolojia wenye phd siyo?
 
Back
Top Bottom