Binafsi sipendi kuongelea watu na mambo ya wasanii lakini hili limenigusa sana sana.
Kama mnakumbuka namna mr Nice alivyokuwa akiishi maisha ya kuigiza,steven kanumba hivyo ivyo pamoja na wasanii wengine sikuua kama msanii mahiri kama Diamond akiingizwa katika ujinga huo huo na wasaka pesa.
Kutokana na ugomvi wa chini chini baina ya kundi la WCB na Clouds media hasa chanzo kikiwa ni mradi wa redio na tv..sasa akina kusaga wameweka wazi kuwa zile Karanga za Diamond Karanga ni mali ya kampuni ya Clouds na Diamond ni balozi tu.
Nimeumia sana,maana nimekuwa nikimuona diamond kama kijana anayesaka fursa licha ya kutokuwa na elimu ya kutosha.
Namuomba diamond afanye yake atatoboa badala ya maisha ya show.
--------------------\