GE2025 Kumbe INEC imechukukua orodha ya wapiga kura kutoka NIDA?

GE2025 Kumbe INEC imechukukua orodha ya wapiga kura kutoka NIDA?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Asa tume inayoongozwa na majaji kabisa wanashindwa hata kuandikisha wapiga kura jamani hadi wachukue ya nida??? This is shame!!
Wakichukua idadi ya kweli huenda hawafiki 5M 🤔
 
sahihi Kwa kutokujua au kujua nilijiuliza kwann uandikishaji uchukue muda mfupi kiasi kile kweli wikimoja! aise
 
Hili Suala siliangalii kwa njia ya hizi tamthiliya na Maigizo ya Demokrasia ambayo yanagharimu sana Kodi zetu...; Bali naliangalia kwa upotevu wa pesa; Kwanini kuwepo na Daftari la wapiga Kura ? Kwanini isiwepo NIDA ambayo inaonyesha mtu ambaye ni eligible hivyo kama ana umri husika basi ni Haki yake akitaka kupiga Kura..., Na siku akifa automatically ananyofolewa kwenye NIDA kutokana na Taarifa zake kuwepo RITA in short NIDA iwe subset ya RITA
 
Nilitaka kushangaa ile idadi ya wapigakura wa mwaka huu 2025 iwe kubwa vile, kumbe jamaa wameungamisha INEC, CCM na NIDA vyote vipo kwenye kitu kimoja!! Yaani ukitaka details wao wanacopy tu!!

Yaani kupiga kura nchi hii ni Kwa upuuzi wako tu!!
Yaani mkuu kwa kifupi ni kwamba...
Hata kama hujajiandikisha...jina lako lipo kwenye daftari la kupiga kura sehemu flani...
Sasa ili kuhalalisha Uchaguzi kwamba watu wengi sana walipiga kura...

Wewe utapigishwa kura bila kujua..
Kwakuwa Wana details zako...wao ni kujaza tuu na kuweka tick...wakija waangalizi sijui wa kimataifa wanaonyeshwa watanzania wengi wamejitokeza na CCM imeshinda kwa 91%
 
Kwa kweli nilishangaa sana pale Tume ya Uchaguzi ilipotangaza ya kwamba wapiga kura waliojiandikisha ni milioni 37 na ushee. Nikashangaa Sana.

Ila Leo nimegundua ya kwamba INEC imechukua takwimu au orodha ya watu waliopo kwenye mfumo wa NIDA na kuwafanya kwamba ndio wapiga kura wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.

Ninaiomba Tume ya Uchaguzi ilete takwimu sahihi ya waliojiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.
CCM inawafanya watanzania hawana akili kabisa, kasoro familia zao tu
 
Kwa kweli nilishangaa sana pale Tume ya Uchaguzi ilipotangaza ya kwamba wapiga kura waliojiandikisha ni milioni 37 na ushee. Nikashangaa Sana.

Ila Leo nimegundua ya kwamba INEC imechukua takwimu au orodha ya watu waliopo kwenye mfumo wa NIDA na kuwafanya kwamba ndio wapiga kura wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.

Ninaiomba Tume ya Uchaguzi ilete takwimu sahihi ya waliojiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.
Mzee wa flyover kila mahali ametema nyongo na ndio kweli!! Vinyambilisi vya buku saba humu vinahangaika kama mtetea anaetaka kutaga ili kuzima hii ishu!!!
 
Kwa kweli nilishangaa sana pale Tume ya Uchaguzi ilipotangaza ya kwamba wapiga kura waliojiandikisha ni milioni 37 na ushee. Nikashangaa Sana.

Ila Leo nimegundua ya kwamba INEC imechukua takwimu au orodha ya watu waliopo kwenye mfumo wa NIDA na kuwafanya kwamba ndio wapiga kura wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.

Ninaiomba Tume ya Uchaguzi ilete takwimu sahihi ya waliojiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.
Kuleta idadi halisi ya waliojiandikisha haiwezekani, hapa tulipo , mfumo uchunguzwe na wataalamu waliobobea kwanza pili zoezi la kuandikisha ukiambatana na kufanyika reforms unatakiwa kuanza upya ,uchaguzi usogezwe mbele ,Taifa kwanza mambo mengine badae
 
Chanzo Cha huo ugonjwa wa ukiki,je unaambukizwa na mbu?Na tiba yake ni Nini(UKIKI)?!
Haaaaah...haaah...sijajua hao wahuni wenzake wa mitandaoni. Wanasema ni Upungufu mkali wa Kinga Kichwani (UKIKI).
 
Nawezaje kuwa mwandishi wa habari bongo ndugu yangu? Mimi hasla tu kama wewe.
Kuna somebody Semtawa kwenye gazeti la mwananchi ndio maana nikakuuliza maana nilishangaa kama ni journalist unawezaje kuamini fubricate news kama hiyo?
 
Kuna somebody Semtawa kwenye gazeti la mwananchi ndio maana nikakuuliza maana nilishangaa kama ni journalist unawezaje kuamini fubricate news kama hiyo?
Hapana. Majina tu ndugu yangu. Halafu hizo jarida nilihoji nilichokiona nikasema wahuni wenzie Polepole mitandaoni.
 
Jukumu la kuondoa waliopoteza sifa za kupiga kura(mfano waliofariki n.k) ni la jamii husika kuanzisha michakato huo wa kuomba kufuta, Sasa kama jamii haitaanzisha mchakato iNEC hawawezi kurupuka tu wakafuta taarifa

Kwamba vizazi na vifo havirekodiwi?
 
Jukumu la kuondoa waliopoteza sifa za kupiga kura(mfano waliofariki n.k) ni la jamii husika kuanzisha michakato huo wa kuomba kufuta, Sasa kama jamii haitaanzisha mchakato iNEC hawawezi kurupuka tu wakafuta taarifa
Hilo ni jukumu la mamlaka inayosajili vizazi na vifo!. Kama mchakato wake unahusisha kutoa cheti cha kifo kabla ya mazishi, Tume ya Taifa ya uchaguzi wanapaswa kusomana na RITA wakati wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
Kitendo cha Tume kukopi orodha ya watu na kuwa ingiza kwenye daftari la wapigakura bila kufanya uhakiki ndio uhuni wenyewe unaopigiwa kelele.
 
Back
Top Bottom