Kumbe kumwaga chini mbegu ya uzazi, ni kosa kubwa sawa na kuua!

Kumbe kumwaga chini mbegu ya uzazi, ni kosa kubwa sawa na kuua!

Sio kosa kumwaga chini ila hakufuata maelekezo yeye kaambiwa akalale na mwanamke wa marehemu ili azae nae, kaenda kaenda kulala nae ila akamwagia nje Mungu aka-mmada😁😁😁
 
Sio kosa kumwaga chini ila hakufuata maelekezo yeye kaambiwa akalale na mwanamke wa marehemu ili azae nae, kaenda kaenda kulala nae ila akamwagia nje Mungu aka-mmada😁😁😁
Sawa,jiteteeni tu
 
Ni kitabu cha Mwanzo 38:6-10 neno linasema hivi:

6. Baadaye Yuda alimwoza mtoto wake wa kwanza Eri, kwa mwanamke aitwaye Tamari.

7. Lakini Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; hivyo Mwenyezi-Mungu akamuua.

8. Basi, Yuda akamwambia Onani, “Mchukue mke wa ndugu yako marehemu, kwani ndivyo inavyokupasa kufanya, upate kumzalia nduguyo watoto.”

9. Lakini Onani alijua kwamba hao watoto wasingekuwa wake. Kwa hiyo, alipolala na mke wa nduguye, alimwaga chini mbegu ya uzazi, asije akampatia nduguye watoto.

10. Tendo hilo likamwudhi Mwenyezi-Mungu, akamuua Onani pia.

😳Kumwagia nje hizo mbegu kumbe ni chukizo mbele ya Mwenyezi Mungu wajameni?🤦
Sio kweli.
Soma tena, hao walimwaga chini kwa hila ili kutomzalia ndugu yao mrithi jambo ambalo lilimchukiza Mungu
 
Sio kweli.
Soma tena, hao walimwaga chini kwa hila ili kutomzalia ndugu yao mrithi jambo ambalo lilimchukiza Mungu
Yaan iwe Hila isiwe hila...ukitema tu uji unacho😜
 
Kuelewa ni kitu muhimu, aliadhibiwa kwa kukiuka maagizo, sio kumwaga mbegu chini.
 
Huyo jamaa alikaidi kitendo Cha kutokusababisha ujauzito Kwa huyo Mke wa ndugu yake, alikaidi maagizo.

Kama kosa lake ingekua kumwaga mbegu nje, zile siku zote mnakutana kimwili kama hazisababishi ujauzito ingekua ni dhambi vile vile.
 
Back
Top Bottom